Mtunzi: __
SEHEMU YA AROBAINI NA SABA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Lakini ilifikia mahali ndoto hiyo inanijia hata mchana nikiwa nimekaa mahali tulivu.Ilikuwa inanipa taswira nzuri ya sehemu ambayo madini yalikuwepo.Basi nilianza mikakati ya kulitafuta eneo hilo na hiyo ni mara baada ya ushauri wa mpenzi wangu Candy hapo akimaaanisha yule dada aliyekuwa naye pale jukwaaani.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Candy alinisihii sana tuende huko Tanzania Moshi Kilimanjaro tukajaribu kuyatafuta madini hayo.Ila kabla sijaanza kuyatafuta madini hayo niliamua kumtafuta kwanza ndugu yangu Leah.Niliangaika sana lakini kwa kuwa kumbukumbu zangu zilikuwa zimejirudi vizuri niliweza kupata baadhi ya taarifa zake japo ziinichanganya kidogo mara baada ya kuambiwa kuwa ni Mzambia.Nilimtafuta Mark mtu ambyae walicheza naye filamu na yeye alinithibitishi kuwa binti huyo ambaye kwa sasa yupo kwenye mashindano ya bigbrother ndiye yeye. Maelezo yangu yalifanaana kabisa na maelezo ambayo Leah alimwambia kuhusu kaka yake. Basi tangia siku hiyo nikawa naisubiri sana siku hii ili nije kuonana na dada yangu na kumueleza kuwa urithi ambao baba yetu alituachia tayari nilishaupata hivyo tutaishi maisha ya raha sisi na vizazi vyetu.
Hapo kuna mshabiki mmoja aliyeguswa sana na maelezo ya James alinyoosha kidole juu na alivyoona asikilizwi alisimama kabisa na kuja mbele na alipopewa kipaza sauti alisema yaani hii stori yenu nimeipenda sana ila naomba utuelezee uliyapataje hayo madini.Naweza kusema swali hilo hata mimi Leah nilitamani sana kama kaka yangu huyo angetuelezea maana haya mambo ya ndoto hata mimi huwa siyaamini sana.
Ila nakumbuka pia mara ya mwisho kuota juu ya madIni hayo ilikuwa ni miaka miwili na niliota kuwa madini hayo yameibiwa mpaka nikaingiwa na hofu kuwa uenda hayapo mahali salama tena. James alichukua kipaza sauti ili ajibu swali hilo na hapo kila mwandishi alikuwa makini sana kusikiliza majibu yake. Naweza kusema na yeye alipata umaarufu wa ghafla maana alikuwa akipigwa picha nyingi sana.
Na historia yake ilikuwa inafanana na historia ya mvuvi mmoja wa South Africa ambaye yeye alipotea baharini na baada ya kupigwa na dhuruba alibahatika kupata mwamba na akakaa hapo akisubiri watu wa kumuokoa.Kinyume na matarajio yake badala ya kuja waokoaji alikuja ndege ambaye alikuwa ni mkubwa sana zaidi ya papa au nyangumi.Ndege huyo ambaye inasemekana huwa anabeba madini kwenye magamba ya mguu yake aliweza kumuokoa mvuvi huyo.
Mvuvi huyo alishika miguuu akaondoka na ndege huyo na kwenda naye mpaka Australia.Na alipotua tu tayari mvuvi huyo alikuwa ameshachomoa madini hivyo akawa tajiri maarufu na Satalite za South Africa zilizokuwa zikifuatilia tukio hilo zilishawishi tukio hilo liingie kwenye kitabu cha kumbukumbu za dunia maarufu kama genesis.Kwa hiyo hata zile kamera na utamu wa simulizi wa maisha yetu aliyoku akisimulia na kufanya kila mtu amsikilize nilihisi huenda zikatupa umaarufu sana duniani.
James akasema waliondoka na kwenda kwenye hicho kijiji ambacho madini yalihifadhiwa. Na baaada ya kutafuta sana bila mafanikio waliamua kutafuata hela nyingi sana kwa kukopa kutoka bank na kwa watu maarufu kama mchumba wangu Mark, Lilian na wengine wote ambapo iliwawezesha kununua ardhi kubwa sana ambayo walihisi kuwa ndo kuna madini hayo.James aliendelea kusimulia kuwa walipata ugumu sana maana walishafukua makaburi mawili na kukutana na mifupa ya binadamu. Baadaye waliliipata eneo moja maarufu sana ambalo lilitengwa kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji. James anasema walifika sehemu hiyo na walifanikiwa kuliona kaburi hilo lakini ugumu ukaja kuwa eneo hilo lilishachukuliwa na serikali na hakuna mtu yeyote aliyeruhusiwa hata kusogea eneo hilo. James anasema walifikiria sana lakini walishindwa cha kufanya maaana serikali ilisema kuwa wataliamisha kaburi hilo wao siku chache zijazo ili waweze kuwapatia wananchi huduma ya maji waliyowahidi.
James ambaye alikuwa ameteka masikio ya watu wengi sana aliendelea kusimulia kuwa baada ya kuona kuwa watayakosa madini hayo waliamua kuomba kibali kutoka kwa serikali ili waweze kuliamisha kaburi hilo.Hapo anaeleza kuwa hawakusita kutumia rushwa ili mradi tu kufanikisha zoezi hilo.James anasema alikuwa na hofu sana juu ya hela nyingi alizozitumia tena zingine alichukua bank kunukua ardhi na kushawishi mradi huo uchelewe kuanza juu ya kitu ambacho hakuna hata mtu aliyejua ualisia wake
Baadaye walikuja kuanza kuchimba eneo hilo hapo James aliongea vitu ambavyo viliwachekesha sana watu alikuwa akilitamka neno chimba, chimba, chimba. hata zaidi ya mara kumi eti hayo ni maelezo ambayo alikuwa akimpa Mark aliyekuwa ameshika sururu kuchimba kaburi hilo la bandia lilojengewa kwa sumenti na mawe… Chimba chimba, chimba, chimba, chimba nasema chimba mpaka eti wakakipata kisanduku cha madini.
Kwa hiyo madini yalikuwa yamepatikana kwa mtindo huo alimaliza kusimulia James na kumkabidi kipaza sauti muendesha show hiyo.
Na kwa mbwembe alimwambia James asiondoke kwanza aseme tu mgawanyo wa madini hayo.Lilikuwa ni swali la utani lakini James alichukua kipaza sauti na kusema baba yangu alinambia kazi yangu ni kutafuta madini tu lakini anayehusika kuyagawa ni Leah nazani yanamsubiri akitoka hapa.
Hapo nilifarijika kidogo na kuona kuwa tayari mungu amejibu ndoto zangu za kuwa mtu maarufu na pia kuwa tajiri mkubwa duniani. Yule host akachuku kipaza sauti na kufanya mbwembwe zake za ki MC. Akawauliza watu kuwa wamechoka wakamwamba kuwa bado hawajachoka wanataka hiyo surprise ya pili. Kelele zililindima wageni wote wakitaka kujua hiyo surprise ya pili ni ipi hata mimi nilikuwa njia panda nisijue ni nini kinafuata.
Surprise namba mbili ilikuwa nikupanda wageni kutoka nchini Dubai.Niliwaangalia kwa umakini wa hali ya juu sana ili nijue kama nawajua au laaa. Nilishangaa kuona aliyekuwa akipanda ni yule mkuu wa kampuni ile niliyowapa kazi ya kumtafuata mama yangu.Hapo nilianza kuwa na shauku ya kuataka kujua nini kilikuwa kikiendelea.Kila mtu alikaa kimya kusubiri atasema nini mwarabu huyo pindi tu atakapofika jukwaani.Alivyofika kwa mbwembewe na yeye aliwasalimia watu kwa kiaarabu.
Nilipomuangalia vizuri nikagundua hapana hakuwa anatoka kwenye ile kampuni ya utafuataji wa watu waliopotezana.Nilijaribu kuendelea kuvuta taswira kuwa nilimuona wapi mtu huyo na nikakumbuka ni kwenye shirika la ndege la fly emirates.Alipanda na kueleza kwa kifupia nini kampuni yao inafanya na alisema amepanda hapo jukwaani kwa ajili ya kazi mbili moja ni kwamba kampuni yake imemtuma aje atangaze dau nono la mkataba juu yangu na nimeshaandaliwa nyumba ya kifahari na maisha yenye hadhi ya juu sana huko Dubai. Mkataba unahusu niwe manager wa masoko wa shirika hilo kwa upande wa Dubai.
Hilo dau lilotajwa hapo kwa kweli hakuna mtu aliyeaamini hata mimi nilifunga mdomo maana ilikuwa ni hela nyingi sana pengine sikuwahi kufikiria kuziiingiza wa mda huo mfupi wa miezi sita iliyotaja hapo.Baada ya kumaliza hilo jambo la kwanza alianza kushuka zake na kufanya watu wapige kelele na kusema bado moja bado moja ulisema una mambo mawili ya kusema.Ilibidi arudi na kuchukua kipaza sauti na kusema nilisahau jamani ila ngoja nimpandishe mtu ambaye atanisaidia kulisema hilo jambo la pili.
Kila mtu akawa ameduwaaa maana sasa surprise zilikuwa zimezidi kwa kweli.Alipanda mwarabu mwingine ambaye walikuwa kama wamefanana kidogo. Hapo sasa moyo wangu ulianza kuzizima kwa furaha kwa sababu mwarabu huyo mimi nilikuwa namjua ni yule wa kampuni ile ambayo niliwapa kazi ya kumtafuta mama yangu.Alionekana mwenye furaha sana na sijui alitaka kusema nini ambacho kingekuwa kweli ni surprise.
Surprise namba tatu ilianza kwa mbwembwe za kujitambulisha yeye ni nani na kampuni yao inajihusisha na shughuli gani.Ilikuwa ni zaidi ya shauku kwangu kutaka kujua kama siku hiyo mama yangu alipatikana au la.Alibwabwaja bwabwaja maneno kabla ya kusema kuwa ili kuthibitisha kuwa wanastahili kuitwa kampuni bora kwenye anga hizo za kukutanisha watu alisemaa ana muomba mama Leah apite mbele aje amlaki mwanaye aliyepotezana naye kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita. Hapo sasa moyo wangu ulizizima kwa furahaa nisiamini nianachoambiwa. Nilimuona mama huyo anayesemekana kuwa ni mama yangu akipanda jukwaa huku akiwa amesindikizwa na binti mwingine ambaye alionekana kuwa mdogo na kwa haraka haraka nilihisi labda ni mwanaye.
Sikuamini kama kweli alikuwa ni mama yangu maana alikuwa amejifunga ushungi huku akiwa amejisitiri kama isemavyo na iatakavyo dini ya kiislam.Kimoyomoyo nikajisemea usikute wananichezea pata potea ule mchezo wa karata tatu.Mama hakutaka kupoteza mda alikuja moja kwa moja sehemu ambayo nilikuwa nimesismama akanikumbatia.Alimwaga chozi na mimi nilimwaga chozi maana ilikuwa ni miaka mingi sana tangia aniache mimi nikiwa mdogo.
Sikujua aliiishi maisha gani kwa kipindi chote hicho na nini kilimkuta mpaka akaamua kukaa kimya miaka yote hiyo bila kunitafuta. Mama kama alijua kuwa nilkuwa sijamuona sura vizuri aliaamua kutoa ule mtandio na kufanya sura yake kuonekana vizuri.Sikuhitaji kuuliza tena maana alifanana kabisa na ile picha ambayo nilikuwa nimeishika mkononi.Nilimkumbatia kwa nguvu na kwa mara ya kwanza nikapata kumbatio la mama ambalo nililitafuta kwa zidi ya mika 20.
Mama akapewa kipaza sauti na kuanza kueleza nini kilimkuta mpaka akapotezana na mwanaye mpendwa.Alianza kusema “ kwanza ninaomba radhi kwa ndugu zangu maana walipinga nisifikie kwenye shindano hil kwa sababu wao ni watu wa imani kali ya dini hivyo wanalichukulia shindano hili kana utovu wa maadili.Nasema nilikuwa sina jinsi na pia sina jinsi kwa maana kupitia ndugu zangu niliweza kumpoteza mwanangu na kupitia hao hao nimeweza kumpata mwanangu.
Nina machungu sana ndani ya nafsi yangu nikikumbuka nini kilifanya kupotezana na mwanagu ila pia nina furaha sana kwa kumpata mwanangu. Nimeugua kwa miaka mingi sana lakini niliposikia kuwa mwanangu amekuja Dubai na kunitafuta nilijikuta napona ghafla. Najua si vizuri kuyaeleza matatizo yaliyonikuta ila kwa ajili ya kuiponya nafsi yangu ambayo imekuwa na machungu sana nitaeleza.
Kwa kifupi mimi nilkutana na marehemu baba Leah alipokuwa akija nchini Dubai kwa ajili ya biashara zake za madini na magari. Kama mnavyojua mapenzi hayachagui umri, rangi au kabila basi nilijikuta kwenye mapenzi mazito sana na mwanaume huyo. Familia yangu haikukubali kabisa mimi kuolewa na rangi nyeusi hivyo walinitenga na kusema hawanitambui kuwa mimi ni ndugu yao.Lakini kutokana na mapenzi mazito niliyokuwa nayo kwa baba yake na Leah nilijikuta nipo tayari kwa lolote hivyo nikahama na kwenda kuishi Tanzania.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO