Mtunzi: Hussein O Molito
SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Khalidi alishangaa kuitwa na mtu asiyemfahamu. Alitoka na kwenda kumuangalia huyo mtu maana kiukweli hakua na ndugu aishie hapa Dar hata mmoja anayemfahamu..
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
Alipigwa na butwaa baada ya kumuona Sabra pale.
“ahsante mungu.” Aliongea Khalidi baada ya kumuona tu yule binti pale.
“pole sasa kaka yangu, nisamahe mie.” Aliongea Sabra kwa masikitiko baada ya salamu.
“ nimeshapoa baada ya kukuona. Naamini wewe ndio unaweza kunifanya nitoke au kubaki humu ndani.” Aliongea Khalidi huku machozi yanamlenga lenga.
“ usijali, hata hivyo nimekuja kufuta kesi. Kwa hiyo wanaweza kukuachia leo hii hii.” Aliongea Sabra na kuufanya uso wa Khalidi kuingiwa na chembechembe za furaha.
“nakushukuru sana dada yangu, sio kuzuri huku.” Aliongea Khalidi huku akionyesha wazi kutopenda maisha ya mule selo.
Sabra alikamilisha taratibu zote za kufuta kesi na Khalidi akaachiwa.
“ wamekuumuza sana..pole kaka yangu.” Aliongea Sabra baada ya kuona majeraha kadhaa kwenye mwili wa Khalidi.
“yote ni mapitio ya maisha dada, nakushukuru kwa kukubali kupoteza gharama zako kufuta kesi hii iliyokuwa ngumu kwangu.” Aliongea Khalidi na kumfanya yule dada kujiona ana hatia kwa yaliyomkuta Khalidi.
Baada ya maongezi machache , Sabra akampa lifti Khalidi kwenye gari yake na kumpeleka kigogo.
“ukinishusha hapa panantosha dada, maana ninapoishi napita uchochoro huu na kwenda katikati huko. Gari si rahisi kufika.” Aliongea Khalidi na kutoa maelekezo kwa mikono baada ya kufika kigogo mwisho.
“sawa, una simu?” aliuliza Sabra
“simu sina, ila nina line ninayotumia nikigongea simu kuwasilina na matajiri zangu wa oda.” Aliongea Khalidi kwa kujiamini.
“ chukua hii. Naamini itakusaidia upande wa mawasiliano.” Aliongea Sabra baada ya kuchomoa line yake kwenye Nokia ASHA 501 aliyokuwa nayo yeye na kupachika line yake kwenye simu nyingine aina ya sumsung.
Khalidi alitoa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango. Simu aina hiyo aliishia kuisoma kwenye magazeti na kuina kwenye matangazo ya kariakoo. Leo ilikua kama zali anamilikisha tena bure bila masharti yoyote.
“kesho njoo ofisini kwangu. Kuna watu wanataka kukuomba msamaha kwa uzushi waliokuzushia Khalidi” aliongea yule dada na kumuachia elfu thelathini.
“hiyo nadhani inakutosha kuchukua tax mpaka pale. Nakuomba usikose. Hata kama utapoteza muda wako wa kazi, nipo tayari kukulipa.” Aliongea Sabra na kuonyesha jinsi gani anavyomuhitaji.
“usijali, nije saa ngapi?” aliuliza Khalidi huku akiwa na tabasamu pana kabisa.
“saa tisa itakua poa sana”
Baada ya maagano, Khalidi alishuka na Sabra akaondoka na kumuacha Khalidi akiliangalia lile gari ambali ndio “bismillahi” kulipanda.
Kesho yake Khalidi alifika mapema ofisini kwa Sabra. Kabla hajaingia ndani, alikutana na Sabra mlangoni. Alijitahidi kuvaa nguo amabayo kwake ni mpalo. Lakini shati lilikua limejikunja na suruali ilikua haiendani na rangi ya shati alilovaa.
Sabra alikua wa kwanza kumsalimia na kumlaki Khalidi. Baada ya salaam alimuomba waende mahali kwa sababu mida waliyoahidiana ilikua haijafika.
Safari yao iligota kwenye duka la suti za kiume. Sabra alimwambia Khalidi achague. Hakuwahi kuvaa suti toka azaliwe. Ndio kwa mara ya kwanza anapata zali.
Suti aliyovaa sanamu kwenye duka lile alitokea kuipenda na kuichagua.
Alipoijaribu alikua kama katengenezewa yeye. Alipendeza kupita maelezo. Alimshukuru Sabra na kurudi ofisini.
Walifika saa tisa juu ya alama. Kila kitu kilikua tayari. Na wafanyakazi walikua katika siti zao. Kuliandaliwa part ndogo ya kumuomba msamaha Khalidi. Kulikua na kila sababu ya kushangaa kwa jinsi palivyopambwa kwa vitambaa vya rangi zivutiazo na maua mbalimbali. Kwenye jukwaa kubwa kulipambwa na maandishi makubwa yaliyoandikwa FORGIVE US KHALID. Alipotupa macho na kuyasoma yale maandishi, alibaki anatabasamu na kumshukuru mungu kumkutanisha na yule msichana ingawaje mwanzoni alikua analaani.
Kulikua na MC aliyeiedesha tafrija ile fupi na kumpa kipaza Khalidi aongee kama ameridhika kwa msamaha waliokusudia kuomba wale wafanyakazi.
“sina la kusema zaidi ya kuwashukuru kwa kutambua kosa na kuamua kuomba msamaha. Kwa moyo mkunjufu nimewasamahe kutoka moyoni, ahsanteni”
Alimaliza kuongea maneno hayo machache na kupigiwa makofi na kila mtu aliyekuwa pale.
Baada ya hapo keki ililetwa mbele yake na kumlisha kila mmoja kama ishara ya msamaha.
Vyakula vya aina mbalimbali vilifika na kila mmoja alijisevia anachokihitaji.
Kuna baadhi ailivijua Khalidi na baadhi ailiishia kuviangalia tu kwa kuhofia kuchafua tumbo kwa ugeni wa vitu vile machoni mwake.
Baada ya msosi na mapumziko mafupi, mziki uliwashwa na kila mmoja aliburudika kwa kucheza na ampendaye.
“twende na sisi tukacheze, hii sherehe ni yako. Au haujaifurahia.” Aliongea Sabra na kutabasamu.
Bila hiyana Khalidi alikubali kuingia kati na kuanza kucheza na bosi yule aliyeheshimiwa na kila mmoja mule ndani.
Baada ya kucheza vya kutosha. Mziki ulizimwa na .sherehe iliishia hapo. Sabra akaondoka na Khalidi na kumpeleka kigogo.
“usije ukanirudishia tena, hiyo ni yako!” alitania Sabra.
“mh…nashukuru sana kwa yote uliyoyafanya juu yangu.” Alishukuru Khalid.
“poa,.. sijui lini tena?” aliongea Sabra na kuonyesha kuwa kuna kitu anakihitaji.
“ ni vyema tukibadilishana namba za simu. Itakiwa rahisi kutafutana.” Alishauri Khalidi.
“wazo zuri.”Sabra alijibu na kuachia tabasamu.
Baada ya kubadilishana namba za simu, Sabra alimkabidhi elfu hamsini na kuondoka zake.
*********************
Sabra akiwa nyumbani kwake, aliliendea kabati na kufungua moja ya Droo za lile kabati na kutoa moja ya album za picha zilizokuwa mule ndani. Alirudi nayo chumbani kwake na kulala kutandani na kuanza kuzipitia picha moja baada ya nyingine. Hakika alitokea kumkumbbuka sana mumewe. Baada ya dakika kadhaa, simu yake ya mkononi iliita. Aliponyanyua simu yake na kutazama screen ya ile simu, alishangaa kuona code number za uingereza. Alijua labda mumewe, lakini aliwaza kwa nini itokee namba ngeni wakati yeye alikua na namba ya mumewe.
Aliopotezea mawazo na maswali yaliyojijenga fasta kichwani kwake na kuipokea ile simu kwa utulivu. Haikua tofauti na sauti ailiyoisikia mwanzo iliyompa taarifa mbaya zilizomstua.
“angalia picha nilizokutumia kwenye e-mail yako ndio utajua kama niongeacho ni kweli au nazusha.” Yule mtu wa upande wa pili aliongea maneno hayo na kukata simu.
Kwa haraka Sabra alinyanyuka na kwenda kuchukua Laptop yake na kurudi nayo kitandani. Alichomeka moderm na kuingia kwenye email yake na kukuta picha kadhaa zikimuonyesha mume wake akinyonyana denda na mwanaume mwenzake.
Aliishiwa nguvu na kuifunga Laptop yake asiendelee kuona uchafu ule.
Wakati akiwa kwenye dimbwa la mawazo, simu yake iliita tena na nammba ileile ya uingereza ikajitokeza tena kwenye kioo cha simu yake. Aliipokea na kumsikiliza.
“nadhani umeona mwenyewe, na ninavyokwambia jumaa pili hii mume wako anaolewa.” Aliongea yule jamaa kwa lugha ya Kiswahili hali iliyozidi kumdatisha Sabra.
“naomba nikuulize, we upo huko uingereza, umenijuaje na umemjuaje mume wangu?, ni nani aliyekupa namba yangu na e-mail yangu?” aliuliza Sabra maswali mfululizo.
“hayo yote utayajua ukifika huku. Njoo ushudie kwa macho yako. Mi nitakua mwenyeji wako na utanifahamu kwakua ni mtanzania mwenzio na nina nia nzuri na wewe.” Aliongea yule jamaa na kukata simu. Sabra alijaribu mara kadhaa kupiga simu, lakini haikupatikana.
Usiku ulikua mrefu sana kwa Sabra. Hakuamini kuwa mume wake mpenzi anaweza kuwa shoga na kuolewa kabisa. Kumbukumbu za kutomuelewa mume wake zilimjia miezi kadhaa iiliyopita. Hakuwa na nguvu ya kurudia tendo wala muda mwingine ilikua kazi sana jogoo wake kusimama sawasawa. Alianza kuamini kutokana na ulegevu wa mumewe toka anamuoa. Maisha ya mumewe yalukua uingereza kuanzia kusoma mpaka anapofanya kazi sasa. Ingawaje alikua chotara wa kiingereza na kibongo kwa mama.
Alitambua fika uingereza kuwa shoga ni kitu cha kawaida. Alifikiri sana na mawazo ya kwenda uingereza siku mbili zijazo yakachukua nafasi ubongoni kwake.
“kuna ulazima wa kwenda kushuhudia kama ni kweli au laa” aliongea Sabra na kukaza macho yake kuonyesha kuwa alichokiisema ndicho anachoenda kutenda.
Baada ya kutimiza vitu muhimu, safari ya Uingereza iliiva na Sabra akakata mawingu kuelekea uingerza. Aliwasiliana na yule mtu aliyempigia simu. Na alipofika alipokelewa na mtu aliyekuja na gari na kumpeleka kwa jamaa.
“kha, Samir??”
Alishangaa Sabra baada ya kumuona mtu aliyekuwa anampa imfomation kuhusu mumewe. Huyu ni rafiki wa mumewe waliokuwa wanasoma wote lakini maisha yake yalikua uswizi. Walioongea mengi ikiwemo juu ya harusi hiyo ya aina yake ya mashoga.
Alipumzika ijumaa na jumaamosi, jumaapili ndio ilikua siku yenyewe ya ndoa.
“wanaoana kanisani kabisa?” aliuliza Sabra baada ya kuona gari likiingia kwenye kanisa kubwa lililopambwa vizuri.
**
Walifurika watu wengi ikiwemo watu ambao wengine Sabra hakuweza kutambua jinsia zao.
Kila dakika ilivyozidi kusogea. Alizidi kutetemeka na kuwa na mawazo. Aliwaza atamuangaliaje mume wake ikiwa ni kweli ndiye muhusika wa ile harusi.
Alishtushwa na vigelegele na makofi yaliyokuwa yanapigwa nyuma yake. Aligeuka haraka na kumuona mwanaume mzee kidogo akiwa amevalia Suti nyeusi na pembeni akiwa mtu aliyevaa shela yenye rangi nyeupe na mapambo ya rangi ya dhahabu wakiingia nule kanisani kwa maringo.
Huku wakishangiliwa na umati wa watu waliojazana mule kanisani, walisogea kwa padri aliyeanzisha sala kwa ajili ya harusi hiyo.
Baada ya sala waligeukiana na bwana harusi akamfunua uso mke wake.
Hamad! Alikuwa mume wa Sabra.
Hapo hapo waliokua kanisani wote waligeuka nyuma baada ya kusikia kishindo. Walimkuta Sabra amedondoka na kuzimia.
Walimtoa kanisani na kumuwahisha hospitali. Na wao wakaendelea na vipengele vya harusi vilivyobakia.
“kesho narudi Tanzania.” Aliongea Sabra baada ya kupata fahamu. Alisikitika sana na hakua na hamu hata ya kumuona tena mumewe.
“umeamini niliyokua nakuambia?” aliongea samir na kumuangalia usoni Sabra aliyekua na uso wa huzuni.
“dunia imeisha Samir, acha nirudi kwetu.” Aliongea Sabra na kuanza kupanga vitu vyake tayari kwa safari.
Akiwa hewani akikata mawingu kurudi Tanzania, kichwa chake kilikua na mawazo mengi sana juu ya mume wake. Aliikumbuka siku waliyofunga ndoa.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO