Mtunzi: Omary John Mndambi
SEHEMU YA THERATHINI NA NANE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Sam alipoona ile hali aliamua kuwaaga na kwenda kukaa kwenye kiti chake akachukua simu na kumpigia mkewe na kumuelekeza aje pale alipo.
Pamoja na Sam kuondoka bado amani haikuwepo hata kidogo kati ya Gwakisa na Nisha, Gwakisa alikuwa tayari na donge moyoni na kila alipotaka kuuliza swali alijibiwa kifupifupi sana.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Kiufupi Gwakisa mudi ilimuishia kabisa, kila akimuangalia Nisha alikuwa anajikuta ana maswali kibao ya kujiuliza lakini aanze na lipi hapo ndio palikuwa pagumu.
Nisha aliligundua hilo akamuuliza Gwakisa…
“Kwani una tatizo gani?”
“Sina tatizo kwani umenionaje”
“Nakuona umejikalia tu na mawazo sijui unawaza nini, kama huna la kuongea uniambie tu niondoke zangu mpaka siku utakapokuwa sawa”
Maneno haya ni kama yalizidi kumchefua Gwakisa kwani alidhani angepewa majibu ya kumridhisha lakini ndio kwanza Nisha hajali hisia zake.
“Lakini kwanini hujataka kumwambia Sam kuwa mimi ni mpenzi wako?” aliuloza Gwakisa?
“Haaa wewe una akili kweli, hivi yamekuwa matangazo?”
“Mbona yeye uliniambia wazi kuwa aliwahi kuwa mpenzi wako?”
“Hahahaaaa Gwakisa bwana, hivi wewe unajilinganisha na Sam kweli? Acha masihara kabisa, Sam ni mtu mwingine kabisa”
“Unasemaje Nisha?”
“Bwana wewe kama huna maneno mengine naomba ukanseli mpaka siku utakapokuwa na mambo ya maana ndio tuonane, sawa wewe mwanaume?” aliongea Nisha huku akiamka aondoke.
“Hebu subiri kwanza Nisha” aliongea Gwakisa alipomuona Nisha anaondoka zake.
Pamoja na Gwakisa kumwambia Nisha abaki lakini hakubaki, aliondoka zake akafika nje akawasha gari na kuondoka eneo lile huku akimuacha Gwakisa na kovu linaloota upya ndani ya moyo wake juu yake.
Kwa hasira Gwakisa alipiga ngumi kwenye meza na kusababisha glass zilizokuwa pale zikadondoka chini kitendo kilichowafanya wahudumu wasogee pale.
“Boss vipi kuna tatizo” aliuliza mhudumu mmoja aliyekuwa anaitwa Recho.
“Kum…a wewe, toka hapa!”
Aliongea Gwakisa kwa hasira akimuondoa mhudumu wake.
Yule mhudumu badala ya kuondoka aliinama akakusanya vipande vya Glass vilivyokuwa vimetapakaa pale chini ili akavitupe.
Alipokuwa ameinama alishtuka anashikwa makalio, aligeuka haraka na kukutana na sura ya Gwakisa akimuangalia huku bado kashikilia yale makalio hadi Yule muhudumu akajisikia aibu.
“Alafu wewe mzuri sana ujue, haya nipelekee whisky moja kule VIP nakuja” aliagiza Gwakisa.
Katika ile baa ya Gwakisa kulikuwa na sehemu ya VIP ambayo ipo kwa ndani nah ii hutumiwa na wageni wenye hadhi ambayo haiwaruhusu kukaa changanyikeni, sehemu hii hata vinywaji vyake huuzwa bei kubwa nah ii ndio hata Gwakisa akija na marafiki zake hupenda kukaa.
………………………………
Rafiki alikuwa kazini kwake ofisi ya hazina mkoa anafanya majukumu yake ya kila siku akasikia mlio wa simu yake na kuiendea.
“Haloo mambo baby”
“Mh makubwa leo…poa niambie”
“Makubwa gani sasa, ”
“Leo napigiwa simu na Kuitwa baby juu”
“Sasa hapo jipya lipi na nyie wanawake hamjui kupendwa nyie”
“Haya babu niambie mpenzi”
“Poa tu vipi uko kazini bado?”
“Ndio ntakuwa wapi na hii ni mida ya kazi jamnani”
“Haya aga basi uje hapa tulikokuwa siku ile nina ishu, chukua hata tax ntalipa”
Rafiki alipatwa na kiwewe baada yam me wake kumuita mida kama ile, alijiuliza sana lakini mwisho akaamua kumuaga rafiki yake kuwa anatoka hivyo amsaidie majukumu yake itakapobidi.
“Mh shoga mbona mbio mbio hivyo, umepata mchepuko wenye hela nini” aliuliza rafiki yake Rafiki mke wa Sam
“Weee, ishia hapo hapo, hivi unaweza kuwa na mume kama Sam alafu ukamtafutia mchepuko kweli?”
“Haya shoga nenda, Sam sam kitu gani amekuwa wa dhahabu nini, omba Mungu asiingie kwenye anga zangu atakusahau” alitania shoga yake Rafiki.
Rafiki hakulijali hilo, alitoka nje akachukua bodaboda mpaka alipoagizwa.
Alipofika pale alimuona Gwakisa akielekea ndani ya ile baa na hapo hapo akamuona mme wake akiwa ameketi pembeni kwenye kona anakunywa Red Bull.
Rafiki alimuendea alipomkuta akamuinamia na kumpiga busu shavuni lakini Sam yeye alimvutia mpaka mdomoni kwake na kuanza kumnyonya mdomo palepale bila kujali wateja wawili watatu waliokuwepo pale mida ile.
“Karibu mpenzi”
Aliongea Sam wakati anamuwekea Rafiki kiti aketi, ile Rafiki anaketi tu hapohapo aliingia na Glory ambaye ni mdogo wake SAM.
Glory aliungana nao pale kisha wakaambiwa waagize wanachojisikia kulak wa wakati huo na kwakuwa ilikuwa bado ni mapema hata saa saba bado waliagiza michemsho ya kuku mzima kila mmoja na kuanza kujiachia.
“Haya tuambie mwenzetu ndio nini kutuita mida hii?” aliuliza Rafiki.
“Malizeni kwanza kula haa” alijibu sam
Mwisho wote wakawa wamemaliza kula na kunawa mikono.
Sam aliingiza mkono wake mfukoni akatoa bahasha yenye barua ndani na kumkabidhi mkewe ambaye aliifungua haraka haraka na kuisoma.
Alipomaliza alijikuta ameshika mdomo kwa hamaki, “Wifi naomba namimi nisome” alisema Glory na kupewa barua hiyo
Wakati huo huo Rafiki alikuwa bado kamkata jicho Sam la mshangao, alipoona haitoshi alinyanyuka na kumuendea mme wake pale alipokaa na kumkalia kisha akapitisha mikono yake kwa nyuma na kumkumbatia.
“Jamani mme wangu ….yani siamini hongera jamani” aliongea Rafiki huku akiwa anampiga mabusu mme wake
Sam nae hakuwa nyuma alipitisha mikono yake kiunoni pa mkewe na kuwa amemshikilia vizuri pale alipomkalia,
Kitendo cha mikono ya Sam kupita kiunoni kwa Rafiki kilimfanya ashtuke kwa mahaba kwani alipokuwa anashikwa na mmewe kiunoni basi mashetani yake huamka.
Sam aliligundua hilo ikabidi amkonyeze mkewe kwani mdogo wake alikuwepo Pale,
Kwa shida Rafiki alimuachia Sam na kukaa pembeni, Glory nae alimaliza kusoma ile barua na kujikuta machozi ya furaha yakimtoka kisha akaamka na kwenda kumpa kaka yake mkono akimpongeza.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Asanteni sana jamani, nimeona niwashirikishe furaha hii kwani nyinyi ndio watu wangu wa karibu, ninyi ndio familia yangu, niko nanyi kwenye raha na tabu…nawapenda sana” aliongea Sam kwa hisia kali sana zilizomfanya alengwe na machozi.
Sikia Mme wangu, kunywa bia utakavyo ntalipa, nataka leo uwe na furaha hadi mwisho jamani…
“Mh mke wangu mida hii hata nikikutwa hapa si aibu kweli”
“Twende VIP” Sam hakuwa na kipingamizi, hakutaka kumkera mkewe aliamua kunyanyuka na kuelekea VIP lakini Glory yeye alisema anawasubiri pale kisha wakamwambie ale na kunywa chochote atakacho.
Sam na Rafiki waliingia kule VIP wakiwa wamekumbatiana kwa bashasha, walipofika walipulizwa na kiyoyozi kwa mbali kisha wakatafuta kochi lililokuwa sehemu nzuri na kukaa.
Alipokaa Sam Rafiki alikuja juu yake na kumkalia.
Haraka haraka mhudumu aliwafwata na kuwataka waagize kisha wakaagiza wote Heineken na kuanza kunywa.
Ndani ya dakika kadhaa Rafiki alitupa jicho lake mbele na kuona kitu kilichomshitua kidogo apaliwe na bia.
“Sam hebu angalia Yule sio shem Gwakisa”
Sam aliangalia kule alipoelekezwa na kumuona kweli Gwakisa akiwa amekaliwa na mwanamke mwenye makalio makubwa wanashikana shikana.
Akili ya Rafiki ilibadilika ghafla na kuona kama vile yeye ndie anafanyiwa usaliti ule na kujikuta roho inamuuma sana.
Sam alilijua hilo na kumvutia mkewe kwake na kuanza kumnyonya mate, alimnyonya midomo kwa lengo la kumpoteza kwa kile anachokiona.
“Achana nao na nakuomba usimwambie Verity chochote, utawavuruga”
Rafiki aliitikia kwa ishara ya kunyanyua uso juu na kuushusha, waliendelea kunywa pombe huku Gwakisa na Yule mwanamke wakipelekana juu ghorofani
………………………..
Gwakisa alikuwa na stress nyingi sana, aliumia sana moyoni kuachana na Nisha katika mazingira kama yele.
Hakutaka kurudi nyumbani akiwa hajatembea na mwanamke mwingine na ndio maana alivyomuona Yule mwanamke mhudumu wa kwenye bar yake hakusita kumtamani haraka haraka.
Walikunywa wisky ya kwanza ikaisha wakaagiza na nyingine na yenyewe ikawa inaisha.
“Hey meneja njoo mara moja” Gwakisa alimuita meneja wake ambaye alikuja haraka haraka.
“Huyu yuko zamu, sindio?” Gwakisa aliuliza akimaanisha Yule msichana aliyeko pale kama yuko zamu.
“Ndio bosi”
“Basi leo mpe off, mtoe kwenye zamu ana kazi maalum, nae leo kawa bosi”
Gwakisa aliongea hayo huku Yule mhudumu akimkunakuna kidevuni.
……………………
Verity alikuwa amefura kwa hasira amesimama nje ya ofisini kwao anasubiria Boda boda, alikuwa anatamani hata akimbie kwa miguu kwani hasira alizokuwa nazo alitamani hata kuua mtu.
“Leo watanitambua, nitaua leo” alijiongelesha Verity akiwa amekabwa na donge la wivu na hapohapoo Boda boda ikaja na kupanda kisha akamuelekeza Dereva…
“Endesha fasta nipeleke Rungwe Hotel and Executive” hili ndio lilikuwa jina la hoteli na Bar ya Gwakisa na hapo hapo Bodaboda ilitimua Vumbi!
Gwakisa alikuwa chumbani na mhudumu wake wanahondomola, kwa pombe walizokuwa wamekunywa ziliwafanya wafanye mapenzi ya kufuru.
Walikiuka mpaka miiko kwani mitandao yote ilikuwa inatumika, yaani kuanzia voda mpaka tigo, walipochoka waliendelea kunywa pombe na kurejea tena mchezoni.
Safari hii Gwakisa alikuwa kamlaza Yule mhudumu kwa kuangalia chini na kuwa makalio yako kwa juu huku kaishikilia miguu yote miwili nayeye akiwa kasimama pembeni ya kitanda kitendo kilichomfanya Yule mhudumu awe kama vile kalalia kifua tu.
Kazi aliyokuwa anaifanya Gwakisa ilichanganywa na hasira na ulevi aliokuwa nao kichwani,
Huku wakiwa wanajiachia vilivyo walisikia mlango unagongwa kwa fujo, hapo ilibidi washtuke na kusitisha walichokuwa wanafanya.
Gwakisa alinyanyuka na kuvaa nguo yake huku mlango ukiendelea kugongwa kwa nguvu, walijiuliza ni nani anayefanya kitendo hicho lakini hawakuwa na uhakika.
Gwakisa hakuwaza kama anaweza akawa ni mkewe kwani aliamini mkewe yupo kazini na hawezi kuwa na taarifa za uwepo wake hapo.
Akili yake haraka haraka ikadhani huenda ni Nisha kwani ndie ambaye alikuwa hapo muda sio mrefu
Alimshauri Yule mhudumu ajifiche bafuni na kisha alipofanya hivyo akafungua Mlango kwa tahadhari.
Ghafla kama mshale alizama Verity ndani huku akiwa amefura kwa hasira anahema juu juu,
“We mwanaume Malaya kama wewe sijawahi kuona…niambie Malaya mwenzako yuko wapi?”
Gwakisa alikuwa kapigwa na butwaa akawa anashangaa tu, wakati huo Verity yeye akawa anaangalia kila sehemu ya chumba.
Kwa ujasiri Mkubwa Verity alizama bafuni na kutoka na mtu anamburuza,
Ki uhalisia endapo Yule msichana kwa jina la recho angeamua kufanya mbaya kwa Verity angeweza kabisa kwani alikuwa na umbo kubwa kuliko la Verity lakini pia yeye alikuwa mzoefu wa mambo kama yale sio kama Verity mtoto wa Mboga saba.
Gwakisa bado hakuelewa afanye nini wakati Verity anaendelea kufanya yake…
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)