Mtunzi: __
SEHEMU YA THELATHINI NA TISA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Nilikuwa na furaha sana huku nikiamini kuwa ndoto zangu za kuja kuwa mtu maarufu zinaweza kufanikiwa hata kabla ya kuyapata yale madini. Sikutaka mbwembwe niliamua kuikopi na kuipesti hiyo stori kama ilivyo na kuifowadi kwa Mark.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Baada ya kama lisaa hivi Mark alipiga na kuniuliza kama kweli ilikuwa nai mimi nimetunga hiyo stori.Nikamwambia ndo mimi kwani mimi siwezi kutunga stori.
Akanambia sio kwamba siwezi lakini ile idea ilikuwa nzuri sana na mtu mwenye utaalamu wa uandishi ndo anaweza kubuni vitu kama hivyo.Nikakomaaa na msimamo wangu kuwa ni mimi ndo nimetunga nia yangu ni kupata maujiko ya bure.Tuliongea ongea kwenye simu na baadae alikata simu na kuniacha mimi niendelea na mambo yangu mengine.
Maisha yaliendelea huku nikimsubiri wanaume huyo kwa hamu na jamu kwa sababu alinambia atakuja moshi hivi karibuni.Baada ya miezi miwili Mark alikuja Moshi na kama kawaida yake alikuja kazini kwangu.Nilimuomba anipe mda kidogo ili niweze kuweka mambo yangu sawa kabla sijawaachia majukumu yote hao mabinti wa hapo saloon. Sijui kwa nini huyu mwanaume alikuwa anapenda kuja sana kazini kwangu.Niliweka mambo yangu sawa na baada ya hapo nilienda nyumbani kujiandaa tayari kwa kuwa na mwanaume huyo ambAye kwa wakati alikuwa akitawala sana ubongo wangu na hisia zangu.Yaani siku hiyo nilijikuta namwaga nguo zote kitandani ili kutafuta nguo ambayo itakuwa ni funiko na kunifanya nionekane binti mdogo mbichi anayechipukia.
Nikampiga na alinielekeza nimkute kwenye hoteli niliyofikia. Na nilivyofika hapo hata hatukukaa sana alinambia kuwa kuna marafiki zake wanamsubiri mahali. Aliwapigia simu na wakamwambia tumkute sehemu inayoitwa Mercury.Tuliingia kwenye gari na kuelekea hiyo sehemu.Sikujua hata hilo gari alilipata wapi lakini sikutaka kumuuliza kwa sababu nilijua kwa umaarufu wake lazima alikuwa na marafiki wake wenye uwezo watakuwa wamemwazimisha.Tulifika eneo hilo na tulikuta kuna shangwe utafikiri kama vile kulikuwa na sherehe. Yaani huyu mwanaume alikuwa na marafiki wengi sana utafikiri ni kijiji. Lakini nikajuiliza mbona paliandaliwa kama vile palikuwa na kitafrija kidogo. Yaani nilipokelewa kama malkia na watu wote walisimama na kuimba wimbo wa karibu shemeji.Ilikuwa ni bonge la surprise kwa kweli sikujua kama ninaweza kupewa heshima kubwa kiasi hicho.
Niliona pia makameraman ambao walikuwa wakichukua tukio hilo. Kumbe siku hiyo ndo ilikuwa ni siku rasmi ya mimi kutambulishwa kwa marafiki zake.Kulikuwa na watu kama 15 tu lakini kulikuwa na shangwe ya kufa mtu.Na tulivyokaa MC alimuomba Mark asimame na kutoa utambulisho.Mark hakuwa muongeaji sana aksimama na kusema “Ndugu zangu part yetu sio ya kuongea bali ni ya kula na kunywa hivyo basi nitaomba vitendo vitawale sana kuliko maneno.Leo ni siku muhimu sana ambapo nitawadhihirishia marafiki zangu kuwa nimepata mchumba ambaye tutaanza safari ya kuelekea maisha ya ndoa.Kwa kifupi leo nitamvalisha pete mpenzi wangu na kumthibitishia kuwa ninampenda na kumuamini.
Mark baada ya kusema maneno hayo akatoa pete ya gold ambayo ilikuwa inametameta na kunivalisha. Haikuwa pete ya ndoa bali ilikuwa ni pete ya uchumba na nilishindwa kuvumilia nilifurahi sana na machozi ya furaha yalinitoka.Pete ile utafikiri ilipimwa vile kwani ilinifiti vizuri sana kwenye kidole changu. Basi tuliendelea na party yetu huku vicheko vituko na burudani ikiendelea.Kuna mwanaume mmoja alikuwa akinichekesha sana kwani mda wote yeye alikuwa bize akinikonyeza. Sasa sijui pombe zilikuwa zimemkolea au alikuwa akimaanisha.
*********
*************
********************
Mark akaendelea kujitapa kuwa yeye huwa habahatishi katika kukamilisha mambo yake kwani binti huyo licha ya kusomea mambo hayo ya urembo pia ni mzoefu na ni dada binamu yake.Akanambia kesho dada huyo atapanda ndege kutoka Dar na kuja Moshi kwa ajili ya kazi hiyo. Akanileza pia kuwa amepanga kuwa nitakuwa na binti huyo kwa mda wa wiki moja ili kumuelekeza mazingira ya hapo salooni kwangu. Sikutaka kumpinga kwa sababu alionesha kuwa alishajipanga sana kuhakikisha hayo yote yanafanikiwa. Pia nisingeweza kutia neno lolote mpaka hapo nitakapo muona huyo Husna ambaye alikuwa akizungumziwa.
Mark akaendelea kujitapa kuwa yeye huwa habahatishi katika kukamilisha mambo yake kwani binti huyo licha ya kusomea mambo hayo ya urembo pia ni mzoefu na ni dada binamu yake.Akanambia kesho dada huyo atapanda ndege kutoka Dar na kuja Moshi kwa ajili ya kazi hiyo. Akanileza pia kuwa amepanga kuwa nitakuwa na binti huyo kwa mda wa wiki moja ili kumuelekeza mazingira ya hapo salooni kwangu.Sikutaka kumpinga kwa sababu alionesha kuwa alishajipanga sana kuhakikisha hayo yote yanafanikiwa. Pia nisingeweza kutia neno lolote mpaka hapo nitakapo muona huyo Husna ambaye alikuwa akizungumziwa.
Hapo pia alitumia hiyo nafasi kuniulizia zaidi ile idea ya stori ya filamu niliyomtumia. Ilibidi nimwambie tu ukweli kuwa ile idea ni ya Eliado mtunzi maarufu wa love stories.Basi akanambia haina shida kwa sababu na yeye yupo kwenye sanaa na hiyo idea ni nzuri na ameipenda hivyo basi anaomba siku inayofuata tufanye mpango tuonanae naye hili tuone tunachanganya vipi idea ili tuweze kupata kitu kizuri zaidi. Kwa kuwa tulikuwa tumechoka sana tulijikuta tumepitiwa na usingizi na kulala fofofoo. Hata yale mawazo yangu kuwa eti usiku nitampandishia mapaja ili adate na kunitimizai haki yangu hayakufanikiwa tena. Maana nilikaaj kushituka ilikuwa tayari pameshakucha.Kweli huyu mwanaume ni kiboko maana tulilala mpaka asubuhi bila kufanya lolote.Hii inanikumbusha ile siku ya kwanza kabisa ya mimi na yeye kuonana.
Kwa hiyo siku ndo ikawa imenza hivyo.Nilitamani nisiende kazini lakini sikuwa na jinsi ilinibidi niende tu japo kwa kuchelewa.Nilimuaga na kumuacha Mark akiendelea kuupiga usingizi. Cha ajabu tofauti na nilivyotarajia siku hiyo kuwa nitakua boadi kwa sababu Mark alishindwa kutoa maugwadu yangu niliyoyarundika kwa mda mrefu siku hiyo nilijihisi mweneye furahaa sana. Kitu kilichokuwa kinanipa sababu za kutabasamu ni yale mawazo mazuri ya Mark mawazo yenye tija, chachu na shauku ya maendeleo.
Niliingia kazini na kabla ya mambo yeyote niliamua kumpigia Eliado ili kumuomba appointment ya kuonana naye ili tupange vizuri kuhusu script ya filamu.Basi alinambia kuwa asubuhi yupo bize sana ila tunaweza kuonana kuanzai mida ya saa nane mpaka saa kumi jioni. Na nilimuuliza tutaonana wapi akanambia itakuwa vizuri kama tuataenda ofisini kwake. Ikabdi mimi niendeleee na shughuli za hapo saluuni huku nikitafuata njia ya kuwatoroka ili niende nyumbani nikapumzike kwa sababu siku hiyo nilikuwa nimechoka sana. Nilizugazuga hapo mpaka saa tano kabla ya kumuaga Waridi na kumuambia kuwa sijisikiii vizuri hivyo naenda kupumzika tuataonana jioni. Waridi kama kawaida yake hakuacha kutia neno akanambia kuwa ni haki yangu kwenda kupumzika kwa sababu inaelekea kazi ya jana usiku na Mark ilikuwa ni kubwa sana.Ilinibidi nicheke na kusema laiti angejua kilichotokea usiku huu anagenyamaza tu kimya.
Nilienda ghetto kwangu na kulala na nilikuja kushituka saa saba mara baada Mark kunipigia na kuniuliza tunaenda kula wapi. Nikamwambia popote anapotaka yeye ila mimi niko nyumbani anifuate hapo.Basi mda mchache baadaye alifika hapo akiwa na gari ya rafiki yake. Tuliondoka na kwenda sehemu moja inayoitwa changbay na hapo tulipata msosi wa nguvu na baada ya hapo tulienda moja kwa moja kwenye ofisi ya Eliado ambayo ilikuwa katikati ya mji.Tulifika na tulimkuta akiwa na mteja wake ambaye nazani alikuwa akimpa ushauri.Alituambia anatuomba tumpe kama dakika 15 hivi kisha atamalizana na huyo mteja kisha atakuja kuonana na sisi.Kweli baada yam da huo tulionana na kila mtu alikuwa na furaha sana kuonana na mwenzake.
Tulisalimiana na moja kwa moja tukaanza kujadili kilichotupelaka pale.Mark alimuuelza kuwa amefurahishwa sana na mwanzo mzuri wa ile stori lakini pia angependa kujua nini kingefuata mara baada ya Jimmy na Yule binti mrembo kuonana. “Ujue Mark kwa uzoefu wangu filamu ambazo zinaelezea maisha ya watu wawili huwa zinavutia sana kama tu kutakuwa na flashback ya kila mmoja wao.Kwa sababu title yenu inasema LET ME LOVE YOU hapo ina maana kuwa lazima kuwe na sababu za wahusika kufikia hatua hiyo na sababu ya msingi ninayoiona mimi ni historia ngumu ya mapenzi ambayo kila muhusika atapitia kabla ya kuyachukia mapenzi.Lakini pamoja na historia hiyo bado anapata mtu ambaye anampenda na anampa sababu za kusema LET ME LOVE YOU. Aliendela kufafanua Mr Eliado ufafanuzi ambao ulimfanya Mark kutingisha kichwa kuonesha anakubaliana na hiyo idea asilimia mia moja.
Mark akasema haoni haja ya kutafuta zaidi cha msingi yeye ataenda kuiandikia hiyo stori script ya filamu jinsi itakavyokuwa na jinsi wahusika watakavyoicheza. Eliado alisema pia kama idea hiyo itakuwa ngumu basi tumpe mda atunge stori ingine ambayo itakuwa rahisi kidogo kucheza.Hapo Mark akasema hii ni nzuri sana labda kama utatutungia ya filamu ingine ila hii mimi nimeikubali kwa zaidi ya mia moja. Basi kwa kuwa mwandishi huyo alikuwa na kazi nyingi sana tulifanya makubaliano ambayo yalihusisha malipo na Mark kwa jinsi alivyokuwa amemkubali alimuandikia cheque na kumwambia hiyo ni advance tu atampa asilimia kumi ya malipo ya filamu mara baada ya kuingia sokoni.Mark nilimpendea hapo kwa sababu siku zote alipenda kugawa riziki kwa watu wengi. Na siku zote mimi na amini kuwa ili ufanikiwe lazima ukubali kushirikiana na watu wengine tena kwa kuwapa hicho kidogo utakachopata.
Tuliaga na kuondoka zetu na tayari yule dada niliyeambiwa kuwa amepanda ndege kutoka Dar es salaam kuja Moshi kwa ajili ya kusimamia kazi ya saloooni alikuwa ameshafika hivyo tukapitia stendi kumpokea. Jamani mwacheni mungu aitwe mungu huyu dada alikuwa ni mrembo sana mapka nikamtamani.Alikuwa ni mwembamba mrefu na pia mwenye sura nyembamba kama mdoli. Alijaliwa macho ya kipekee sana na sauti yake ndo ilinifurahisha zaidi yaani utafikiri ya mtoto mdogo. Halafu alikuwa na babaface na mambo ya kizungu zungu hivi.Akitembea ndo utapenda hayo madaha yake utafikiri twiga anayetafuta maji au nyasi laini. Alikuwa akinyata kwa kweli. Kweli hata mimi nilimkubali tu siku ya kwanza ingawa bado nilikuwa sijajua ufanisi wake wa kazi.
Nilikaa nae hapo kwangu kwa mda wa siki tatu huku asubuhi tukiamka na kuendelea na kazi.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO