Mtunzi: __
SEHEMU YA THELATHINI NA NANE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Usiku nilishituka usingizini baada ya mbu kuning’aata na kunisumbua sana. Niliwachukia sana hao mbu kwa sababu walinikatisha ndoto yangu ambayo nilikuwa nikiota.Ndoto ilikuwa ikielezea jinsi harusi yangu na Mark itakavyokuwa. Ndoto ilikuwa tamu sana maana ilinipa taswira ya picha halisi ya maisha yangu ya mbeleni.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Nilishusha neti na kurudi kulala zangu huku nikitamani ndoto ile ijirudie. Ile ndoto ya harusi yetu mimi na Mark haikujirudia na badala yake niliota ndoto ambayo ilinikosesha raha siku iliyofuata.
Niliota kuwa kwenye lile shamaba la marehemu baba yangu ambapo ndo madini yalihifadhiwa kuna mtu alijenga na aliamua kuliamisha lile kaburi. Ndoto iliniweka njia panda kwa sababu haikueleza kuwa yale madini yaliiibiwa au la. Sikujua ile ndoto ilikuwa na maana gani ila kwa kweli ilinishitua sana na kuhisi labda yale madini hayapo tena sehemu salama. Siku hiyo ilikuwa mbaya sana kwangu kwa sababu ya mawazo ya madini niliyokuwa nayo.Nikajikuta siku hiyo inaisha bila kumtafuta Eliado kwa ajili ya ile stori itakayotengeneza filamu itakayoitwa Let Me Love You.Usiku Mark alinipigia na kuniuliza kama nimeshapata hiyo stori ambayo itatengeneza script ya filamu ambayo kwa namna moja au nyingine itaelezea maisha yetu ya kimapenzi.
Basi nikaona isiwe tabu ngoja nilifanyie kazi wazo la Mark ili mradi yeye si ana taka shorti stori tu kisha mambo mengine atafanya yeye. Kwa kiherehere kabla sijamtafuta Eliado nilijaribu kutunga kwa uwezo wangu na niliposhindwa ndo nilinyanyua simu na kumpigia. “Halow, helow vipi habari za siku nyingi” nzuri sana sijui ni nani mwenzangu aliuliza mwandishi huyo mara baada ya kupokea simu yangu. Jamani umenisahau niliamua kumlegezea sauti ili tu kumdatisha kidogo. “Siunajua mimi na marafiki wengi sana hivyo ni vizuri ungejitambulisha alisema mwandishi huyo kwa kujiamini.” “OK, mimi naitwa Leah kuna kipindi nilikutafuta ukanisaidia sana kunishauri kuhusu maisha yangu ya kimapenzi ambayo kwa kipindi hicho yalikuwa yamepoteza dira.
Basi akanambia karibu na ananisikiliza. Nilianza kwa kumwambi kuwa “sasa leo sitaki ushauri wa mapenzi wala nini bali ninachotaka ni unitungie kastori kafupi sana kanachoitwa LET ME LOVE YOU.Alafu sasa stori hiyo ndo nitampelekea mchumba wangu ili tuandae filamu ambayo itaelezea maisha yetu ya mapenzi. Kwa hiyo unataka hiyo stori iweje aliniuliza mwandishi huyo.Mimi sina idea yeyote na ndio maana nikakutafute wewe ilinibidi niwe mkweli. Cha msingi ni kwamba isiwe ndefu tukashindwa kuigiza kwa mtindo wa filamu. Kuhusu malipo wewe usijali wewe fanya kazi ilinibidi nimuhakikishie ulaji mara baada ya kuniuliza swali hilo la malipo.
Akanambia nimpe lisaa limoja atakuwa amekamilisha swala hilo.Ilinibidi nishangae yaani lisaa limoja tu atakuwa tayari ameshatunga hiyo stori wakati mimi
Mark alinipa kazi hiyo tangia juzi na sikuweza,Nikaseama kweli muache mungu aitwe mungu kwani ameumba watu wenye vipaji mbali mbali. Nikaendelea na shughuli zangu huku na mimi nikijaribu kuvuta taswira ya hiyo Let Me Love You ili nikitumiwa nione kama iatendana na yangu au ndo nitaendelea kuwa kilaza kwa upande wa fani za watu. Kweli huyu ni kiboko maana hata kabla ya lisaa alilosema kuisha yaani ndani ya dakika kumi tu alinitumia meseji na kuniambia nifungue email yangu tayari ameshafanya yake.Kwa kihoro cha kutaka kujua aliandika nini ndani ya mda mfupi huo nilichukua tablet yangu na kufungua email yangu na kuanza kuisoma hiyo stori.Mistari miwili ya mwanzo tu ilinivutia na hako kastori kalisomeka hivi.
