VAMPIRE NUSRATY (7)
Zephiline F Ezekiel
---
Mtunzi: Hafidh J. Ikram
SEHEMU YA SABA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Nikamuuliza, “hivi Shekhe kwanini namimi unaniita Shekhe haliyakuwa bado sijafikia hata cheo cha kuwa Hustadhi?"
Akatabasamu na kunijibu,"
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
“Napenda nikuite Shekhe kutokana na ucha Mungu wako,
Kwani natarajia Allah akijaalia utakuja kuwa Shekhe mkubwa sana kwahiyo mpaka sasa wewe ni Shekhe!"
Nikamuuliza swali lingine
“hivi Shekhe mbona Shekhe Yusuf alishindwa kupambana na Nusraty?"
Akaniambia,
“Kuhusu swala la Shekhe Yusuf tuseme alijisahau hakika Shetani ana vitimbi vya kila aina,
Kwahiyo yule Jinni akaona njia pekee ya kumteka Shekhe Yusuf ni kupitia mkewe
Akaenda kumuingia mwilini
Usiku Shekhe akafanya tendo la ndoa na mkewe akajisahau au kusahaulishwa kwenda kuoga kwa ajili ya kuondoa Janaba,
Akalala ndipo yule Jinni akatumia nafasi hiyo kumdhuru.
Kumbuka unapokuwa huna
Hudhu Qur'an inakuwa mbali nawe
unakuwa hauna ulinzi wowote,
Cha umuhimu tudumishe kuwa na hudhu kila sekunde kila dakika na masaa yaendayo kwa
Allah (s.w.t)!"
Baada kuniambia vile tukawa tayari tushafika nyumbani kwake
Akasema kazi ianze,"
Baada Shekhe milongo kusema
Kazi ianze tukatia hudhu, baada kusali kama rakaa mbili hivi
Kisha Shekhe milongo akaniambia hivi
“Hafidhi kijana wangu.
Au Shekhe wangu tambua kitu kimoja huyu Shetani ni kiumbe mjanja sana kwanza kabisa amejijengea kwenye akili yake ya kwamba binaadamu ni viumbe waoga mno,
Yani utakuta mtu anapandisha mashetani na kuongea sijui nataka mtindi au Pete sijui furani
Mchawi tambua huo ni uwongo yani anachotaka ni kuwapima imani
Embu nikuulize swali kijana kwa mfano Mkeo akapandisha Mashetani na kusema Mama yako ni Mchawi utaamini au?"
Nikatikisa kichwa kukataa yani siwezi kuamini kamwe,"
“vizuri sana kijana siku zote dawa ya moto ni?,,,,,,
Nikadakia kwa kujibu
“ni moto"
Akasema
“Ehee ewaa kumbe kijana unaakili sana mi nilijuwa utasema maji wakati maji yatachemka tu, sasa ukimuona mtu anapandisha Mashetani cha kufanya msomee kisomo cha Ruqiya hakika huyo Shetani au Mashetani yatakimbia kabisa kwenye kichwa cha huyo mtu kamwe hawatoweza kuja tena
Maana utakuta mtu anapandisha na kuanza kutaja vitu vya gharama sijui Pete cheni za dhahabu mtu kama huyo mchape makofi tena ya nguvu
Huwenda Shetani wake anataka kuwa Sharobaro,,,,,,"
Nikajikuta nacheka mbavu sina,
“Ha!ha!ha!ha!
tehe,,,tehe!
Shekhe akaniambia huku akinishika begani
“ohoo kijana basi usicheke sana matokeo yake ukajamba hapa!"
Hakika Shekhe milongo alikuwa na maneno yenye utani mwingi sana nikamuuliza",
“kwani Shekhe Majinni wapo ambao ni Masharobaro?"
Akatabasamu kwa kunijibu
“ndio wapo tena wengi tu tambua kitu kimoja Jinni siku zote anapenda kufanya kile ambacho binaadamu hupenda kufanya
tukianzia katika Kula kulala kufanya mapenzi
Yani hadi kwenye hiyo mitandao ya kijamii majinni wapo!"
Nikabaki kusema
“Duhuu kumbe Majinni noma ehee
Yani kila kona wapo"……
“ndio kila kona wapo tena Majinni ni wengi kuliko binaadamu
Maana wengine tunaishi nao kwenye Majumba yetu wengine wapo Baharini wengine kwenye miti kwa mfano ukitaka kumkamata jinni subiri nitakufundisha Yani jinni anakatika kama kifaranga cha kuku,"
Nikawa na shahuku ya kutaka kujuwa jinsi ya Kumkamata Jinni sema Shekhe akaniambia nisiwe na haraka
Atanifundisha tu
Basi kisomo kikaanza tulisoma mpakaa saa nane Usiku ndipo tukapumzika na kupitiwa na Usingizi
Ghafla nikahisi maumivi makali sana mwilini mwangu
Baada kuchapwa bakora sijui ina miba au vipi nikastuka,,,,"
Mama yangu weee sikuweza kufahamu nipo wapi yani sehemu niliyokuwepo inatisha vibaya mno
Kibaya zaidi nilikuwa nimelalia mafuvu ya watu nikajikuta natoka mbio yani nilikimbia huku nikiita
“Shekhe milongo nisaidie msaada tafadhali yani kukimbia kote kule ajabu nikajikuta nipo pale pale.
Dahaa mbona majanga, nikazidi kutandikwa bakora tu mpaka nikahisi mwili wangu kuchanika chanika vibaya sana.
Nikiwa sijui huku nimefikaje kwani
Ghafla ile fimbo ikadakwa kile kiumbe kilichokuwa hakina nyama hata moja mwilini yani mifupa mitupu
Kikageuka kuangalia nani kaidaka ile fimbo. Akastukia anapigwa zinga la kofi akarushwa hewani
kumbe alikuwa
Nusraty basi akanifata pale nilipokuwa nimejikunyata nikiugulia maumivu akaniambia
“Hafidhi nisamehe Mimi sikutaka wakuadhibu hivi niliwatuma tu waje kukuchukuwa na kukuleta huku!"
Unajuwa kitu ukikizoea bwana huwezi kuwa na hofu kubwa ndio mimi kwa Nusraty sikuwa namuhofia sana
Kingine ukishajuwa unapendwa
lazima ulinge basi nikamkazia macho na kumuuliza
“kwani Shekhe milongo yupo wapi?"
Akanionyeshea kiganja chake cha mkono nikaona Eti nyumbani kuna msiba tena aliyekufa ni mimi.
Nikapiga kelele kwa kusema
“Hapanaa,,,,,,,"
Nilipiga kelele kama mwehu vile sikutegemea kuona eti nimekufa dahaa
Nusraty akaniambia
“kuanzia leo wewe ni Mume wangu Mimi huwezi kurudi tena duniani utabaki huku katika dunia yetu mpaka siku utakayo kufa",
Nikamwambia
“hata kama utanifanyia kitu gani siwezi kuwa Mumeo kamwe bora nife tu,
Nikaokota kimfupa kimoja wapo kilicho chongoka na kutaka kujiuwa
Huku nikisema
“ni bora kufa tu kuliko kuwa huku
Nusraty sikupendi sikutaki mbona husikii,"
Nae akaniambia
“tafadhali mpenzi wangu usijiuwe ukijiuwa unafikilia nitaishi na nani Mimi niambie kitu gani unataka nikufanyie ili usijiuwe?,,,,,
Nikamwambia
“Nirudishe nyumbani,,,
Ghafla nikasikia naitwa kwa mbaali na
Shekhe Milongo
“Hafidhi!!!,,,,,hafidhi,,,amka Shekhe wangu muda wa kwenda kuswali nikastuka kumbe khaa nipo kwenye kile chumba cha Shekhe Milongo,
Baada Shekhe milongo kuniamsha kwanza nikabaki kushangaa huku nikigeuza shingo yangu huku na kule kukitizama chumba kile.
Kisha nikamtizama Shekhe usoni
Na kumuuliza swali ambaro jibu lake ninalo Mimi mwenyewe,
“kwani niko wapi hapa?"
Shekhe milongo hakujibu kitu zaidi ya kunisaidia kunyanyuka tukaongozana kwenda msikitini,
Njia nzima nikawa naona nyota nyota tu miguu ilikuwa mizito kutembea yani nilikuwa kama vile nimebebeshwa mifuko ya Cement kama sita hivi kichwani arafu niambiwe kimbia nayo.
Shekhe alikuwa kimya tu
Mpaka tukafika msikitini tukatia Hudhu
akaniambia niadhini kiukweli nikamwambia hapana sitoweza maana kichwa changu hakipo sawa kabisa,
Baada kuswali
Shekhe akasimama na kusema kitu kimoja tu yani ifikapo saa tatu Asubuhi Mashekhe wote mnaitajika kufika hapa msikitini kutakuwa na kisomo kizito sana, hakuna aliyeuliza kila mmoja akatawanyika kimpango wake.
Nikarudi nyumbani,
Dada akaniuliza
“Kaka Hafidhi usiku wa jana ulikuwa wapi?",,,,maana kuna mgeni wako alikuja jana usiku akakusubiri wee akijuwa labda utakuwa msikitini"
Nikamuuliza
“huyo mgeni jinsia gani na anaitwa nani?"
“ni Mwanamke kasema anaitwa Nusraty!"
Nikajishika kichwa huku nikisema
“Mungu wangu wee!!!
unasema ni Nusraty ndio kaja hapa jana usiku?",,,,,
“ndio tena kaniachia ujumbe nikupe"
Dada akingia ndani na kutoka na bahasha kisha akanikabizi kwa kusema
“ujumbe wenyewe huu hapa!"
Kwanza nikapokea huku mikono ikinitetemeka yani kama vile unanipa kaa la moto nikijuwa kabisa nitaungua.
Nikaipokea Fatuma akaondoka nikaenda kukaa kibarazani nikaifungua kiumakini sana.
Kisha nikakutana na barua hii yenye maajabu kwanza haikuandikwa kitu chochote kile, yani karatasi nyeupee
Nikawa naigeuza huku na kule kisha nikasema
Nusraty ghafla akatokea kwenye ile karatasi mmh!
Nikataka kuitupa chini ajabu haikutoka mikononi mwangu,
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni