Notification
Tidak ada notifikasi baru.

VAMPIRE NUSRATY (5)


SEHEMU YA TANO
TULIPOISHIA...
Nimchinje ilikuwa saa nne Asubuhi hatimae ikatimia saa sita mchana muadhini akadhini…."

Mawaidha yakaanza

Nikatulia kimyaa kusikilia maana niliweza kuyasikia vyema.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
“ndugu zangu Waislamu khutuba yangu ya leo itahusu Madhambi makubwa kabisa ambayo kamwe Allah (s.w.t) hatoweza kukusamehe kamwe mpaka unaingia kaburini na kesho

Kiama

Kwanza kabisa kuuwa kwa

kukusudia hii dhambi moja wapo hata kama utajenga misikiti billion.

hata kama utaswali kila sekunde hakika wewe ni wamotoni tu,

hii dhambi ya kuuwa kwa

kukusudia inaendana kabisa na dhambi ya kujiuwa maana utakuwa umeizurumu nafsi yako,

ewe ndugu yangu iyepuke dhambi hii

kwanini uuwe wakati Allah amekataza, kwanini ujiuwe wakati unajuwa kabisa umejiangamiza?"

Hakika ya Allah ndio mjuzi wa yote.

Ametakasika kila jinsi ya sifa njema anastahiki,

Dhambi ya pili na nikubwa mno ni Shirki yani kwenda kwa waganga sijui kutaka utajili au mtoto kivyovyote vile itakuwa ni shirki hakuna Apasae kuabudiwa wala kuombwa

Zaidi ya Mwenyezi mungu hivi jiulize kitu kimoja unaenda kwa mganga kutaka utajili kwani yeye hautaki huo utajili au?…..

Unataka mtoto wakati yeye mwenyewe analia usiku na mchana kutaka mtoto

Siku Allah akakuruzuku kupata

Mtoto utaanza kumpa sifa kedekede yule mganga…yani unasahau kabisa aliyekuumba ni nani,,,

Hakika nikajikuta nasitisha Zoezi langu la kutaka kuuwa,

Sijui huyu shekhe aliambiwa kama

Hafidhi leo anataka kutenda

kitendo hiki au vipi?"

Baada kuswali nikatoka zangu

msikitini

nikamuona Hasina akiwa na wasichana wenzie.

Nae akaniona akaja mbio na kunisalimia huku akinipa kiganja cha mkono kwa kukiweka kwenye kanga,

Siku zote Waislamu haturuhusiwi kushikana nyama kwa nyama yani baina ya Mwanaume na Mwanamke.

Asiekuwa halali yako,

“Assalamu alaykum warahamatullah wabarakatur ewe Hafidhi?"

Kiroho safi nikaitikia wakati huo kisu changu kipo kibindoni

Asingekuwa Shekhe leo

Wallahi ningemchinja,

“Waleykum ssalamu warahamatullahi wabarakatur yaa ukhty"……

Akaniambia

“Kwanza pole sana kwa msiba Hafidhi nikuulize kitu?"

Nikaitikia

“Asante sana nishapoa ndio niulize!"

Akaniambia kama sitojali twende tukakae sehemu,

Basi tukatafuta sehemu nzuri yenye utulivu akanitizama ukimya wa kama dakika mbili hivi ukatanda

kisha akavunja ukimya kwa kusema

“Wacha nikupe historian ya Nusraty,

Nikamtizama na kumuuliza

“Nini!?"

Nilikuwa na shahuku ya kutaka kuifahamu hiyo historia ya maisha ya

Nusraty, basi

Hasina akaanza kunisimulia,

“kwanza kabisa Dada tokea akiwa mdogo alikuwa na wadudu kichwani.

Nikamkatisha kwa kumuuliza

“alikuwa na wadudu kichwani kivipi na hao wadudu ni wepi?"

Hasina akanitizama kisha akanijibu na kuendelea kusimulia

“Binafsi ninapozungumzia wadudu ni Mashetani, ndio alikuwa anaishi nao kichwani kwake

Hakika walimtesa sana

yani walikuja saa yeyote ile na kuanza kupandisha iwe kwenye daladala au shuleni popote pale

Kwa siku alikuwa anapandisha zaidi ya mara tatu au mbili

Kila siku zilivyozidi kwenda Dada akazidi kukonda basi Mama

Akampeleka kwa Shekhe huko bagamoyo akachanjwa mgongoni

Kisha akapakwa dawa

yule Shekhe akamsomea pale

Huku akimpiga piga kichwani na usinga sijui mkia wa ng'ombe au mbuzi,

Hapo nikamkatisha tena kwa

Kumwambia

“please huyo sio Shekhe ni mshilikina anaechafua hadhi za Mashekhe wetu tambua kitu kimoja

Unapoenda kwa Shekhe kusomewa kwanza ukikuta sijui vitambaa vyeusi vyekundu na nyeupe

tena ana kibuyu na pembe ya mbuzi au ng'ombe tambua huyo sio

Shekhe hata kama anaswali swala tano au Anafundisha madrasa huyo

Hafai kabisa mbele ya macho ya jamii

Shekhe wa kweli anakusomea au kukuandikia thafarani basi!"