“Licha ya mali na utajiri aliokuwa nao kijana Jimmy bado alipenda kujishusha na kuishi maisha ya kawaida. Kuna wakati alikuwa akiamua kuacha usafiri wake wa kifahari na kuamua kutembea kwa miguu. Zoezi la kutembea kwa miguu huwa analifanya karibu kila wiki huku akiamini kuwa ni moja ya sehemu ya mazoezi ya mwili.
Jimmy akiwa katika matembezi yake ya jioni ya siku ya valentine day anamuona binti mmoja akiwa mbele yakee huku akitembea kwa mwendo wa taratibu sana lakini alikuwa upande wa pili wa barabara.Tofauti na watu wengi ambao uvalia nguo nyeusi siku hiyi special kwa wapendanao binti huyo alivalia nguo nyeusi.
Ghafla moyo wa Jimmy unazizima kutokana na uzuri wa binti huyo. Ingawa Jimmy alikuwa akitembea kwa miguu lakini alijiuliza kwa nini binti mrembo kama huyo aliamua kutembea kwa miguu.Akajikuta amechanagnyikiwa kwa sababu umbo, suara na muonekano wa binti huyo ndo vilikuwa vigezo vya mwanamke ambaye siku moja angependa kuja kumuoa. Mwenyewe alimuita “the girl of my dream” yaani msichana wa ndoto zake.
Bila kutarajia Jimmy akajikuta amevuka upande wa pili wa barabara na kuanza kutembea nyuma ya msichana huyo.Jimmy alipunguza mwendo huku akiendelea kuburudishwa vyema na mjilindimo ya makalio ya binti huyo ambayo yalijazia vizuri na kufanya milindimo ambayo imgempa shida mwanaume yeyote mwenye tamaa. Jimmy pamoja na ujanja wake wote lakini bado alishindwa kuelewa ni vipi atamwingilia binti huyo nakuanza kuongea nae.Akajikuta akiendelea kumsindikiza na kuendelea matembezi tofauti kabisa na njia ambayo yeye alitaka kuipita
Kwa haraka haraka akawaza kuwa huenda binti huyo angefika sehemu aliyokuwa akienda bila hata ya yeye kumsemesha. Jimmy akaamua kujikaza kisabuni na kupiga hatua za haraka haraka na kumsogelea mrembo huyo.Bila kutarajia Jimmy akajikuata anaropoka “dada habari”.Yule dada aligeuza shingo yake kama twiga mwituni kisha akamuangalia Jimmy kuanzia juu mpaka chini alafu hakujibu salamu hiyo akanyamaza kimya akarudisha shingo yake na kuendeleaa na safari yake.Jimmy alijikuta akiishiwa ujanja na kujikuta akirudia tena kutoa salamu kwa kumwambia “dada nakusalimia”. Yule dada akafanya kama mwanzo yaani kugeuza shingo kumwangalia chini mpaka juu a kukaa kimya huku akianza kuongeza mwendo.
Jimmy akawa ameishiwa mbinu akaamua kunyamaza kimya na kuendelea kutembea pembeni ya mrembo huyo.Wakaendelea na matembezii yao kama vile watu waliokuwa wakijuana ila waliamua kuwa mabubu tu.Wakafika makutano ya barabara hapo yule binti mrembo akavuka barabara na kwenda ng’ambo ya pili.
Jimmy akakata tamaa na kuamua kurudi zake alipotoka, akageuka zake huku akimsindikiza yule mrembo kwa macho. Akaanza kupiga hatua kurudi alipotoka lakini bado roho yake ilipingana na mwili na akili yake kutokana na maamuzi hayo ya kukubali kushindwa.Akajikuta akijisemea kwa nguvu “No I cant tolerant any more, she is a girl of my dream,LET ME LOVE YOU.(Hapana siwezi kuendelea kuvumilia, ni msichana wa ndoto zangu, wacha tu nimpende)
Jimmy akajikuta anavuka barabara kwa nguvu bila kuangalia kushoto na kulia.Piipiii pipiiiiiii piiiiiii, paaaaaah paaaaaah haaaaaaaaa ni mlio wa honi ya gari ndogo aina ya spaciao new model ambao uliambatana na kishindo kuashiria kuwa kuna ajali mbaya ilitokea.Mlio huo na mshindo vilimshitua yule dada ambaye Jimmy alikuwa akimfuatilia.Tofauti na Watanzania wengine waliojaliwa roho ya utu, upendo na huruma dereva aliyemgonga Jimmy hakusimama na badala yake aligeuza gari yake na kutimua mbio. Binti yule mrembo aliingiwa na huruma na kujikuta akiaamua kumsaidia Jimmy. Binti wa watu alichanganyikiwa mara baada ya zoezi lake la kupungia mkono magari kushindikana kwa sababu magari yote yalikuwa yakipita kwa kasi. Binti huyo ikambidi atumie mbinu za kike kwa kusimama katikati ya barabara na kuanza kupiga piga miguu kama mtu aliyechanganyikiwa.Hapo alifanikiwa kupata msaada na kumkimbiza Jimmy hospitali.Binti huyo hakuweza kumuacha Jimmy mweneyewe pale hospitali hivyo akajikuta anamwangalia mpaka hapo hali yake itakapokuwa nzuri.
Jimmy alikuja kupata ufahamu na kushituka kutoka usingizni na kujikuta akizungukwa na dripu za damu na maji.Alipoangalia pembeni akakutana na tabasamu zito la binti mrembo ambaye alikuwa pembeni yake. Jimmy akauliza kwa sauti hapa nipo wapi? Yule binti akamuangalia kwa huruma kisha akatabasamu na kumwambia relax ulipata ajali ndo maana upo hapa hospitalini.Huo ndo ukawa mwanzo wa Jimmy kujuana na binti huyo.Kujuana huko kukapelekea wote wawili kuzama kwenye dimdwi zito lenye matope mekundu na yenye umbo la moyo yaani mapenzi.
Stori hiyo ya Eliado ilishi hapo ikabidi nimpigie na kumuuliza mbona sasa ameikatisha stori na imekuaje ameitunga kwa mda mfupi hivyo yaani dakika kumi tu.Hapo Eliado akacheka na kuniambia hiyo stori ilikua kwenye library yake na inaitwa “THE GIRL OF MY DREAM” Hivyo amaikata kipande cha mwanzo wa stori hiyo na kunitumia kwa sababu anaamini kuwa kama filamu yetu itaanza kwa mtindo huo itakuwa inavutia sana watazamaji.Ikabidi nikubaliane na yeye ndio itavutia sana kwa sababu ndo itakuwa ni mwazno wa mapenzi ya watu wawili sasa nini kitafuata baada ya hapo ilibidi nimuulize swali hilo maana bado aliniacha njia panda.
Akacheka kwanza na kuniambia mbona simple sana kinachofuata hapo ni huyo bint mrembo ambaye ndo kwenye filamu utakuwa wewe kuleza historia yake ya mapenzi ambayo ni mbaya sana na ya kukatisha tamaa na inayosababisha wewe kuchukia wanaume na kutowaamini kabisa. alafu Jimmy ataeleza kwa nini alivutiwa na kupagawa na wewe mara baada ya kukutana na wewe siku ile ya kwanza. Kwa hiyo ili filamu iwe tamu itakuonesha wew na matukio yako ya nyuma na Jimmy na matukio yake ya nyuma na itafafanua kwanini Jimmy anakuona wewe ni msichana wa ndoto zake.
Kwa hiyo hilo jina lenu litaingia kwa sababu kutokana na maisha ya kuumizwa kimapenzi aliyopitia Jimmy na kujikuta anawachukia wanawake na anajikuta wewe ndo uanweza kuziba pengo hilo hivyo kupelekea “LET ME LOVE YOU” na wewe ulikuwa huna mpango wa kumpenda mwanaume lakini kutokana na upendo aliokuonesha mwanaume huyo hauna jinsi LET YOU LOVE HIM. Alitoa ufafanuzi mtunzi huyo ufafanuzi ambao ulinifurahisha sana.Ikabidi nimwagie sifa kem kem na ilibidi nimuulize “umesema kipande hiki umekitoa kwenye stori yako inayoitwa THE GIRL OF MY DREAM, je haitaleta shida sisi tukiktumia.
Akanambia haina shida kwa sababu kwenye sehemu ya story writer tuataweka jina lake. Alisistiza kuwa hiyo sio mara yake ya kwanza kuhusishwa kenye filamu hivyo itakuwa pia ni mwanzo mzuri wa sisi na yeye kufanya kazi. Basi tukakubaliana kufanya kazi hiyo pamoja na atatusaidia kuendeleza matukio ya stori hiyo.
Nilikuwa na furaha sana huku nikiamini kuwa ndoto zangu za kuja kuwa mtu maarufu zinaweza kufanikiwa hata kabla ya kuyapata yale madini. Sikutaka mbwembwe niliamua kuikopi na kuipesti hiyo stori kama ilivyo na kuifowadi kwa Mark.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO