Mtunzi: __
SEHEMU YA AROBAINI NA SITA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Nilikuwa kama niliyepigwa butwaa nisiamini nilichokuwa nakiona mbele yangu. Oooooh my God hold me on yalikuwa ni maneno yaliyonitoka kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu mara baada ya kumuona James kwa uzuri zaidi na kuamini kuwa yule kweli alikuwa ni kaka yangu.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Nilishindwa kuelewa nini kimetokea mpaka yeye kurudi katika hali yake ya kawaida.Maana alikuwa anavutia alikuwa anapendeza na hata huyo binti aliyepanda naye alikuwa amependeza sana.
Kitu cha kwanza alichokifanya ni kunifuata na kunikumbatia.Nililia machozi ya furaha na hakuna alieongea neno.Tulikumbatiana kwa mda mrefu sana kabla ya kuachiana. Najua huwezi amini lakini hiii ni dunia na mungu pekee ndiye ajuaye maisha ya mwanadamu mwanzo na mwisho wake alisema James. Kisha akanikabidhi ile picha ambayo ilituonesha sisi tukiwa wadogo yaani mimi yeye baba na mama.
Nilishindwa kuelewa picha hiyo aliipata wapi kwa maana yeye alivyochanganyikiwa hakuwa na hata uwezo wa kuchukua kitu chochote.Hapo kumbukumbu zangu zilinijia kuwa marehemu baba yangu alinambia katika yale madini aliyoyaficha kule shambani ndani ya kiboksi aliweka picha ambayo ilionesha watu ambao wanatakiwa wanufaike na madini hayo.Kwa hiyo picha hizo zilikuwa mbili moja ndo hiyo na nyingine nilikuwa nayo mimi.
Na nakumbuka siku naingia kwenye jumba hilo la Big brother walikataa nisiingie nayo hivyo nilimkabidhi Lilian.Wakati bado naendelea kuitafakari ile picha na wosia wa baba kuwa nikipata yale madini nihakikishe kuwa watu hao nawatafuta na kuyafufua matumaini ya maisha yao. Kweli ilikuwa ni surprise nikachukua mike na kusema Lilian popote ulipo tafadhali naomba uniletee picha yangu.Haikuchukua hata dakika Lilian alionekana kwenye screen kubwa akiiletea hiyo picha yangu. Mungu wangu ni kweli zilikuwa zinafanana hivyo nilizi kubaki njia panda nisijue nini cha kufanya.
Nilishindwa kuelewa na sikutaka kuamini kuwa kaka yangu huyo alikwenda kule shambani na kuyafukua yale madini.Sasa yeye alijuaje mahali yalipo hili hali mimi nilishasumbuka juu ya urithi huo kwa miaka mimgi bila mafanikio.Sikuelewa kwa kweli nini kilitokea na nini James anataka kusema kwa sababu kipindi baba yetu anafariki yeye hakuwepo nyumbani na alikuwa tayari aeshachanganyikiwa.
James alichukua maiki na kuanza kueleza nini kimempandisha hapo jukwaani.Leo ni siku kubwa na siku ya furaha kwa Leah , kwangu na kwa wote waliofika hapa. Najua kwa wasiojua historia yetu mimi na Leah lazima watakuwa bado wako njia panda.Lakini nitaeleza kwa kifupi sana ili na nyinyi mjue nini kinaendelea. Mimi na Leah ni ndugu kabisa tuliyezaliwa na baba mmoja ingawa amama zetu walikuwa tofauti. Tulibahtika kuzaliwa kwenye familia ya kitajiri na baba yetu alitupenda sana.
Baba yetu alihakikisha tunapata elimu bora ambyo inetuwezesha kupambana na changamoto za maisha.Katika harakati hizo za baba mimi alinileta nchini humu (south Africa) kwa ajili ya masomo ya mambo ya utalii.Kwa bahati mbaya nilibahatika kukutana na msichana kutoka nchini Uganda ambaye tulipendana sana. Mpaka ikafikia kuwa siwezi kuishi bila yeye yaani upendo uliovuka mipaka.Baadaye binti huyu alirudi kwao mara baada ya kumaliza chuo na alikuwa amenizidi mwaka mmoja hivyo mimi niliendelea na masomo.Baadaye nilipata taarifa kutoka kwa rafiki yake wa karibu ambaye ndio binti huyu niliyenaye hapa kuwa binti yule niliyempenda alikuwa anaolewa.
Hapo James akampa kipaza sauti binti huyo na kabla hajaongea zilisikika kelele za shangwe zikimshangilia binti huyo. Kumbe binti huyo naye alikuwa ni msouth Africa na alikuwa ni maarufu sana nchini humo. ‘Binti huyo akasema kwa kifupi jamani leo tumeamua kuwapa suprrise na kuwazihirishia kuwa wafrika wote ni wa moja.Kweli mimi ndo nilikua rafiki wa karibu sana wa binti ambaye walikuwa wanapendana sana na kijana huyu.Niliamua kumpa taarifa kijana huyu mara baada ya kujisikia uchungu sana kuona binti yule alifanya kitu ambacho hata mimi kiliniuma sana.Kumbe jamani binti yule alikuwa na mchumbaa wake nchini kwao na ndiye aliyemleta pale chuoni kusoma na alikuwa akimlipia kila kitu.
Sasa sikuona haja ya kumficha James kwa maana alikuwa akidanganywa.Mimi nilimwambia ukweli James kwa sababu hata mimi nilikuwa nikimpenda sana. Kauli hiyo ilifanya ukumbi ufurike kwa shangwe maana ni wanawake wachache sana wanaoweza kukiri jambo hilo mbele ya kadamnasi ya watu.
Kwa hiyo kumbe wema wangu huo ndo ulikuwa unamwaribia James maisha yake kwani baada ya hapo alichanganyikiwa kabisa akajikuta anaingia kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya na baadaye akawa chizi kabisa.Tulimrudisha kwao nchini Tanzani tukamkabidhi kwa wazazi wake.Aliishia hapo binti huyo na akarudishia kipaza sauti James ili aendelee kuongea. Kwa hiyo ndugu zangu nilichangyikiwa na kupoteza fahamu na nilikuwa nazunguka mitaani na kuokota makopo na kula majalalani alisema James mara baada ya kupewa kipaza sauti.
Niliishi hivyo na kila siku nilikuwa nikitembea kwa miguuu na kutokomea pasipo julikana.Hali hii sitaki kuielezea sana kwa sababu naweza kutumia mda mwingi sana ila naomba nipeleke shukurani zangu kwa Dokta Patrick na namuomba aje mbele aelezee nini kimenifanya nirudi katika hali yangu hii ya kawaida na kuwa binadamu nianyejielewa.
Hapo surprise ziliendelea kwa sababu alipanda huyo daktari ambaye alikuwa ni mzungu.Asante sana James kwa kifupi mimi ni daktari wa magonjwa ya akili na saikolojia. Nikiwa Tanzania miaka mitatu iliyopita nilipoenda kwenye mambo yangu ya utaliii.Nilimkuta kijana huyu kwenye bonde la Ngorongoro na niliogopa sana maana niliambiwa huko pia kuna wanyama wakali.
Nilishindwa kuelewa alifikaje huko porini na alikuwa akitafuta nini.Niliingiwa na imani sana na kwa kutumia elimu yangu niliamua kuweka gari pembeni na kuamua kumsaidia. Nilijua kabisa atakimbia hivyo nilishuka na picha kubwa sana iliyovutia ambayo huwa natembea nayo na nikikutana na mtu yeyeote aliyechanaganyikiwa basi huwa namuonesha.
Picha hiyo ilikuwa imechorwa kwa kutumia rangi zote zilizopo duniani na mtu ambaye alirukwa na akili akiona lazima atakumbuka kitu chochote kizuri kilichowahi kutokea na kuanza kuiishangaa. Ndivyo ilivyokuwa kwa James alitulia tuliii na kushangaa picha hiyo hapo tuliweza kumkamata na kumfunga kamba na nilpofika getini tuliwaeleza kuwa tumemkuata barabarani na tumeamua kumsaiidia kwa sababu mimi ni daktari wa mambo hayo.Cha ajabu wale walinzi getini walicheka na kusema kuwa huyo ameshindikana kwa sababu ana uwezo wa kuishi na wanyama bila ya wao kumdhuru.Wakatuleza huyo ni kiboko kwa sababu alishawahi kukutwa amekaa na simba na taarifa hiyo ilirushwa mpaka BBC.Maelezo hayo ndo yalinifanya niamue kumsaidia kijana huyu.
Niliomba kibali kwa sereikali ya Tanzania ili niweze kumsaidia kijana huyu na nilikuja naye hapa South Africa ambapo ndo yalikuwa makaoo makuu ya ofisi yetu na hospitali ya kuwasaidia watu wenye matatizo ya namna hii. Basi serikali ya Tanzania ilikuwa tayari kunisapoti na iiahidi kugharamia matiababu ya kijana huyu. Basi kwa uwezo wa mungu na utaalamu wetu kijana huyu alianza kupona na siku hadi siku alianza kurudisha kumbukumbu zake na baadaye alikumbuka historia yote ya maisha yake.
Historia yake ndo ilituwezesha kumtafuta huyu binti ambaye walisoma nae.Kweli mungu ni mwema binti huyu tulimpata na kuwakutanisha na baadaye walienda Uganda na kukuta binti yule bado anaendelea na maisha yake ya ndoa.Pia tulimfundisha James vitu vya kufanya ili aweze kumsahau kabisa binti huyo na kukubaliana na matokeo.Hiyo ndo historia fupi naweza kuieleza juuu ya kijana huyu alimaliza daktari huyo mzungu na kurudisha kipaza sauti kwa James
Asante sana Dr Patrick na mungu akuzidishie uendelee kuwa na moyo wako huo wa ukarimu alisema James.Hapo ukumbi mzima ulikuwa umepoa sana na yule binti ambaye alikua naye alichukua mike na kuimba wimbo mmoja maarufu nchini humo.Kumbe yule binti alikuwa ni mshindi wa shindano na Cocacola Popo idlez shindano ambalo ni maarufu kwa kuinua vipaji vya wasanii.Nazani kwa Kenya ni sawa na lile la Tusker project na kwa Tanzania ni sawa na Bongostar search. Mmmmmh hata mimi nilimshangaa binti huyo kutokana na kipaji chake cha kuimba na alikuwa akiimba wimbo wa Beyonce wa Listen, yaani alivyouimba utafikiri ulikuwa ni wake. Watu wakafurahi kidogo na kutuliza machungu ya historia waliyopewa na dr Patrick.
Mimi nilikuwa namfuatilia yule binti jinsi akiimba vizuri na kusema kama ni kweli anampenda James basi kaka yangu huyo atakuwa ameokota embe dodo chini ya mbuyu. Baadaye James alirudishiwa kipaza sauti na kuendelea. Nilitamani sana kama angezungumzia kuhusu ile picha aliyokuwa nayo kwa sababu ndo ilikuwa bado inaniweka njia panda. James akaendelea kwa kusema najua hii picha itakua inawachanganya sana ila sio mbaya nitaielezea. Hii picha jamani ilikuwa imefukiwa ndani ya kaburi ambalo kaburi hilo ndo lilikuwa urithi wetu.Hapo kila mtu alishangaa kabisa kusikia eti ilifukiwa karibuni.Msishangae sana jamani nitatoa ufafanuzi wa kauli hiyo ilibidi James awaondoe watu hofu baada ya kusema kauli ambayo ilikuwa haijakamilika.
Marehemu baba yetu alikuwa ni mfanya biashara wa madini na alivyofariki tulizulumiwa kila kitu ambacho tulikuwa nacho kuanzia jumba,ardhi na kila kitu.
Lakini naweza kusema baba yetu alikuwa na maono ya mbele sana maana pamoja na kuzulumiwa mali zote hizo basi yeye aweza kuyaficha madini mengi sana sehemu ya kijijini kwenye shamba lake.Ili kuhakikisha madini hayo yanakuwa salama sana aliamua kutengeneza kaburi la bandia baada ya kuyahifadhi madini hayo chini ya ardhi.Siri hii hakuna aliyeijua zaidi ya Leah.
Hapo sasa James akawa ameniongezea hamu ya kujua kama yeye alikuwa haijui siri hiyo sasa ameipata wapi. Mimi tangia nikiwa nimechanganyikiwa baba yangu alikuwa akinitokea ndotoni na kuniambia siri hii na alikuwa akinisihi sana nimsaidie dada yangu kufanikisha dili hilo.Sasa nilivyopona na kuwa mzima kabisa ndoto hiyo ilikuja tena.Nilijaribu kumuelezea Dr Pactrick kuhusu ndoto hiyo ambayo ilikuwa inanitokea mara kwa mara lakini aliipinga na kusema hizo ni hisia tu hakuna ukweli wowote.
Lakini ilifikia mahali ndoto hiyo inanijia hata mchana nikiwa nimekaa mahali tulivu.Ilikuwa inanipa taswira nzuri ya sehemu ambayo madini yalikuwepo.Basi nilianza mikakati ya kulitafuta eneo hilo na hiyo ni mara baada ya ushauri wa mpenzi wangu Candy hapo akimaaanisha yule dada aliyekuwa naye pale jukwaaani.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO