Mtunzi: Omary John Mndambi
SEHEMU YA HAMSINI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Kwakuwa aliikuwa amefanana sana na mwanae japo alikuwa wa kiume ilikuwa Rahisi sana kumwambia Gwakisa kuwa ni mwanae na Gwakisa hakukataa kwani hata hivyo alikuwa na hamu sana ya kuitwa baba baada ya kusingiziwa mtoto wa kwanza.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Verity aliamua kumpa Gwakisa Yule mtoto kwani alijua bila hivyo Gwakisa atazeeka bila kuitwa baba lakini pia Dr Kelvin alishafariki hivyo mtoto wake angeyakosa mapenzi ya baba.
Gwakisa pamoja na kutengana na Verity lakini alikuwa anamtembelea na kumpa mahitaji yote kwani kulingana na Verity kujifungua kwa Operation ilibidi akae bila kazi kwa muda mrefu. Hatimaye mpaka Verity anatoka ndani baada ya kumaliza maternity alikuwa amenona na kupendeza sana.
Urembo wake ulirudi mara dufu zaidi ya awali, stress za kuwa muathirika alishazizoea na kuona ni ugonjwa wa kawaida tu, semina alizokuwa anapewa alijikuta akiamini kuwa ukiwa na UKIMWI unakufa tu kama binadamu wengine na unafurahia maisha kama watu wengine.
Alijiona akiwa na amani huku akiendesha shughuli zake na miradi kwa kujua kuwa anatakiwa amuachie mwanae urithi hapo baadae.
………………………………………..
“Unakumbuka ahadi yangu”?
“Ipi?”
“Ile niliyokuwahidi kwamba itakuwa zaidi ya ZAWADI YA USHINDI kwenye riwaya za F.M. Topan?”
“Oooh nimekumbuka”
“Ennh kwahiyo uko tayari kuipokea?”
“Niko tayari hata saivi tena naitaka sana”
“Basi jiandae twende sehemu ukapate zawadi yako”
Sam japo alikuwa na hofu lakini alikubali kuingia kwenye gari moja na NISHA kisha wakawa wanaenda sehemu ambayo alikuwa haijui. Mapigo ya moyo wake yalikuwa kasi sana kwani NISHA alishafanya jaribio la kumuua hivyo hata kwa wakati huu akawa hamuamini kwa asilimia zote.
“NISHA”
“Niambie baba”
“unanipenda?”
“Kuliko kitu chochote”
“Basi usije ukaruhusu mtoto wako aishi bila baba”
“Acha uoga we si mwanamume….!”
Nisha alisema vile kwani alijua hofu iliyokuwa ndani ya moyo wa Sam…
“Nimekuahidi Zawadi kwhiyo jiandae kwa zawadi na sio kitu kingine”
“Haaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!” Sam alishtuka baada ya kuiona zawadi iliyokuwa mbele yake, hakuamini na machozi yalianza kumwagika usoni mwake.
“NISHA WHY?” (KWANINI?)!
“Nisamehe Sam!”
Verity alikuwa mwanamke mrembo sana, dawa alizokuwa anameza, tumaini la maisha aliyokuwa nayo vilimfanya aishi maisha ya amani sana, hali yake kimwili ilikuwa ya kuvutia, rangi na umbo lake vilimvutia mtu yeyote aliyekutana naye.
Pamoja na huduma kuhusu mtoto ambazo zilikuwa zinamfanya Gwakisa awe anaonana na Nisha mara kwa mara lakini pia urembo aliokuwa nao Verity ulimfanya Gwakisa awe anavutiwa kuwa nae wakati wote.
Kuna wakati alitamani kumwambia warudiane lakini alishindwa, alikosa jinsi ya kumuanza kwani talaka aliziandika yeye mwenyewe.
“Haloo habari Dada Verity”
“Salama tu habari za kazi Kaka”
“Nzuri tu, uko wapi?”
“Niko Nyumbani ”
“Nakuja ili tumalize ile kazi”
“Sawa karibu sana”
Ni Verity alikuwa anaongea na mtu kwenye simu wakiahidiana kuonana hapo nyumbani, Gwakisa alikuwa ametegesha masikio akitaka kujua ni nani anayeongea na Verity.
Alitamani amuulize lakini akasita, wakati huo Nisha alimuacha akaingia bafuni akaoga na kuvaa vizuri kisha akasogea pale sebuleni alipokaa Gwakisa.
“Vipi unatoka?”
“Hapana kuna mgeni wangu anakuja”
“Ndio maana umependeza hivyo”
“Mbona kawaida tu, siwezi kuwa vile mbele ya mgeni ninayemheshimu”
Kauli ile ilimuuma Gwakisa akijiuliza ina maana yeye haheshimiki! Ndani ya muda mfupi Gari ilikuwa inapiga honi getini ambapo VERITY aliamuru iruhusiwe kuingia ndani.
Baada ya kuingia ndani alishuka kijana mmoja mweupe mrefu aliyevaa nadhifu huku mkononi akiwa kashika notebook ndogo.
“Karibu sana kaka”
“Asante sana”
Baada ya utambulisho mfupi Verity na Yule kaka walitoka mpaka nje kwenye veranda ndogo iliyokuwa na makochi na meza ndogo kisha wakakaa na kujadili mambo yao.
Kule ndani alipokuwa Gwakisa moyo wake ulikuwa unafukuta kwa wivu. Alikuwa anajiuliza inakuwaje mwanamke aliyemuacha kwa maradhi leo hii wengine wanampenda!
“Nilikosea sana kumuacha” alijisemea Gwakisa
Wakati akisema hivyo wazo lingine lilimjia kuwa huenda Verity hakumpenda, lakini kwanini? Hapo alizidi kujiuliza na kujisikia vibaya.
Kwa hasira aliamua kufungua mlango mwingine na kuondoka zake bila hata kuaga, aliwasha gari lake na kuondoka kimya kimya akaelekea Bar kwake na kuanza kunywa poombe kwa fujo.
Huku nyuma verity alimaliza maongezi na mgeni wake ambae walikuwa wanasainiana mkataba wa kusuply Kuku wa Nyama kwenye hoteli maaraufu pale Mbeya alirudi ndani ila hakumuona Gwakisa.
Akiwa anajiuliza kwanini ameondoka bila kumuaga iliingia sms kwenye simu yake,
‘yani ndio unaleta mabwana zako hadi nikiwepo, poa bwana’
Verity alishtuka sana asiamini kuwa Gwakisa anaweza kumtumia sms ya vile, alijiuliza kwani hata ingekuwa ni kweli yeye inamuuma nini!
“Huyu mwanaume ana matatizo huyu” alijisemea Verity
……………………………………………………………………………………………..
Ndani ya Jumba lililokuwa chini ardhini mbele kulikuwa na darasa lenye watoto wengi zaidi ya aarobaini waliovalia nguo nadhifu na wenye afya njema.
Kati ya wale alikuwepo mtoto Nice ambaye alikuwa amekua na kupendeza sana. Sam alikuwa ameshika mdomo asiamini kile anachokiona.
Alikuwa anamwangalia Nisha usoni ambaye nae hakukwepesha macho yake akawa anamuangalia sam Vilevile.
“Mwanao huyo Sam”
“Hii ndio zawadi yenyewe?”
“Ndio hiyo Sam”
“Why Nisha”
“Don’t ask why” (usiulize kwanini)
Sam alikuwa na furaha mooyoni lakini pia alikuwa na hasira na alipaanga kufanya jambo baya juu ya wale watu endapo atatoka pale salama na mwanae.
“twende Sam”
“Wapi Nisha wakati sijamsalimia hata mtoto”
“Twende atakufwata”
Walitembea hadi sehemu kulikokuwa na mandhari nzuri kisha wakakaa hapo na baada ya muda akaletwa Nice.
“Nice huyu ni baba yako”
Nice baada ya kuambiwa vile akawa anamuangalia Sam kwa kumkagua kisha akatikisa kichwa kuashiria kukataa.
“Not my dady” sio baba yangu
“Who is your dady?” baba yako ni yupi.
“That one over there” Yule pale.
Nice alimuonyeshea kidole Baba mmoja aliyekuwa ameketi kwenye kiti kizuri chenye muonekano wa kimamlaka.
“Ndio mimi ndie baba wa hawa watoto wote” Yule baba alidakia
Gwakisa alipigwa na butwaa kwa kauli zile alizozisikia.
“Haya tuondoke mtoto amekukataa”
“Usiniambie kitu hicho hata kidogo, nitavuruga watu wote hapa na hamtaamini”
“Usijitafutie matatizo kijana”
“Unasemaje? Unajua mimi ni nani?” Sam alichimba mkwala kwa hasira.
“Tuondoke Sam”
“Nitaondoka endapo nitakuwa na Mwanangu”
“Huwezi kuondoka nae Sam”
Kwa hasira Sam alimshika Nice kwa nguvu na kuanza kutembea akitafuta sehemu ya kutokea. Katika hali ambayo hakuitegemea alikuja kijana mdogo mwembamba akaanza kumshiniiza asimame na amuache mtoto lakini Sam alizidi kusonga mbele.
Yule kijana alisimama mbele yake na kuzuia njia. Kwa hasira Sam alimshusha mtoto na kumwendea Yule kijana ili ampige.
Alipomfikia alirusha ngumi ya nguvu akiwa ameilenga usoni lakini ilipita kama upepo, alirusha nyingine nayo ikapita kama upepo.
Aliamua kutumia mateke alirusha zaidi ya mateke manne lakini la nne liliishia kupiga ukutani.
Sam alipoona vile alichomoa bastola ili aifyatue lakini kabla hajavuta triga alishtukia ile Bastola ikiangukia mbali baada ya kupigwa teke kali lililokuja kwa kasi ya ajabu.
Sam ilibidi amuangalie vizuri Yule kijana kwa kumkagua. Bado hakuamini kuwa Yule kijana ndie wa kumsumbua kiasi kile kwa mwonekano ule alio nao.
Sam aliamua kumfwata ili amkamate kwa nguvu. Alipeleka mikono yake shingoni mwa Yule kijana lakini miikono yake ilishikwa kwa nguvu hadi akasikia mifupa kama inasagana.
Aliugumia kwa maumivu makali hadi machozi yakawa yanamlenga. Huku akiwa anaugua kwa maumivu alijikuta anapigwa kidogo tu eneo la shingoni kisha akaanza kuishiwa nguvu na macho yakapoteza nuru yake mwisho akawa anaona giza tupu.
………………………………………..
Alizinduka baadae sana akajikuta amekaa mbele ya wanaume wanne waliovalia mavazi kama wa Nigeria huku Nisha akiwa amekaa pembeni akiwa na NICE.
“Karibu bwana Sam”
Sam alikuwa anaangaza angaza macho kama mtu aliyetoka usingizini huku akirudisha kumbukumbu taratibu.
Walipohakikisha kuwa kumbukumbu zake zimekaa sawa wakamletea Karatasi zenye mkataba ambao Sam alitakiwa kusaini.
“Mheshimiwa tunaomba usaini hapo”
Sam alibaki amekodoa macho tu,
“Soma vizuri alafu usaini”
Sam alianza kusoma ule mkataba wote kisha akashusha pumzi nzito, alichukua zile karatasi kwa lengo la kuzirudisha lakini alivyommwangalia mwanae Nice akachukua kalamu na kusaini ule mkataba.
Alipomaliza kusaini tu akasikia makofi yakipigwa kuashiria kumpongeza.
“Hongera sana Mr Sam Mda sio mrefu utakuwa RPC kwenye mkoa tunaokuhitaji”
Sam alishtuka baada ya kusikia vile akijiuliza hawa watu wana uwezo gani wa kuamua mambo yanayohusu jeshi la Polisi.
“Unajua Bwana Sam ulikuwa unapaswa kujiuliza siku nyingi kuhusu ofa ulizokuwa unapata za kwenda kufanya mafunzo nje ya nchi huku ukipanda vyeo haraka haraka”
“Enheee” sam alijibu
“Hiyo ni kazi yetu”
…………………………………………………….
Sam, Nisha na NICE walikuwa wako kwenye gari wanarudi nyumbani. Ndani ya akili ya Sam alikuwa anawaza ni jinsi gani atamwambia Verity kuhusu Yule mtoto.
Aligeuza macho yake akamuangalia NICE ambaye alikuwa amelala usingizi fofofo kisha akaendelea kuendesha Gari.
Walifikia Nyumbani kwa Nisha akamuacha NICE pale kisha akarudi nyumbani kwake huku kichwa chake kikiwa na mawazo mengi sana.
Akiwa kwenye mawazo simu yake iliita.
“Habari ndugu Sam”
“Salama habari yako”
“Nzuri tu naomba kuonana na wewe hapa ofisi za NBC mjini kati”
Sam aliwasha gari haraka haraka na kuelekea kule alikoitwa na kukutana na Yule aliyempigia simu ambaye alikuwa ndie meneja wa ile benki.
“Tunaomba usaini kuingiziwa kiasi cha hii fedha kwenye akaunti yako”
Sam alishangaa kwani kiasi kile kilikuwa kikubwa sana na hakujua ni kwa ajili ya nini……
Katika akili ya Verity hakutaka kuwaza tena kuhusu mapenzi, alichotaka yeye ni kumlea mwanae pamoja na kuendeleza miradi yake. Kwake suala la mapenzi hakulifikiria kwani aliamini mapenzi ndiyo yaliyomfikisha hapo alipo, maradhi aliyo nayo pamoja na kuvunjika kwa ndoa yake aliamini yote ni kwasababu ya kuendekeza mapenzi. Hakutaka tena mapenzi yawe sehemu katika maisha yake yaliyobaki.
Katika kulisimamia hili aliamua kujiweka bize sana na kazi zake za ofisini pamoja na miradi mbali mbali, swala la starehe aliliweka kando akawa ni mtu wa sala kila wakati.
Pamoja na hayo maamuzi yake lakini kupendeza kwake na muonekano alioupata akiwa kama binti ambaye hajawahi hata kuzaa mbele ya macho ya watu ikawa ni mtihani.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)