Hasina akatabasamu na kusema

“basi sawa tuseme ni mganga baada kufanya matibabu yule Mganga akasema Jini makata anataka Pete ya Almasi huku Maimuna akitaka Pete ya dhahabu,

Baba akauza kiwanja chake kimoja ili aweze kumnunulia Nusraty hizo pete

Baada kuveshwa na kufanyiwa

Tambiko kwa kuchinjiwa mbuzi kama kafara kila kitu kikatulia akawa apandishi tena akaanza kunenepa

Mpaka siku aliyokufa,

kifo chake kilikuwa cha utata sana

Yani aligongwa na nyoka akiwa jikoni anapika akapiga kelele ghafla akawa kimya,

Hata tulipofika tulimkuta Dada tayari ameshakufa,,,,

Hasina akaanza kulia nikaitaji kumshika nimbembeleze nikasita

kwa sababu pindi Mwanaume na Mwanamke

Wanapojitenga kwa kukaa peke yao wawili tu basi watatu yake ni Sheitwani, kwakuwa alizidi kulia hakika kama alijitonesha kidonda ambacho kilikuwa kishapona na kubaki kovu tu.

Nikamshika kichwani kisha akajiegemeza kifuani kwangu. Nikamsihi asiendelee kulia, baada kumbembeleza kwa muda kidogo,

Hasina akanyamaza na kunyanyuka ili aende nyumbani kwao. Nikaona si vyema kumuacha mtoto wa kike kama yule aende nyumbani kwa peke yake. Japokuwa ilikuwa mchana wa saa 8 na nusu,

Nikamsindikiza huku nikimpa maneno ya kumfariji, ajabu

Hasina mwendo wake haukuwa wa kawaida alikuwa anayumba yumba huku akinesa

Tulipofika karibu na nyumbani kwao akadondoka chini.

Nikawai kumdaka haraka sana nikapaza sauti kuita msaada

Ndipo wakaja Wazazi wake, hawakuuliza kitu zaidi ya Kaka yake kumbeba na kuingia nae ndani, nikataka kuingia na mie nikazuiwa na Baba yake

Hasina akaniambia

“kijana tunashukuru sana kwa msaada wako wee nenda nyumbani tu",,,,,,

Kisha akafunga mlango na kuniacha na maswali kibao kichwani.

Hatimae siku hiyo Usiku ukaingia nikiwa nimekaa Mimi pamoja na Baba

Ajabu Baba akaniuliza swali,

“hivi Hafidhi mwanangu kwanini unakuwa na roho ya kinyama namna hiyo?"

Nilishangaa sana kutokana na lile swali nikauliza,

“Baba unamaanisha nini kuniuliza hivyo?

“Najuwa hujui lakini unajuwa kabisa baada kumuuwa Mama yako unataka kuniuwa na Mimi sio yani mtoto mshenzi kabisa haufai!",,,,,,

Nikajikuta nainuka pale nilipokaa nikabwata kwa sauti kubwa nikavunja adabu ya kutowatolea sauti kubwa Wazazi wetu hakika ni dhambi kubwa sana leo hii si ajabu kumuona Binti akimwambia Mzazi wake

Eti unabahati umetangulia vinginevyo ningekuzaa…(Astaghafilullah)..

Yani wewe ungemzaa Baba yako au Mama yako kumbuka ni laana kubwa hiyo…

yani unapandisha sauti kumsuta Mama yako kisa fitina za mkeo au Mumeo ni ujinga huu tena ni laana kubwa kabisa….

Sasa mie maneno ya Baba kusema nimemuuwa mkewe eti bado yeye nikajikuta napayuka tu.

“wee Mzee shika adabu yako usiniletee bange zako hapa,,,,"

Akaniuliza huku na yeye akiwa kanyanyuka…..

“Eti Hafidhi mimi nishike nini,,,,leo hii mie navuta bange sio?….kwa hasira Baba akanipiga zinga la kofi ajabu sikuweza kusikia maumivu yeyote Yale zaidi ya Baba kuanza kulia huku akiwa kaushikilia ule mkono alionipiga kofi,

“Hii mkono wangu,,,,,ayaaa,,,uwiiiiiiiiii

….Baba akadondoka chini huku akitapatapa nikaita kwa sauti huku nikimshika

“Baba!!!baba,,,,,,"

Nikamuona Dada na ndugu wengine ambao walikuja kwenye msiba wa Mama walikuwa bado hawajaondoka wakaja mbiombio na kuuliza

Kunanini kimetokea kumbe nyumbani alikuja mganga maana nae akatoka ndani ajabu

Aliponiona mimi tu akatoka mbio ajabu huku tunguri zake akizitupa ndugu baada kuona vile nao

Wakanihofia.

Nikabaki nikijiuliza maswali mazito pasipo kupata jibu hata moja.

Kwanini Baba amenipiga kofi kisha sikusikia maumivu yeyote,,,,"kwanini yule Mganga amenikimbia Mimi

Huku ndugu nao wakianza kunihofia, maana wakambeba Baba

na kuingia nae ndani kisha wakafunga milango. Nisiweze kuingia ndani, nilibisha hodi sana huku nikiita na kuwaomba wanifungulie,

“Shangazi tafadhali njoo unifungulie mlango please nawaomba jamani kwanini mnanifanyia kitendo kama hiki jamani",,,,,,usiku wote huu nitalala wapi mie!!!,,,,Dada Fatuma

Kwanini nawewe unanitendea hivi kumbuka sisi ni damu moja njoo unifungulie usiniache hapa nnje peke yangu",,,,Baba mdogo unaniachaje mwanao!!!,,,,

Niliongea huku nikilia ajabu hakuna hata mmoja aliyekuja kufungua mlango basi nikaenda kibarazani kujilaza

Nikaomba duwa Allah (s.w.t) anilinde usiku ule

Nikiwa najilaza ghafla akaja

Nusraty huku akiwa anatabasamu na kuniita

“whao Mume wangu mtarajiwa huyoo vipi mbona mpaka saa hizi hujaenda ndani kulala?"

Nilimkata jicho la gadhabu nikamtusi kwa kumsonya

Huku nikimwambia kitu kimoja

“Nyoo***mshenzi mkubwa wewe nani Mumeo hivi unadhani Mimi naweza kuowa zombie?,,,,,,arafu vitu vingine sio vya kuuliza wakati unajuwa kila kitu kwanini nipo nnje kwa wakati huu, kwa taarifa yako nilikuwa nakungojea wewe nikuuwe,,,,,"

Akaniambia

“Hafidhi tambua kitu kimoja tu binafsi nakupenda sana tena sana tu siwezi kukuacha ukiteseka kwa jambo.lolote lile!"

“Nyamaza Mwanamke usiekuwa na haya kabisa ungekuwa unanipenda ungemuuwa Mama yangu mpendwa hivi unaijuwa thamani ya Mama wewe?",,,,,,,

Akaniangalia kama dakika mbili hivi kwa sauti ya upole akatamka

“Kwanza nisamehe Mume wangu maana inaonekana umekasirika vibaya mno nimefanya yote haya kuhitaji wewe uniowe Mama yako sijamuuwa nipo nae ukikubali kufunga ndoa nami

Nitamrudisha Mama yako!"

Nikawa kama siamini hivi, maana kwa macho yangu Mama tulimzika tena nilikuwa mmoja kati ya watu wanne tulioingia kaburini kuupokea mwili wa Mama. Iweje huyu aseme eti

Mama bado yupo hai, nikamuuliza

“je nitakuamini vipi kama Mama yangu bado ni Mzima?"

Akageuza shingo yake na kuita

“Mama mkwe"….mama mkwe!!!

Sauti ya Mama ikasikika akiitika

Abee mkwe wangu!"

“Embu njoo Mara moja,"

Unajuwa nikatoa macho pima kama mjusi vile kabanwa na mlango maana dahaa,,,,,,ni kweli alikuwa ni Mama mbele ya upeo wa macho yangu akasimama kwa heshima na taadhima akaniuliza

“Hafidhi mwanangu kwanini unamtesa mwenzio kila siku akulazimishe wewe tu tena kitu kimoja tu!"

“hapana Mama sio hivyo binafsi siko tayari kufunga ndoa na Nusraty kumbuka yeye sio binaadamu

Kuonyesha kuwa sitaki nitamuowa mdogo wake,"

Nusraty akasema

“Whaoo unamaanisha utamuowa Hasina sio?"

Nikamuitikia

“ndio maana yake",

Akakunja ndita kwa hasira akapotea na Mama ajabu Mama kuna kikaratasi alikiacha pale aliposimama

Basi nikaenda kukiokota

Nikakitupia macho niweze kukisoma nikashindwa,

Kwa mara ya kwanza sikuweza kwenda kuswali swalati subuhi mpaka kunakucha,,,,nikaja kuamshwa na

Baba ndipo nikastuka kutoka usingizini

Nikamsalimia

“Assalamu alaykum warahatullah wabarakatur yaa Abii?,,,,,,

Baba akaitikia kwa sauti ya unyonge sana akaniambia

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)
Simulizi Vampire Nusraty Z73
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni