THE NIGHTMARE (8)

0

SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
Walipofika feri, walipewa nahodha mwingine tofauti na yule aliyemuota na boti ilikuwa ndogo tu ya kawaida tofauti na ile aliyoiota.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
Sharji alijikuta anapiga makelele baada ya kumuona Balqis akiwa amejaa damu mdomoni huku ametoa makucha yake akimfata kwa nia ya kumdhuru.

“AAAAAAAAAAAGH”

Sharji alipiga kelele na kukurupuka. Alipofungua macho yake alishangaa kumkuta kaka yake akiwa ameshika mswaki wake akimuamsha. Alitoa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango baada ya kumuona kaka yake aliyempenda kuwa hai tena.

“Sharji, amka basi ujiandae. Unasubiriwa wewe tu.” Aliongea Karimu na kumuangalia mdogo wake ambaye muda huo moyo ulikua unamdunda kupita kiasi.

Sharji alifikicha macho yake ili kuhakikisha kuwa ni kweli aliyesimama mbele yake ni kaka yake.

Alimsogelea na kuanza kumpapasa kama anamkagua Fulani hivi.

“vipi kwani, umeota ndoto mbaya nini?” aliuliza Katimu huku akionyesha wazi kumshangaa mdogo wake.

“kaka, hivi Balqis yupo wapi?” aliuliza Sharji na kumfanya kaka yake acheke.

“Balqis?.... Balqis ndio nani?... yaani watu uliowaota ndio unanitajia mimi, hebu amka basi twende.”

Aliongea Karimu na kumfanya mdogo wake kutaharuki. Kila kilichomtokea usiku kucha kilifanana na ukweli. Alivuta taswira ya toka jana yake kuanzia aliposikia harufu kali ya perfume ya Baiqis mpaka alipopewa bahasha ya hela. Pia alivuta taswira ya safari ya mashaka ambayo mpaka muda huo alikua haamini yote hayo yalikua ni ndoto.

“twende wapi?” alijikuta sharji akimuuliza kaka yake.

“acha ubwege, we hujui kama leo ndio safari yetu ya kuelekea visiwa vya Comoro?” aliuliza kaka yake ambaye mpaka muda huo aliamini mdogo wake alikuwa na mawenge ya ndoto.

“nyie nendeni tu, mimi siendi popote.” Aligoma Sharji.

“acha utoto wewe, unajua hii safari nimeiandaa kwa ajili yako?” aliongea Karimu kwa hasira.

“tatizo lako kaka hujui nilichokiota juu ya hii safari. Laiti kama ungelijua, basi ungeli ghairi hii safari.” Aliongea Sharji na kumuangalia kaka yake ambaye alikua amekasirika muda huo.

“haya niambie umeota nini?” hatimaye Karimu alimuachia uhuru mdogo wake amuelezee.

“tuache tu kaka, maana inatisha sana.” Aliongea Sharji na kuonyesha hali ya kuogopa kumuelezea kaka yake.

“pole mdogo wangu kwa ndoto mbaya uliyoota juu ya safari yetu. Hayo ni mawenge tu yampatayo mtu yeyote ambaye hajawahi kusafiri majini. So we amka kajiandae tuondoke zetu.”aliongea Karimu kwa sauti ya upole.

Baada ya kubembelezwa sana, Sharji akakubali kiroho upande na kwenda kujiandaa kwa kuoga na kuvaa nguo nyingine tofauti na ile aliyopanga kuvaa hapo awali ambapo aliiota ile nguo.

Alipomaliza kunywa chai, alitoka nje na kuwakuta wasafiri wote wakiwa hai wanamsubiri yeye tu kwenye coaster iliyopaki nje kwao.

Katika watu wote waliokuwa pale, hakumuona Balqis. Ndipo alianza kuamini kuwa ile ilikuwa ni ndoto tu.

Walipofika feri, walipewa nahodha mwingine tofauti na yule aliyemuota na boti ilikuwa ndogo tu ya kawaida tofauti na ile aliyoiota.

Safari hiyo ilianza kwa furaha ya watu wengi kasoro Sharji ambaye bado ana wasi wasi japokuwa upande mwingine aliamini kuwa ile ilikuwa ni ndoto tu na haiwezi kuwa kweli.

Mziki mkubwa ulirindima. Watu walicheza, walikula na kunywa huku wakiburudika kutokana na upepo mwanana uliokuwa unawapuliza.

Walifika salama usalimini safari yao hiyo na kupokelewa na wenyeji wa hotel waliyopanga kufikia na kwenda kwenye vyumba vyao.

Usiku wa siku hiyo hawakulala. Maana wasanii wawili mapacha kutoka Nigeria walikuwa na shoo huko visiwa vya Comoro.

Baada ya kuwashuhudia P.square live walirudishwa hotelini na gari ya hotel na kwenda kupumzika.

Mchana wa siku hiyo walienda kwenye zoo ya wanyama na kuangalia wanyama mbali mbali. Baada ya hapo jioni walirudi hotelini na kuangalia Live band ya huko iliyokuwa ikitumbiza kwenye hotel hiyo.

Matukio yote hayo yalimfanya Sharji kurudi katika hali yake ya kawaida kwakua alikua na hofu kubwa iliyokaa akilini mwake muda mrefu. Sasa alikuwa huru na furaha yake ikajitokeza dhahiri baada ya kuwaona wanenguaji wa kicheza kwa style iliyomvutia.

“ndoto zingine zinaweza kukufanya uwe kichaa.” Aliongea Sharji peke yake na kujicheka ujinga kwa kutaka kukataa kula raha zile ugenini.

Baada ya live band kumaliza. Waliamua kwenda kupumzika kwenye vyumba vyao.

Asubuhi ya siku ya tatu iliwadia na Ratiba ilikua ni kwenda kwenye jumba la makumbusho ya huko Visiwa vya Moroco.

“ Fred anapenda sana kulala. Yaani mpaka muda huu hajaamka?” aliongea mmoja wa marafiki wa Karim.

“si unajua jana alipombeka sana. Sasa tunafanyaje, tunamuamsha au tunamuacha?” aliongea Karim baada ya gari la ile hoteli kuwa lipo tayari kwa safari yao.

“tumuamshe bwana, sio vizuri kumuacha.” Alishauri Sharji .

“poa, kamgongee.” Aliongea Karimu na Sharji akaenda kugonga kwenye chumba alicholala Fred.

“ mbona mtu mwenyewe haamki?” aliongea sharji baada ya kugonga muda mrefu bila ya majibu.

Wote kwa pamoja waliungana na kugonga mlango. Lakini waliambulia patupu.

“itakuwa amepatwa na tatizo. Mtafute manager wa hotel atupe funguo nyingine tufungue.” Aliongea Karimu na zoezi la kumtafuta manager lilianza. Baada ya manager kufika pale, walifungua mlanguo na kupigwa na butwaa baada ya kumkuta Fred yupo kitandani huku akiwa na mapovu mdomoni,

Manager alimsogelea na kuangalia mapigo ya moyo wake, hakusikia chochote.. alipomgusa mwili wake ulikuwa wa baridi.

Manager alimfunika macho na kuwafanya watu waliokuwa pale kujiinamia.

“ameshapoteza maisha huyu. Ngoja tutoe taarifa polisi.”

Aliongea Manager wa hotel hiyo na kuwapigia simu polisi.

Waliuchukua mwili wa Fred na kuupeleka kwenye maabara kwa uchunguzi.

Karim na wenzake waliitwa polisi kwa mahojiano.

Wakati wote wa tukio hilo, Sharji alianza kukosa amani tena kutokana na tukio hilo kufanana na ndoto yake. Maana kwenye ndoto alilala na Fred na yeye kumtoroka na kwenda kulala na Balqis hali iliyomfanya Fred kupoteza maisha wa kwanza katika ndoto yake.

Walipofika polisi walianza kuhojiwa mmoja baada ya mwengine. Ilipofika zamu ya Sharji, alianza kutetemeka huku kijasho chembamba taratibu kikaanza kumtoka. Hata siku moja hajawahi kufika kituo cha polisi. Hali ya uoga ikichanganywa na hali ya wasi wasi juu ya safari hiyo ndio kulimfanya apatwe na kitete.

Baada ya muda alimaliza mahojiano japokuwa alikuwa na wasi wasi mkubwa. Waliingia watu wote na Amina ndio alikuwa wa mwisho kufunga dimba.

Muda ulizidi kwenda toka Amina aingie kwenye chumba cha mahojiano. Hatimaye masaa mawili yalipita bila Amina kutoka.

“huyu askari anamuhoji kweli au anafanya mambo mengine?... maana masaa mawili sasa yameshapita” aliuliza Juma baada ya kuona muda unazidi kuyoyoma bila dalili zozote za Amina kutoka.

Dakika tano baadae, walishangaa kumuona yule askari aliyekuwa anawahoji akiwa ndio anaingia na gari la polisi.

“samahani afande, kwani nyie mpo mapacha?” aliuliza Karim ambaye alimsimamisha yule askari.

“hapana, kwani vipi?.” Alikanusha yule askari.

“sijakuona wakati unatoka ndio maana nashangaa?” aliongea Karim na kumfanya yule askari kumshangaa.

“kwani tumesha onana mimi na wewe leo?” aliuliza yule afande na watu wote waliokuwa pale nje wakabaki wameduwaa.

“jamani maajabu haya, wewe si ulikua unatuhoji ndani!!!?” aliuliza Karimu kwa mshangao mkuu.

“mmenifananisha, mimi ndio kwanza naigia ofisini mida hii.” Aliongea yule afande na kuigia kituoni.

“sasa aliyekuwa anatuhoji ni nani kama sio huyo?”

Alijikuta anajiuliza mwenyewe swali lililompa utata mkubwa kichwani mwake.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)