MY DIARY (48)

0
Jina: MY DIARY
Mtunzi: __

SEHEMU YA AROBAINI NA NANE
TULIPOISHIA...
Familia yangu haikukubali kabisa mimi kuolewa na rangi nyeusi hivyo walinitenga na kusema hawanitambui kuwa mimi ni ndugu yao.Lakini kutokana na mapenzi mazito niliyokuwa nayo kwa baba yake na Leah nilijikuta nipo tayari kwa lolote hivyo nikahama na kwenda kuishi Tanzania.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
Katika miaka hiyo tuliyokaa nilibahatika kupata mtoto huyu ambaye sasa ndo anaweka historia nyingine katika bara la Afrika.

Naomba leo nimuombe msamaha kwa sababu ndugu zangu walinishinikiza sana na nikajikuta namuacha mwanangu na kurudi Dubai.Nilimshawishi sana baba yake tuhamie Dubai lakini alikataa wazo hilo akidai kuwa Arusha Tanzania ndo ilikuwa makao yake makuu ya kibiashara.Wakati naondoka nchini Tanzania nilijua kabisa nitawza kurudi tena.Lakini kilichonikuta nashindwa hata kuelewa ni nini.Nahisi nilifungwa nikashindwa kabisa kurudi Tanzania.

Nikalazimishwa kuolewa na mwanaume ambao wao walinichagulia. Nilianza maisha mapya lakini sikuwa na amani na nafsi.Maisha yaliendelea lakini kwenye ndoa hiyo ya shinikizo kuna tatizo lingine lilitokea katika ndoa mpya hiyo ambapo hatukuweza kuapata mtoto.Ndo ikawa ngumu sana na baadaye nilianza kuugua maradhi ya moyo pressure nna kisukari. Maisha yangu yalikuwa magumu sana na mme wangu aliamua kuoa mwanamke mwingine. Nilijaribu kuwaelewesha kuwa mimi sio mgumba lakini hawakunielewa manyanya so yalizidi siku hadi siku mpka ikafikia mahali nikaomba talaka yangu.

Nayaongea haya kwa machungu makubwa sana kwani hata hivyo sikuwepo nchini mwangu.Nilikuwa nchini India kwa ajili ya matibabu ya moyo.Kuna ndugu yangu mmoja ambaye ni mdogo wangu ndo alikuja kuniambia kuwa kuna kampuni inaonesha picha zangu na kunitafuta ili niweze kukutana na mwanangu. Bado ndugu zangu walilipinga hilo swala la mimi kujitokeza hazarani kwa ajili ya mwanangu.Walinileza kuwa hawamtambui mtoto huyo.

Pia walisema sikuwahi kupata mtoto na hiyo ilikuwa ni mbinu tu ya kujisafisha kutokana na tatizo langu la kutokuzaa.Niliandamwa kwa maneno sana na waliniita Malaya na kusema matatizo yote hayo ni kutokana na mimi kukubali kwenda kufanya umalaya Africa. Sikuvunjika moyo mdogo wangu aliendelea kunifariji na siku zote mtoto wake huyu ndo amekuwa kama ni mwanangu na huwa ananipa kamapnai na kuenda nae sehemu yeyote ile ambayo nilihitaji.

Nilimuomba mungu aendelee kunitia nguvu ili niweze kufanikiwa katika kila jambo langu ninalolifanya kwa haki.

Niliapa kama nikipona maradhi ya mwili basi ni lazima nitamtafuta mwanangu Leah popote alipo na kwa gharama yeyeote ile.Nilisema kama nilivyompenda baba yake na kukubali kutengwa katika familia ndivyo hivyo nitakavyofanya kwa Leah na kuwa tayari kutengwa na familia kwa ajili ya mwanangu wa pekeee. Kitu kilichokuwa kina nizuia ni ugonjwa ulionisumbua kwa mda mrefu naweza sema tangia niachane na baba yake.Leo hii nakiri mbele za watu wote mliofika hapa kushuuhudia mshindi wa Big brorher kuwa nilipona mara baada ya kampuni ya kutafuta watu kunifuata nchini India na kuniambia kuwa mwanangu yupo na ameingia tatu bora ya shindano hili.

Baada ya hapo mama yangu alinyamaza kimya kama mtu ambaye alikuwa akiwaza jambo kisha akasema mwanangu Leah naomba unisamehe kwa yote yaliyotokea nakuhaidi kuishi na wewe sehemu yoyote utakayopenda niwe. Hapo hata mimi maneno hayo yaliniumiza sana nikajikuta namsogelee mama yangu na kumkumbatia.Machozi yalikuwa yakinitoka kwa sababu maneno aliyoyasema kwa kweli yalikuwa yakiniumiza mno.

Sio mimi tu niliye mwaga chozi bali kila mwanadamu ambaye alikuwa na hisia za karibu.Nilimuona yule binti aliyepanda nae pale stagini naye akimwaga chozi.

Tulikumbatiana kwa mda mrefu kabla ya baadae host wa show kusema maneno yaliomaanisha kuwa tulikuwa nyuma ya mda hivyo tuache mambo mengine yaendeleeee.

Mama alishuka jukwaaani huku na mimi nikisema asante mama na asante Mungu kwa upendo huu mkubwa wa kumpata mama yangu ambaye siku zote nilikuwa nikimtafuta na kuumiza kichwa kuwa alikuwa ni mwanamke wa namna gani aliyezaa na kumuacha mwanaye bila kumtafuta kwa miaka yote hiyo.Nikapata funzo kuwa tusipende kutoa lawama kwa jambo ambalo hatujui chanzo chake.

Ilniibidi niishukuru ile kampuni kwa msaaada mkubwa walionifanyia na nikawahidi kuwalipa asilimia mia ya pesa zilizobaki kuacha zile hamsini walizokuwa wakinidai. Tofauti na mawazo yangu kuwa kuwalipa mara mbili itakuwa ndo shukurani yao yule mwakilishi alikataa na kusema kuwa kamapuni imemtuma kuwa wanaomba kufanya kazi na mimi ili wanitumie katika kuatangaza kampuni yao katika nchi za Kiafrika hivyo sio mimi nitawalipa hiyo hela wanayonidai bali ni wao watanilipa. Nilishangaa kwa sababu kila kampuni ilikuwa ikitaka kufanya kazi na mimi hivyo naweza kusema ilikuwa ni zaidi ya Baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu.

Basi kwa kuwa mda ulikuwa umeenda sana host alimpandisha mtu wanne ilia je atoe surprise yake na hapo nilimuona kaka yangu James akijiandaa. Sasa nilishindwa kuelewa kuwa atatoa surprise gani tofauti na ile ya kwanza ya mimi na yeye kukutaka baada ya kupotezana.

Surprise namba nne ni kwamba James alishika kipaza sauti na kusema leo najua mtakuwa mnashangaa sana ila nimeamua kuweka historia ingine leo katika maisha yangu.Nimemeamua mimi na mpenzi wangu Candy kufanya jambo kubwa ambalo litawashangaza watu wote mliofika hapa.Nimekuwa nikipitia mambo mengi sana katika maisha yangu na kwa kweli kwa imani yangu itakuwa ni vibaya sana nisipo mshukuru mungu kwa yote aliyenitendea.Kwa imani yangu bwana yesu alishawahi kusema kuwa ukimkiri mbele za watu na yeye atakukiri mbele za Mungu.

Hivyo leo nataka kumkiri Mungu mbele ya watu wengi wenye imani tofauti tofauti.Sitaki kuwapotezea mda wenu maana nimeambiwa kuwa pia bado kuna surprise moja ambayo ndo itakuwa ya mwisho usiku huu wa leo.Namuomba kiongozi wa dini aliyendaliwa kwa shughuli hii apite mbele. Na wakati huo huo mke wangu mtarajiwa afike mbele ya jukwaa.Hapo nikamuona mbaba alieyevalia suti kali akipita mbele huku akiwa ameshikilia biblia na yule binti mrembo kipenzi cha wananchi wengi wa South Africa alipita mbele huku akishangiliwa kwa nguvu na mashabiki wake waliokuwepo hapo.

Yule mchungaji akapewa kipaza sauti na kusema “Najua hapa tumekusanyika watu wa imani mbali mbali wanaonamini dini na wasioamini dini.Hivyo sitotumia zaidi ya dakika mbili ili nisiwakere watu wengine.Mgeukie mwenzio mwambie Mungu yupo. Watu wote ukumbini wakafanya walivyoagizwa na kusema Mungu yupo. Yule mchungaji akasema mgeukie tena wa kulia kwako mwambie Mungu ni mmoja watu wote wakageuiana na kusema Mungu ni mmoja. Hapa nikakumbuka ule utani kuwa eti kuna mchungaji alikuwa anahubiri na kuwaambia waumini kuwa shida zao zote zimeisha hivyo akaanza kusema mgeukie mwenzio na umwambie umwambie umasikini bye bye, shida zote kwisha, maradhi yote kwisha.

Kwa wale mabinti wasiopata mimba mgeukie mwenzio leo utapata mimba.Hapo ndo kasheshe sasa eti mtoto kamgeukia baba yake na kumwambia leo utapata mimba. Ni utani tu jamnani niekumbushia kidogo, ila tusipende kuweka utani kwenye mambo ya dini. Mungu atatulaani bure.

Basi yule mchungaji akaendelea kusema “Sikuzote nimekuwa nikisisitiza upendo na amani duniani kote.Hakuna haja ya kubaguana kwa sababu ya dini, rangi, sura wala kabila.Nachukua nafasi hii kuwataka wa South Africa wanowabagua wafrika wenzao na kuwafukuza waache mara moja kwa maana Waafrika hao hao walishiriki kuupigania uhuru wa nchi hii.Jamani si mnakumbuka nchi kama Tanzania ilivyokuwa mstari wa mbele kuakikisha kuwa tunapata uhuru. Na sio Tanzania bali ni nchi nyingi sana zilitusaidia kupinga ubaguzi uliokuwa unaendelea nchini.

Ni ombi langu tuwe na moyo wa kizalendo kama wa baba wa taifa hayati Nelson Mandela.Ukimbi wote ulikuwa kimya sana maana ilionekana kiongozi huyo alikuwa anaongea maneno ya busara sana.Kwa hiyo ndugu zangu kusibitisha hilo kuwa waafrika wote ni wa moja na mungu ni mmoja nitakwenda kuwapa neema ya ubatizo na kuwafanya ndugu hawa waliopendana kuokoka. Nawaalika wote wanaotaka kuokoka na kukiri mbele ya kadamnasi kuwa wanamuamini Mungu waje mbele.Hapo Leah mimi sikutaka kujiuliza mara mbili mbili na mimi nilisimama na kujiunga na watu hao.

Wakati mchungaji huyo akiendelea kutoa wito nilimuona pia Mark akipanda na kuja kuungana na sisi. Waliongezeka na watu wachache tukawa kama 60 hivi. Siunajua tena kumkiri Mungu mbele za mataifa ni jambo gumu sana kwa watu wengi. Naomba mtarudia maneno haya nitakayoyasema alisema mchungaji yule mara baada ya kurizishwa na idadi ya watu waliopandda jukwaani. “This is my decision to receice Christ as my savoour( Huu ni uamuzi wangu kumpokea Yesu awe mwokozi wangu)

Akendelea kusema “Confessing to God that I am a sinner and believing that the Lord Jesuse Christ died for my sin on the cross and was raised for my justification. (Naungama kwa mungu kwamba mimi ni mwenye dhambi, na kuamini kwamba Bwana yesu kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zangu juu ya msalaba na alifufulwa kwa ajili ya kuhesabiwa haki.)

Akaendelea kusema kwa kimombo “I do now receive him and confess him as my personal savoiur(Tangu sasa ninampokea na kumkubali Bwana kuwa mwokozi wangu).

Baada ya maneno hayo ambayo yalinitoa jasho mchungaji na wale wengine waliokiri kumpokea Yesu walishuka kwenye jukwaa na kumuachia host kipaza sauti. Naye akasema asante sana mtumishi wa mungu kwa kufanya kazi yako naamini sasa taifa la mungu litakuwa, alafu akachelka kidogo.Yaaani huyu MC alikuwa na utani sana mpaka kwenye mambo ya mungu.

Akasema pia nawaalika kama kuna kiongozi wa dini ya kiisalam na yeye aje aseme neno kwa ajili ya kusisitiza umoja kwa waaafrika na dunia nzima. Akapanda kijana mmoja ambaye kweli alionekana ni shekheee na yeye akasema amefurahishwa na maneno ya mchungjai kuwa Mungu ni mmoja.Akasema pia lazima tusisitize amani na upendo kwa sababu ndo kitu tulichoagizwa na mungu. Akatoa wito kuwa kama kuna mtu anataka kuslim basi apite mbele.Hapo napo walipanda watu wengi na kupewa huduma hiyo ya usilimisho.Kweli hii ilikuwa ni historia kubwa sana maana watu waliamasika utazani labda ndo ilikuwa mwisho wa dunia..

Baada ya maneno ya kusilimu ambayo waliambiwa wayatamke kiongozi huyo alisema neno ya mwisho kabla hajashuka.” Kila alie na akili timamu, mwenye busara naa anaetaka haki, na kusimama pamoja na haki, basi akiangalia dunia ilivyo na jinsi inavyokwenda basi lazima kutakuwa na nguvu kuuu nayo ni mwenyezi mungu.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)