Mtunzi: Hussein O Molito
SEHEMU YA KWANZA
Ni kipindi cha mvua za masika. Upepo mkali, na mvua kubwa iliendelea kunyesha kwa kasi kila kona ya nchi ya Tanzania.
Ipo mikoa iliyofurahia mvua hizo kwa kuwa walikua wanaisubiria kwa hamu kwa ajili ya kilimo. Lakini ipo mikoa iliyokua inapata shida kwa uharabifu wa mazingira na mengineyo mengi.
Moja ya miko hiyo ni Dar-es-salaam. Watu wanaoishi katika mkoa huo walichukia mvua mfululizo kutokana na sababu mbalimbali. Biashara nyingi zilikwama kutokana na maeneo kadhaa kuwa na maji.
Baadhi ya watu walisema “mvua si bora inyeshe kijijini huko kwenye mashamba?”
Wakimaanisha kuwa jiji hilo halitegemei kilimo bali ni biashara ambazo hazihitaji sana mvua.
Ilikua asubuhi moja mishale ya saa kumi na mbili asubuhi. Mvua iliendelea kunyesha kwa kasi ikiambatana na upepo mkali. Bardi ndio usiseme.
Hivyo vyote havikuwa kikwazo kwa kijana KHALIDI kuamka na kwenda kutafuta riziki.
Aliingia kavu kavu bila koti wala mwamvuli. Alianza kuukanyaga kama kwaida yake kuanzia Kigogo anapoisha mpaka kariakoo anapofanyia shughuli zake.
Njaini hakukua na mtu zaidi ya yeye mwenyewe tu. Aliendelea kukata mitaa hadi kufikia maeneo ya jangwani na kuamua kupumzika kwenye ofisi moja iliyokuwa imefungwa kutokana na baridi alilokuwa analisikia.
Alikaa kwa muda usiojulikana kutokana na mvua zilizokua zikiendelea kupiga wakati huo
Masaa yalizidi kusogea bila wingu kuonyesha dalili zozote za kukucha. Hadi ilipokuja gari moja aina ya Range rover na kupaki maeneo yale. Alishuka dada mmoja akiwa amevalia suti nzuri ya drafti akiwa na mwamvuli wake.
Yule dada alisogea maeneo aliyosimama Khalidi na kumsalimia.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
“habari kaka.” Alisalimia yule dada na kutoa tabasamu dogo lakini lililoonyesha vizuri uzuri wa sura yake.
“salama.” Alijibu Khalidi huku akitetemeka mwili mzima kutokana na baridi lililokuwa likimpiga bila kipingamizi kutokana na kulowana mwili mzima.
“mbona umeloa hivyo kaka, na unajua fika kuwa huu ni wakati wa baridi?” aliuliza yule dada huku akionyesha kujali.
“maisha tu dada, mimi ndio kila kitu katika maisha yangu. Mimi ndio mtaji, mimi ndio mfanya kazi wa kulihudumia tumbo langu. Ndio maana nimekubali kulowa ili nikapate chochote cha kutia tumboni.” Alijibu Khalidi na kuuangalia yule dada ambaye hakua na tabasamu kama lile la mwanzo. Zaidi alijawa na Huzuni kila amuangaliapo.
Bila kuongea chochote, yule dada aliliendea gari lake na kutoa Jacket na kurudi nalo pale aliposimama Khalidi.
“chukua hili jacket na huu mwamvuli basi ili uwahi kazini.” Aliongea yule dada na kuondoka kuelekea Ghorofa ya pili kutoka pale. Khalidi alizidi kumtazama yule dada anapoelekea mpaka alipopotea katika upeo wa macho yake.
Alienda kariakoo shimoni ambapo yeye alikua anafanya kazi ya kubeba mizigo. Ilipotimia mida ya saa tano mvua ilikua imeshakata na kijua cha matumaini kilitoka mida hiyo. Khalidi alinyanyuka na kuondoka kueleka kule ofisini kwa yule dada aliyemuazima vile vitu asubuhi.
Alifika katika jengo lile refu na kutaka kuingia ndani. Kabla hajafungua mlango, alifatwa na mlizi na kuzuiwa.
“ humu ndani hawaruhusuwi watu kama wewe “ aliongea yule mlinzi na kumtazama kwa kumkagua.
“watu kama wapi ndio wanaruhusiwa humu ndani?” aliuliza Khalidi kwa ukali kuonyesha kukwazika na kauli ya yule mlinzi.
“we hujioni ulivyomchafu?” aliendelea kuongea yule mlizi maneno yaliyozidi kumkera Khallidi.
“naweza kuwa mchafu duniani na kuwa msafi mbinguni. Usinijaji kwa muonekano wa nje wakati hujui kilichomo ndani yangu. Naomba chunga kauli zako.” Aliongea Khalidi maneno ya kishujaa na kumuacha yule mlinzi na kuzama ndani.
“unaelekea wapi we mkaka??” ilikua sauti nyembamba kali ilkifoka kutokea kwenye chumba cha mapokezi.
“naenda kumtafuta dada mmoja hivi nina amana yake.” Aliongea Khalidi kwa upole na kukisogelea kile chumba.
“we unapita kama chooni, mimi niliyekaa hapa unaniona kinyago au?” aliongea yule dada kwa nyodo.
“samahani dada, sikujua utaratibu wenu.” Alijibu Khalidi na kutambua kosa lake.
“anaitwa nani huyo dada?” aliongea yule dada wa mapokezi n a kupunguza ukali wa sauti yake baada ya kuombwa radhi.
“simjui ni mara yanu ya kwanza kumuona, ila amevaa suti ya draft na ni mweupe sana kama shombe shombe hivi.” Alizidi kuelekeza Khalidi na yule dada akamuelewa ni mtu gani anayemuulizia.
“ ulikua una shida naye gani?.. maana huwezi kuonana nae bila appointments.” Aliongea yyule dada kuonyesha ni jinsi gani huyo mtu aliyekua anamuulizia ni muhimu kuliko yeyote pale ofisini.
Waliongea kama dakika tatu na muafaka ulikua ni kupiga simu kwa huyo Dada.
Maelekezo ya yule dada wa mapokezi juu ya ujio wa mtu yule mchafu yalitosha kumjulisha yule dada kuwa ni yule mtu wa asubuhi.
Alikubali aingie na Khalidi akapata nafasi kwa mara ya kwanza kupanda lifti. Alifikishwa kwenye chumba kilichoandikwa Managing Director.
Alifika ndani na kupokelewa na yule dada kwa tabasamu.
Mbele ya meza kubwa kulikua na kibao kilichoandikwa SABRA BAHAJ.
“nimekuletea amana zako tu, mi si mkaaji.” Aliongea khalidi baada ya salamu.
“kumbe ulikua hujaelewa…mi nilikupa tu.” Alijibu yule dada na kutabasamu.
“samahani..”aliongea yule dada na kuipokea simu iliyokua inaita kwa muda mrefu mezani kwake.
Aliisikiliza ile simu na mara akaanza kuzunguka zunguka kile chumba na kuonyesha kuwa taarifa alizozipata zilimshtua sana.
“NINI?????”
Hiyo ndio ilikuwa kauli ya mwisho kwa yule dada. Baada ya hapo alianguka chini kama gunia la viazi.
Khalidi alishtuka na kumsogelea yule dada alipoanguka. Alipomuangalia alikuta anatoka damu mdomoni na kichani zikimiminika kama maji. Aliangalia huku na huko hakuona mtu mwingine aliyekuwamo zaidi ya yeye tu mule ndani.
Wakati anamnyanyua na kumtikisa yule dada, alisikia kelele kutoka kwa secretary aliyeingia mule ndani ghafla baada ya kusikia kile kishindo cha haja ikiomba msaada.
“ jamani kauaaaaaaaaaaaaaaaaaa”
Hizo kelele ndizo alizokimbia nazo yule Secretary na kutoka nazo nje.
Haikupita hata dakika moja, tayari watu walishajaa kushudia lile tukio. Khalidi akiwa anashangaa, alisikia kauli ya askari mmoja kati ya maaskari watatu wenye silaha ikimuamuru anyanyue mikono yake juu. Alikiri na kunyanyua mikono juu na askari aliyekuwa jirani yake kwa umakini mkubwa alimsogelea na kumvisha pingu.
Hakuna aliyejali kuondolewa yeye pale na maaskari kwa kua waliamini kuwa wale maaskari wamemuokoa maana wao wangemuua kwa hasira walizokuwa nazo.
Ambulance ilifika haraka eneo la tukio na kumyanyua Sabra na kumuwahisha hospitali. Huko alipokelewa haraka na kuwahishwa emergency. Huko aliingizwa chumba maalumu na matibabu yalianza mara moja.
Kwa Khalidi hali ilikua ngumu. Alikula kibano cha nguvu na kuteswa kwa kosa ambalo hakulifanya.
“nani aliyekutuma kumuua Miss Sabra?” aliuliza mpelelezi mkuu mwenye veo vyake begani.
“sijatumwa na mtu yeyote afande.” Aliongea huku akilia kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata kwa muda ule.
“kwa hiyo wewe mwenyewe tu ndio umeamua kumuua??...ili upate nini labda nielezee!” aliendelea yule mpelelezi kumbana Khalida kwa maswali mfululizo.
“kaanguka mwenye….”
Hakumalizia kauli yake. Alikutana na ngumi nzito iliyomtoa kwenye kiti na kudondoka chini.
“mrudisheni ndani, si anajifanya hataki kusema. Mi ndio dawa ya watu jeuri kama hawa.” Aliamuru yule mpelelezi na maaskari waliokuwa pembeni wakatii amri na kumnyanyua Khalidi msobe msobe na kumpeleka selo.
Akiwa ndani kwenye selo peke yake, alilia sana na kujilaumu kwa kuwa mwema na kumrudishia amana yake yule dada.
Alitamani airudishe yuma au angeiruka ile siku ngumu kuliko siku ngumu alizowahi kupitia. Alitamani asingekutana na yule bint hata kwa bahati mbaya maishani kwake.
Usiku alitulia na kumgeukia mola wake na kumuomba amjaalie yule binti awe mzima na amtetee kwenye kesi ile ngumu. Alijua kabisa kama yule dada akifa, basi na yeye maisha yake yataishia gerezani.
Aliomba usiku kucha na kulia akiomba afueni ipatikane kwa Sabra.
*****************************
Baada ya siku mbili, sabra alirejewa na fahamu na aliweza kukumbuka yote yaliyotokea nyuma. Baada ya kufumbua macho, alikutana na watu kama sita anaowafahamu. Walikuwa wafanyakazi wake waliokuja kumuangalia wakati ule.
“pole Miss Sabra”
Zilitoka sauti kwa pamoja kwa wafanyakazi wake wote waliofika pale.
“ahsanteni.” Alijibu na kutabasamu.
“mungu mkubwa sana , mungu anakupenda bosi. Maana walidhamiria kukuua kabisa !” aliongea dada mmoja kati ya madada waliofika pale.
“kwanini unasema hivyo Diana.” Aliongea Sabra na kuonyesha kutokumbuka tukio la yeye kutaka kuuliwa.
“umeshasahau bosi yule mtu mchafu alivyotaka kuua. Yaani bila secretary wako kuona angekumaliza kabisa.!” Aliongea yule dada kana kwamba alikua na asilimia zote juu ya Khalidi kuhusika kutaka kumuua bosi wao.
“hamna kitu kama hicho Diana, …. Kwanza sijamuona secretary wangu. Yupo wapi kwani?” aliuliza Sabra baada ya kuona sura moja ya mfanyakazi wake haikuwepo pale.
“ ameeenda mahakamani” alijibu haraka Diana.
“mahakamani?... kuna kesi ya nani?” aliuliza Sabra kwa mshangao.
“si kuhusu kesi yako. Yeye kachukuliwa kama shahidi pekee wa lile tukio.” Aliongeza Diana na Kumfanya Sabra kunyongea.
“masikini kijana wa watu, mbona yeye hahusiki na kitu chochote?” aliongea Sabra na kuwafanya wafanyakazi wake watazamane.
“ kwani bosi unakumbuka kabla hujakuja hapa hospitali kulitokea nini?” aliuliza jamaa mmoja aliyekuw pembeni.
“ nilipigiwa simu kutoka uingereza na kupewa taarifa mbaya kuhusu mume wangu. Ndio nikapata mshtuko na kudondoka chini. Hicho ndicho ninachokikumbuka.” Aliongea Sabra na kuwaacha wafanyakazi wake hoi.
“basi bosi maaskari wasingekuja tungeshaua mtu asiyekuwa na hatia.” Aliongea Diana kwa huzuni.
“kwa hiyo leo ndio siku ya hukumu au?” aliuliza Sabra huku akiwa hana raha kwa taarifa alizozipata juu yu Khalidi.
“hapana. Leo ndio kesi inasikilizwa kwa mara ya kwanza.” Aliongea Diana na kumtia matumaini Sabra.
***********************
Siku tatu baadae, Sabra aliruhusiwa na kurudi nyumbani. Alipumzika siku hiyo na kwenda mahabusu alipokuwa Khalidi akisubiri hukumu.
Khalidi alishangaa kuitwa na mtu asiyemfahamu. Alitoka na kwenda kumuangalia huyo mtu maana kiukweli hakua na ndugu aishie hapa Dar hata mmoja anayemfahamu..
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO