KITABU CHA SHETANI (7) Jina: KITABU CHA SHETANI Mtunzi: Aziz Hashim SEHEMU YA SABA TULIPOISHIA... “Hapana, sihitaji ambulance, nimekuja na gari langu,” alisema Samantha huku akivaa tena ile nikabu yake na kuuficha uso wake, manesi na madaktari wakasaidiana kumpakiza mgonjwa kwenye gari kisha baada ya hapo daktari mkuu akataka manesi wawili waongozane naye lakini Samantha alikataa, IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI 👉INSTALL👈 TUENDELEE... jambo lililowashangaza wote. Harakaharaka akaingia kwenye gari na kupiga ‘starter’ kisha akawasha taa za mbele za gari hilo, akaondoka kwa kasi mpaka getini. Akiwa anataka kutoka na kuingia barabarani, alishtuka baada ya kuliona gari la baba yake nalo likiwa linakata kona ya kuingia hospitalini hapo. “Mungu wangu!” alisema Samantha kwa hofu kubwa. Harakaharaka msichana huyo alipandisha vioo vya gari lake, akamuona baba yake akivua miwani na kulikodolea macho gari hilo akiwa ni kama haamini. Akaingia barabarani na kukanyaga mafuta kwa nguvu, …