Notification
Tidak ada notifikasi baru.

VAMPIRE NUSRATY (6)


SEHEMU YA SITA
TULIPOISHIA...
Nikamsalimia

“Assalamu alaykum warahatullah wabarakatur yaa Abii?,,,,,,

Baba akaitikia kwa sauti ya unyonge sana akaniambia

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
“Hafidhi mwanangu kwanza pole sana kisha naomba unisamehe mimi kwa kile nilichokufanyia jana usiku

Hukustahili kulala nnje mwanangu

hakika Mama yako kanijia ndotoni kanisema sana mimi

Baba akaanza kulia

Ghafla tukasikia sauti ikitusalimia

“Assalamu alaykum jamani"

Hakuwa mwingine kumbe ni Shekhe milongo imamu wetu mpya baada Shekhe Yusuf kufariki

Basi tukaitikia akauliza

“vipi mbona kama mnalia kwema lakini?"

Nikamjibu,

“ewe Shekhe wetu nahofia kukwambia hili nikijuwa ya kwamba na wewe nitakupoteza!"

Akastaajabu pia na kuniuliza ni jambo gani hilo kijana wangu huku akikaa pale kwenye kabaraza

Sikuwa na jinsi zaidi ya kuanza kumpa full.story

Baada kumaliza akajifuta jasho yani story mpaka watu wakatokwa na vijasho kisha akasema

“Binafsi sikuwai kufikilia kama waumini kama nyie mnaishi na matatizo makubwa kama haya yani mnakuja msikitini kila kipindi kumuomba Allah kumbe kwenye vichwa vyenu mmebeba gunia lenye misumari

Sasa basi baada swalati dhuhur

Huyo jini nitamwita mbele yenu nitampa onyo aache ujinga

tena nitamwita akiwa na wenzake wawe mashahidi

Asipo sikia atakiona cha mtema kuni

Jini kwa binaadamu kama sisimizi tu utakiwi kuwa na hofu kabisa subirini muone.

Hakika kauli ya Shekhe mirongo kusema ya kwamba ataweza kumwita Nusraty na kumpa onyo kilinifurahisha sana, nikatamani hiyo saa

Saba iweze kufika haraka maana nilikuwa na kimuhemuhe ajabu. Niliweza kuongea mambo mengi sana nikiwa na Baba, hatimae Adhana ikasikika nikasema

“ehee ule muda ndio huu"

Tukatoka kwenda msikitini kuswali

Alhamdulillahi Shekhe milongo alikuwepo…"

Baada kuswali ndipo akasimama na kutoa mawaidha kidogo kwa kusema

“Assalam alaykum warahamatullah wabarakatur",,,,,

Waumini wote tukaitikia

Kisha akaendelea.

“Watukufu Waislamu ningependa kuzungumza japo kwa uchache tu kuhusu Asiri ya viumbe wanaoitwa Majinni kwanza kabisa Jinni ameumbwa kutokana na ndimi ya moto katika karne hizo, hakika ya majinni walikuwa na mji wao basi wakawa wanafanya mambo mabaya tena machafu kabisa ya kumkufuru Allah (s.w.t) ndipo Allah akamtuma Malaika kwenda kuuwangamiza mji ule,

Malaika akaenda na kuuchota ule mji kama wewe unavyoweza kuichota chapati kisha ukaigeuza ndivyo ilivyokuwa

Malaika yule akaupindua mji ule kichwa chini miguu juu,

Mji wote ukaangamia isipokuwa akabaki mtoto mdogo tu wa Kijinni

Basi akachukuliwa mpaka mbinguni huko akalelewa na kuisoma Qur'an

yote,

Baada kupita karne kazaa ndipo Mwenyezi Mungu akawageukia Malaika na kuwaambia anataka kuongeza kiumbe kingine ambaye ni Adam,

Malaika wakapinga na kukataa kwa kusema

“hakika unataka kumuumba mwanaadamu atakuja kufanya mambo mabaya machafu watamwagana damu.

Bora usimuumbe tu sisi tunatosha maana tunakusabihi na kukutukuza.

Allah akasema hakika ya yeye anajuwa yaliyo jificha na kufichikana.

Ndipo akaumbwa Adam na kufundishwa majina ya vitu vyoote kisha

Mwenyezi Mungu akawageukia Malaika na kuwaambia wamtajie majina ya vitu vile,

Malaika wakashindwa kwa kusema

“ewe Mola wetu hakika sisi hatuna elimu yeyote ile isipokuwa ile uliyotufundisha"

Mwenyezi Mungu akamwambia Adam ataje akataja ndipo

Malaika wakaambiwa wamsujudie Adam wote wakakubali isipokuwa yule Jini akakataa kwa kusema

“hakika Mimi ni bora kuliko huyu Adam kwanza Mimi nimeumbwa kwa moto yeye kaumbwa kwa udongo

Kingine yeye ni mdogo kwangu.

Allah (s.w.t)

Akampa laana yule Jini ndipo likapatikana jina la Shaitwani ibirisi

Na kuambiwa hakika milango saba ya moto ni yakwake yeye na vizazi vyake vyote,

Jini yule akaomba kitu kwa kusema

“najuwa nimepewa laana kubwa sana ila naomba usiniuwe wala usinipotezee uwezo wangu mpaka nitimize kiapo changu hiki

Nitawateka watoto wa Adam ili milango saba ya moto niingie nao

Allah (s.w.t) akamkubalia ombi lake kisha akatupwa kutoka kule mbingu ya saba mpaka huku Ardhini

Je unajuwa kilichotokea baada kutupwa huku Ardhini tukutane baada swalat Ishai….."

Hakika mawaidha yalinigusa sana

Basi ikapigwa duwa kisha tukatoka msikitini tukiwa na Shekhe milongo mpaka nyumbani kwake.

Tukala chakula cha mchana kisha tukatia hudhu tena na kuswali rakaa mbili hivi,

Shekhe akachukuwa kichanja akaweka moto akawasha Udi kisha akasema

“jamani ndugu zanguni hili jambo tunaro taka kulifanya hapa sio jambo dogo kabisa kwanza msiwe na uwoga wa aina yeyote ile pindi watakapo kuja hapa"

Tukaitikia kwa pamoja

“sawa Shekhe"

Akauliza,

“ehee huyo binti anaitwa nani yani jina lake kamili?"

Nikamtaja japokuwa la babu yake silifahamu,

“Anaitwa Nusraty Nassoro"

Shekhe akasema

“sawa Hafidhi embu chukuwa ubani kisha taja ilo jina kimoyomoyo Mara tatu!"

Nikafanya kama Shekhe alivyo niagiza kisomo kikaanza

Hakika kilikuwa kisomo kweli

Alisoma Surat Mulk tena harakaharaka akaongea maneno flani hivi kwa kiarabu kisha akaita

“Binti makata,,,binti Nusraty Nassoro,,,,binti Kidawa Maimuna

Nawaita haraka sana mje hapa,,,,

Moshi ukaanza kufuka ndani ya chumba kile kupitia pembe ya Chumba viumbe vya ajabu vikaingia huku wakiwa wameinamisha sura zao chini kwa heshima na taadhima wakapanga mistari

Mpaka hapo nilihisi haja ndogo na kubwa vikitaka kunitoka kwa pamoja

Nusraty akainua Uso wake akanitizama kwa gadhabu sana.

Mpaka nikaona Aibu

Shekhe kwa ujasiri mkubwa kabisa akasema

“kwanza kabisa samahanini kwa kuwaita hapa najuwa mnamajukumu kibao tu ya kufanya,

Nilichowaitia hapa ni kuweza kuwapa mashitaka kuhusu Binti yenu kumsumbua kijana wangu nikaona si vyema kujichukulia hatua mikononi mwangu. Pasipo kuonana na nyinyi wakubwa zake.

Kwanza kabisa naomba amuachie Mama wa huyu kijana yani Mke wa huyu Baba kingine aache kumfatilia huyu kijana, kuanzia muda huu,

Asipofanya hivyo

Tusije tukatafutana, wote kwa pamoja wakatikisa vichwa ishara ya kwamba wamekubaliana na

Shekhe milongo kisha wakapotea

Baada vile viumbe kupotea kimiujiza mule ndani,

Shekhe milongo akaongea maneno flani kisha akasema

“binafsi naweza kusema kazi imekwisha japokuwa siwezi kusema yule Binti ametii hii kauli moja kwa moja au laa,

Cha umuhimu ni kumuomba Allah hakika yeye ndio mjuzi wa kila kitu,

Baada kusema vile tukasoma kisomo cha kuagana

Kisha tukarudi nyumbani,

Fatuma alifurahi sana kutuona nikajuwa furaha yake labda kamuona Mama karudi nikaingia ndani kwa shahuku kubwa sana,

Nikaambulia patupu hakuna cha Mama wala nini, kama kawaida saa mbili Usiku ikatimu nikaenda msikitini kuswali

Nikiwa nimepiga hatua kazaa kuupita ule mbuyu nikasikia kicheko kikitokea nyuma yangu sikuogopa wala nini nikageuka na kumuona

Nusraty akiwa na Shekhe milongo nilistuka sana na kutamani kukimbia,

Kwa sauti ya unyonge yenye kukata tamaa

Shekhe milongo akaongea

“Tafadhali kijana nisaidie please usinikimbie ukaniacha hapa peke yangu nisaidie!"

Nikabaki kumtizama tu nikaitaji kwenda kumshika ghafla nikajikuta napigwa na kitu kizito sana tumboni mpaka nikarushwa na kwenda kutua chini nilihisi kama mguu wangu umeteguka hivi, nikawa naugulia maumivu pale chini nikatapika nyongo

Dahaa

Nusraty kwa mwendo wa speed akanifata pale nilipolala kisha akaninyanyua kwa kunikaba yani akanining'iniza utasema kuku kishingo vile

Nusraty macho yake yakabadirika na kufumbua mdomo wake Minjino yake miwili ikachomoza

Na kuwa kama vampire. Nikahisi haja ndogo ikinidondoka,

Akiwa kanikazia macho.

Hafidhi sikuwa na jinsi zaidi ya kufumba macho tu kama kufa wacha nife wamekufa Mitume sembuse mie kapuku tu,

Ajabu akaniachia na kujirudi katika umbile lake la kuwa binti mrembo

Akanishika na kusema

“Hafidhi pole sana mpenzi hivi kwanini unataka haya yote yatokee kipenzi changu, tambua sitaki uumie sitaki upotee please nielewe Hafidhi nakupenda,

Akanishika kichwani kisha akapotea huku yale maumivu yakiniisha

Nikatoka mbio mpaka msikitini nikakuta watu washaswali wanamalizia sunna tu,

Nikatawadha

Na kuingia kuswali ajabu

Shekhe milongo alikuwepo msikitini nikabaki kushangaa pasipo kufunga Sala,

Sijui alifahamu au vipi maana akasimama na kuja pale nilipo simama akasema kwa sauti ya kuninong'oneza

“kijana usiogope fanya ibada kwanza!"

Kisha akarudi sehemu ile ya aliyokaa na kuendelea kusoma Qur'an

Siwezi kujuwa wala kufahamu kama swala yangu iliweza kupokelewa au vipi.

Maana niliswali pasipo kujuwa idadi za rakaa, baada kuona nimemaliza nikatoka nnje

Binafsi nilikuwa na uwoga sana,

Shakhe milongo akanikimbilia huku akiniita

“Hafidhi kijana wangu embu njoo usikimbie Shekhe wangu,,,," unaogopa nini kwani?"

Nikasimama na kugeuka, kwakuwa alikuwa tayari ameshanifikia

Akanishika mkono

Na kuniuliza,

“embu niambie nini tatizo Shekhe wangu?

Sikuwa na jinsi zaidi ya kumwambia ukweli wote,

Shekhe milongo mpaka ikapelekea Mimi kuchelewa kuswali!"

Akatamka shahada kwa kusema

“Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwa hakika Muhammad ni mjumbe wake!"

Kijana huyo jini katangaza vita embu twende nyumbani kwangu haraka sana

Maana tukisema tulale usiku wa leo utakuwa mgumu sana kwetu"

Tukaongozana kufika tu pale

Mbuyuni nikaona wenge baada

Nusraty kututokea akiwa na wenzake nikataka kukimbia Shekhe milongo akanishika mkono

huku akisema

“tulia kijana unaogopa kuku tu hawa!"

Nusraty akacheka kicheko cha kifedhur

huku akisema

“Shekhe au panya leo ndio mwisho wenu akapiga kombora kumuelekezea Shekhe ajabu

Shekhe akatoa kitabu na kufanya kama ngao yake vile kombora likamrudia

Nusraty mwenyewe

Akarushwa hewani huku wenzake wakitoka mbio nae akapotea,

Nilifurahi balaa huku nikikenua meno 32 yote nnje kumbe Shekhe milongo balaa hakika

Nusraty leo kajamba

Ha!ha!ha!ha!

Shekhe milongo nae akacheka na kuniuliza

“ha!ha!ha!….vipi kijana mbona wacheka sana mpaka umeniambukiza namie nicheke?"

Nikamjibu huku nikiunyanyua mkono wake juu yani kama bondia au mcheza mieleka kashinda

“hakika Shekhe milongo wewe ni mshindi,

“Hapana Shekhe wangu Mimi sio mshindi kama vita ndio vimeanza cha umuhimu tumtegemee Allah (s.w.t)

Hakika yeye ndie muweza wa kila kitu!"

Nikamuuliza, “hivi Shekhe kwanini namimi unaniita Shekhe haliyakuwa bado sijafikia hata cheo cha kuwa Hustadhi?"

Akatabasamu na kunijibu,"

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)
Simulizi Vampire Nusraty Z73
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni