THE NIGHTMARE (9)

0

SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
“mmenifananisha, mimi ndio kwanza naigia ofisini mida hii.” Aliongea yule afande na kuigia kituoni.

“sasa aliyekuwa anatuhoji ni nani kama sio huyo?”

Alijikuta anajiuliza mwenyewe swali lililompa utata mkubwa kichwani mwake.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
Wakati wakiwa hawajui hili wala lile, walishangaa kuona maaskari wakijazana pale na ambulance ikafika haraka. Wakiwa makini kufuatilia ni nini kilichotokea, walishangaa kuuona mwili wa Amina ukiwa umeraruriwa vibaya huku damu iliyoganda ikiwa imechafua nguo zote alizovaa..

Hali hiyo iliwashangaza sana na kubaki wakiwa wamepigwa na bumbuwazi. Sharji ndio kabisa. Aliamua kuondoka na kukimbia bila kujua alikua anaelekea wapi.

“Sharji,…..Sharji subiri.”

Ilikua sauti ya kaka yake ikimuomba asimame.

Ilikua kama kachanganyikiwa baada ya kuushudia mwili wa Amina. Kumbu kumbu zikamrudisha kwenye boti na kugundua kua ni Amina ndio mtu wa pili kufa. Hapo aliamini si ndoto tena. Hali waliyonayo ni halisi na hakuna atakayesalimika.

Baada ya kukimbia mwendo mrefu, Sharji alichoka na kujibwaga chini. Alijua bila shaka atakua jini Baqlis aliyemuota kwenye ndoto.

Dakika tatu baadae, Karimu na kundi lake walimfikia Sharji pale alipo huku na wao wakiwa wanahema kutokana na kukimbia umbali mrefu.

“kuwa na moyo wa kijasiri mdogo wangu. Hapa inatakiwa leo hii hii turudi kwetu.” Aliongea Karimu baada ya kupumzika kwa muda wa dakika tatu.

“kaka ile ndoto niliyoi….. angalieni kulee”

Sharji hakumalizia kauli yake, kwa mbali alimuona ndege mkubwa mwenye umbo la binaadamu akishuka kwa spidi ya ajabu. Kabla hawajafanya lolote, yule ndege alitua na kumchukua mtu mmoja kati ya watu waliokuwa pale.

Walinyanyuka na kuanza kukimbia kila mtu na njia yake. Baada ya mwendo mrefu. Sharji alianza kusikia sauti ya kaka yake ikimuita huku analia. Alipogeuka nyuma. Alimkuta yule ndege akimkata kata kaka yake kwa makucha yake. Sauti ya kaka yake ikakatika baada ya kushuhudia kwa macho yake kichwa cha kaka yake kikichomolewa na kudondoka chini.

Baada yule ndege kumaliza mauaji hayo, yule ndege wa ajabu mweye umbo la binaadamu, alimuangalia kwa macho makali Sharji na kumrukia

Yule ndege alimchukua Sharji kwa spidi na kuruka naye juu kabisa ya anga. Kutokana na spidi kuwa kali,Sharji hakuweza kuona vizuri kutokana na upepo mkali. Alilia huku akimuomba yule ndege amshushe. Yule ndege alimpulizia hewa yake usoni na Sharji akazimia.

Fahamu zilipomrudia. Alijikuta yupo sehemu nzuri yenye maua mengi yenye harufu nzuri. Akiwa anashangaa mandhari hiyo ambayo hajawahi kuyaona toka azaliwe, alisikia jina lake linatajwa.

Alipogeuka nyuma, alishangaa kumuona msichana mzuri akija kwa madaha akiwa amevaa kofia iliyokuwa na nyavu mbele ambayo ilimzuia kuiona sura ya yule msichana.

Yule msichana alimsogelea na kuivua ile kofia na kuiweka pembeni. Uzuri wa binti huyo ulimfanya Sharji ashtuke baada ya kumkumbuka. Huyo msichana alikuwa ni BALQIS aliyemuota kwenye ndoto yake. Alifikicha macho yake labda alikua ndotoni. Lakini aliamini kuwa haikuwa ndoto baada ya msichana huyo kumsogelea na kumuamuru akae. Bila ubishi, Sharji alikaa na kusikiliza kitu atakachoambiwa.

“pole kwa kufiwa na kaka yako mpendwa.” Aliongea Balqis na kumuangalia Sharji aliyekuwa na wasi wasi mkubwa.

“wewe ni mtu mbaya sana. Kama umeamua kumuangamiza kaka yangu. Unasubiri nini kuniangamiza na mimi?” aliongea Sharji huku akimuangalia Balqis kwa macho makali.

“upo gizani Sharji. Hivi unajua kuwa safari ya Comoro ilikuwa inahusiana na kifo chako?” aliuliza kwa hasira Balqis.

“unamaanisha nini?” aliuliza Sharji kwa mshangao mkuu.

Balqis alinyanyuka bila kuongea kitu chochote. Alinyoosha kidole chake kwenye moja ya maporomoko ya maji yaliyokuwa eneo hilo na kutokea TV kubwa.

“angalia mwenyewe ujionee.”aliongea Balqis baada ya kuiwasha ile tv ya ajabu.

Alionekana Karimu akiwa ofisini kwa baba yake wakigombana kuhusu swala la hela. Karim aliondoka na kwenda kumuhadithia rafiki yake juu ya mzazi wake anavyombania hela za matumizi. Rafiki yake akamshauri kwenda kwa mganga. Walipofika, mganga aliwasikiliza shida yao na maamuzi yalikuwa kumtoa uhai baba yake.

Tukio la uchawi wa mganga kumuingia Khalidi na kusababisha ajali aliuona Sharji kwa macho yake. Baada ya hapo mganga alienda hospitali kummalizia na ndio ukawa mwisho wa maisha ya baba yake na mama yake kufa kwa preasure baadae.

Haikutosha, alimuonnyesha pia baada ya miezi sita kupita. Karim akishirikiana na rafiki yake wakirudi kwa mganga ambaye aliwaambie wafanye kafara ya mwisho ambayo ni kumtoa mdogo wake ampendaye Sharji. Karimu alikubali na kupewa masharti ya kuazisha safari ya mbali na wanapoishi na kumuua huko bila yeye mwenyewe kujua wala kuhisi tukio hilo. Wakishirikiana na marafiki wengine, walipata wazo la kuandaa picnic na kwenda visiwa vya Comoro ambapo watamuua huko.

“nadhani umeona yaliyotaka kukuta… we unafikiri ningefanyaje?... nilikuotesha ile ndoto ili ukatae hiyo safari. Lakini uliidharau hiyo ndoto na ndio maana nikatumia uwezo wangu kuwaangamiza wabaya wako ili mradi wewe uwe mzima.”

Aliongea Balqis baada ya kuzima ile tv kimaajabu. Sharji aliipata picha nzima na hakuamini kuwa kaka yake alikuwa mnyama kiasi kile. Alipigwa na butwaa na kumuangalia Balqis na kujiuliza maswali ambayo yalikosa majibu ya haraka.

“kwanini umeamua kunisaidia?” aliuliza Sharji baada ya kuona ni jinsi gani jini huyo alivyokuwa karibu na yeye muda wote huo.

“mimi narudisha fadhila kwako kwa kunikomboa mimi.” Aliongea Balqis na kumfanya Sharji ashangae.

“nimekukomboa?.. kivipi yaani. Maana hatujawahi kuonana wewe na mimi zaidi ya kwenye ndoto na leo ndio nakuana live.” Aliuliza Sharji kwa mshangao mkuu.

Balqis alinyanyuka na kuileta ile Tv.

Alijiona yeye akiwa na familia yake yote wakiwa Beach. Wakiwa wanaogelea maji ya bahari, alikiokota kichupa kilichofungwa na kukifungua. Alipoona hamna kitu, alikitupa na kuendelea kuogelea.

Balqis alizima tv yake na kuanza kumuelekeza Sharji.

“mimi ni jini mzuri na ninayependa kuwasaidia watu. Pia nina uwezo mkubwa tofauti na majini wengi. Kwa hiyo majini wengi walinichukia na kuniwinda kwa ajili ya kuniangamiza. Walifanikiwa kunikamata na kunifungia kwenye ile chupa miaka mia mbili iliyopita. Siku hiyo ulipoifungua ile chupa. Ulinifanya nitoke na kuwa huru tena. Toka siku hiyo nikaanza kuangalia maisha yako na kuyalinda. Na yeyote aliyekuwa na nia mbaya na wewe. Nilikuwa tayari kupoteza maisha yake. Akiwemo kaka yako na wenzake. Samahani na pole kwa kukupotezea kaka yako uliyempenda lakini ukweli yeye hakukupenda hata kidogo.”

Aliongea Balqis na kumfanya Sharji amshukuru baada ya kugundua ukweli.

“ukijihisi mpweke duniani, unaweza kuishi na sisi huku. Au una semaje?” aliongea Balqis na kuwaita majini wenzake anaoishi nao. Walikuwa wazuri na wenye sura za kuvutia. Walikuwa rika mbali mbali. Na wote walionekana wakitabasamu kama ishara ya utayari wa kumpokea Sharji kama mwenzao.

“nashukuru. Sema naomba unirudishe duniani.” Aliongea Sharji baada ya kufikiria kwa muda.

“sawa. Fumba macho yako. Na nikikuambia fumbua utakuwa umeshafika duniani.”

Sharji alifumba macho yake. Haikupita hata dakika moja. Akasikia sauti ya Baiqis akimuambia fumbua.

Alipofumbua macho yake alijikuta yupo nyumbani kwao. Alishangaa na kuanza kuikagua ile nyumba ambayo ilikuwa haina mtu mwingine zaidi yake.

Alienda kudhuru makaburi ya wazazi wake na kumuombea msamaha kaka yake kwao kwakua alikua hajui alitendalo.

Balqis alimtokea mara kwa mara Sharji na kumpa company alipokuwa mpweke. Alimuokoa na vitu vingi kama ajali na mambo mengi yaliyohatarisha uhai wake.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
MWISHO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)