KABURI LA KAZULA (8)

Zephiline F Ezekiel
0

SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
giza hilo kwisha kutanda, ile nyimbo ya kiarabu ilikata... wakati huo huo ikasikaka sauti nzito. Sauti hiyo ikisema ikianza kwa kicheko" Hauna haja ya kuogopa,usihofu jisikie uko nyumbani"

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
Ilisema hiyo sauti. Lakini Mele akaishia kuguna tu...na mwishowe akajitahidi kuhoji japo kwa wasiwasi "kwani wewe nani? Na uko wapi? Alihoji Mele.. swali ambalo lilimfanya yule mtu kucheka kwa mala nyingine..safari hiyo kicheko chake kiliambatana na upepo mkali na ngurumo nzito zilizo mfanya Mele kuogopa sana. "Unataka kuniona? Yule alihoji. "Ndio" Mele nae akajibu hivyo. Ambapo kimya kidogo kilitawala. Baada kimya hicho kutoweka,ghafla Mele aliona mwanga hafifu..na katika mwanga ule Mele alimwona mtu akitembea kuja mahali alipokuwa amesimama.

Mele alizidi kuogopa kwa maana huyo mtu hakuwa wa kawaida. "usiogope kwani huko utakutana na mwenyeji wako ambae nae atakuwa mtu mwenye jicho moja usoni nywere zake zitakuwa vichwa vya nyoka huku miguu yake nayo ni kama kwato za ng'ombe. ... Kwahiyo Wala usimwogope Binti maana huyo ndio atakupa mbinu zote za kumpata Memeo huko kuzimu" Mele alikumbuka maneno hayo aliyo ambiwa na mzee Baluguza....Baada Mele kukumbuka hatimae akashusha pumzi kwa kasi huku akimeza mabunda ya mate kila sekunde yote ikiwa dalili ya woga. Yule mtu alizipiga hatua za polepole kumfuata Mele.. Na baada kumfikia, akasema "Fumba macho"

Mele alifumba macho,ghafla akasikia joto kali..akataka kufumbua macho lakini nafsi ikamsuta akiamini kuwa huwenda akapata madhala. Hivyo aliendelea kuyafumba macho yake mpaka pale alipo ambiwa fumbua. "Fumbua" Mele alifumbua macho,hakika hakuamini baada kuona yupo katikati ukumbi mkubwa,ukumbi ambao ulikuwa umepambwa na maua ya kila aina huku marashi mbali mbali nayo yakiupendezesha ule ukumbi. Mele hakuwa peke yake...aliyainua macho yake kutazama kila upande katika ule ukumbi,akaona kila kiti kina mtu.

Na watu hao hawakuwa wa kawaida kama ilivyo binadamu...kwani kuna baadhi walikuwa hawana hata Nyama katika miili yao zaidi ya mifupa mitupu huku wengine wakionekana nusu mtu nusu binadamu..si wote walikuwa hivyo,la khasha wengine walikuwa binadam wa kawaida.. Na siku hiyo kumbe ilikuwa siku ya Sherehe kuzimu. "Twende huku" Mele wakati akiendelea kustaajabu,aliambiwa hivyo na yule mwenyeji wake aliemfikisha kuzimu kwa kupotia njia ya ziwa Victoria. Mele aliambatana na yule mtu,moja kwa moja wakaingia mpaka kwenye chumba ambacho kilikuwa kikinukia harufu ya damu huku sauti za nafsi za watu zikisikika kila kona.

Baada Mele kuingia katika kile chumba kilichokuwa kikinukia harufu ya damu..huku zikisika sauti za nafsi za watu waliokufa.. sauti ambazo zilikuwa zikilia wakati wote. Hatimae yule mtu ambae alikuwa nae wakati wote, alimwambia Mele "Tazama mbele " Mele akatazama akaona mlango mkubwa ulijengwa kwa dhahabu...wakati Mele akishangaa,ghafla ule mlango ukajifungua mbele wakaonekana watu wakila nyama za binadam..kiukweli alistaajabu sana,mwemgewe akajiuliza je, nitafanikiwa kweli? Akiwa bado hajapata jawabu juu ya kile alicho jiuliza,punde akadikia tena sauti ikisema "ingia kwa hicho chumba"

Mele aliambiwa aingie mle chumbani..hivyo Mele hakusita,hara sana akazivuta hatu akaingia kwenye kile chumba...kisha lango lile la dhahabu liliokuwa limepambwa kwa nembo mbali mbali za mashetani likajifunga."keti kwenye kiti " Sauti iliyosikika kwa uzito,ilimwambia hivyo Mele ikiwa Mele akiendelea kuwashangaa wale watu waliokuwa wakishambulia nyama za binadamu. Hatimae Mele alikaa,na punde si punde akaletewa bilauli lililojaa nyama za binadamu,ambapo Mele alipozigeuza geuza akakuta ni Sehem ya siri za mwanaume.

Kwa hakika Mele alijikuta akitaharuki ghafla kinywa chake kikajaa mate,kichefu chefu nacho hakikuwa mbali. Mele akajihisi kutapika,lakini kabla hajatapika Mele akakumbuka " Kitu kingine ambacho nakuasa, tafadhali usiogope wala usikatae kula chakula au kinywaji chochote utakacho letewa..maana endapo ukikataaa,basi kurudi duniani kwakweli itakuwea vigumu...hivyo chunga sana usicheze vibaya katika huu mchezo wa kufuata hirizi aliyo ivaa mumeo" kwisha kukumbuka hayo,ile hali ya kichefu chefu ilimpotea Mele ambapo alianza kula zile nyama bila kuogopa. Na hayo yote Mele aliyafanya kwa kutaka kumrejesha Kazula duniani.

Mele alikula zile nyama kwa tabu sana ambazo zilikuwa ni makorodani na ume. Kabla hajamaliza akaletewa kikombe kikubwa kilicho sheheni damu ambayo ilikuwa bado ya moto kwani ilionekana kutoa mfuke. Hakika Mele alishtuka akajisemea "Kweli mtaka cha uvunguni sharti ainame,uko wapi Kazula nafanya yote haya kwa ajili yako" Alijisemea hivyo Mele huku akitafuna Makorodani,ikiwa mbele yake bado kuna kikombe cha damu kikimngojea.

Na wakati hayo yalipokuwa yakimkuta Mele kuzimu,upande wa pili nako duniani. Alionekana Marongo akihaha kutafuta namba ya Simu ya Mele ili apate kumpigia baada kuona taklibani siku tatu hamuoni nyumbani kwake kwa maana safari ya Mele kwenda kuzimu,Marongo hakuijuwa. "Mmh huyu nwanamke siku hizi kabadilika saana,yaani haiwezekani siku tatu zote asirudi nyumbani " Alijisemea Marongo mume wake Mele huku akiweka Simu sikioni kwake,na punde si punde simu ya Mele ikaita bila kupokelewa.

"Unaona? wanawake wengine bwana bora ukaishi na sokwe. Inakuaje unaondoka bila kuaga harafu hata simu hupokei! Aah " kwa hasira zisizo kuwa na mfano Marongo aliyasema hayo maneno huku akipiga ukuta kwa kutumia mkono wake wa Kulia... lakini mwishowe akaamua kutoenda kazini siku hiyo,moja kwa moja akaelekea kwa rafiki yake Mele ambae alifahamika kwa jina la Somela. Marongo akafika nyumbani kwa Samela kwa lengo la kutaka kujuwa mahali alipo Mele,hivyo kwa kuwa Somela ndio rafiki yake wa karibu Mele..Marongo akaona Somela huwenda akajuwa Mele alipo kwenda.

"Habali yako Somela" Marongo akionekana kuwa na hofu alimsalimu Somela ambae nae alionekana kuwa bize kupika chapati,maana Somela kazi yake ilikuwa ni hiyo kuuza chapati kwa wapita njia. "Salama tu shemeji, vipi mbona wanaonekana hauko sawa?.." Somela alijibu hivyo huku akikomea na swali lililomfanya Marongo kushasha pumzi na kisha kusema. "Somela,nimekufuata hapa ili uniambie wapi alipo mke wangu.. siku tatu sasa haonekani nyumbani na hata nikimpigia simu hapokei "

"Nani Mele?..kiukweli shem mimi sijui chochote kuhusu Mele,nakumbuka mala ya mwisho kuonana nae ilikuwa juma tano..na siku hiyo aliniambia kwamba ulimpiga sana kwa kigezo eti hazai..kwahiyo tangu siku hiyo sijamtia tena machoni"

"Oooh Mele wangu weee...Ni kweli tangu nijuwe kuwa Mele hazai,ghafla Upendo wangu wa dhati ukapungua,nikawa simpendi hata kidogo...lakini baada kufikilia sana nikaona sio vizuri kwani hata yeye huo ugumba hakuupenda" Alisema Marongo kwa masikitiko makubwa huku machozi yakimtoka.

"Sawa shem,lakini ngoja nikushauli kitu" Somela alisema akimwambia Marongo.

"Ndio ndio...nishauli shemeji yangu"

"Kuna mganga mmoja hivi,yupo vizuri nadhani anaweza kukusaidia tukajua mahali alipo mkewe, hapa mjini huwezi juwa. Kama kachukuliwa msukule,utajuaje sasa?.." Somela alisema hivyo kwa kukazia hilo jambo. "Ok nitashukuru sana...kwahiyo lini sasa nije ili twende?..."

"Tungeenda hata leo, lakini nina oda ya chapati hamsini za wakandarasi..kwahiyo kesho jioni asubuhi we njoo"

"Sawa..Ahsante " Aliaga Marongo kisha akaondoka zake akimwacha Somela akiendelea kazi yake "mmmh wanaume mnashida sana,yaani unategemea mwanamke ukimpiga kama punda atavumilia tu kila siku?..aawapi hatakama ni mimi siwezi" Alibaki akijisemea hayo Somela huku akigeuza geuza chapati iliyokuwa kwenye flampeni.

Wakati hayo yakijili duniani,kuzimu sasa kule alipo Mele..alijikuta akiwa katika wakati mgumu baada kumaliza chakula na damu lakini punde akaanza kutapika..Harufu ya damu ilimshinda...akajikuta akitapika sana huku akiwa amegusa tumbo lake kwa mikono miwili..ambapo watu wale wa kawaida na wakutisha waliokuwemo ndani ya kile chumba..ghafla walimgeukia Mele huku wakimtazama kwa hasira kali.

Mele baada kuhisi kichefu chefu kwa muda mrefu,hatimae alianza kutapika..kitendo ambacho kiliweza kuwashtua wale watu wengine waliokuwa wakiendelea kula zile nyama za binadam. Ghafla wote wakamgeukia Mele na kisha kumtazama kwa macho ya hasira wakati huo mapigo ya moyo ya Mele yalikuwa yakimwenda mbio akiamini kuwa tayali kavunja moja ya mashrati hivyo uwezekano wa yeye kurudi duniani ni ndoto.

"Mmmh nitafanya nini mimi? Mele alijilaum mwenye huku machozi yakimtililika mashavuni mwake ikiwa muda huo huo akatokea binadam mmoja ambae miguu yake ilikuwa kama kwato za mbuzi,huku kichwa chake kionekana kuwa na mapembe ya mnyama Swala. Mtu huyo alionekana mbele ya Mele,Mele aliogopa baada kumwona kiumbe huyo wa kutisha,hima alirudi nyuma. Na wakati akizipiga hatua za kurudi nyuma,mala ghafla yule kiumbe aliyetua mbele ya Mele,aliwaamlisha wale watu waliokuwa wakila nyama za binadam kuwa wamshambulie Mele.

Kweli punde si punde wale watu walioonekana kuwa na meno marefu,walimfuata Mele kwa kasi,lakini kabla hawajamfikia,ghafla akatokea yule kiumbe aliempokea Mele kule ziwa Victoria. Kiumbe huyo aliwadhibiti wale watu waliotaka kumjeruhi Mele hali iliyopelekea yule kiumbe alietoa amri kukasirika,na hivyo akawataka wale watu watulie ili wao waanze kupigana. Amri ilitoka kwa yule mwenyeji wake Mele,akasema "Ukiniangusha tu chini,hakika nakutunuku huyu mtu mmfanye mtavyo " Alisema kiumbe huyo huku sauti yake ikisikika kwa uzito mkali. Lakini yule kiumbe mwingine nae baada kusikia maneno hayo,alicheka saana kwa dharau huku miale ya mwanga mkali kama radi imulikavyo ..ikamulika kila kona, na punde si punde akanyoosha mkono juu ukatokea upanga makali wa dhahabu...upanga ulionekana kumelemeta kwa makali.

Hivyo kiumbe yule ambae ni mwenyeji wake Mele kuzimu, baada kuona adui yake kashika panga kali la dhahabu,nae hakufanya kosa akachukuwa upanga kama uleule na punde si punde mapigano yalianza...viumbe hao wakutisha walipigana,Mele aliogopa sana kwani hao viumbe walipokuwa wakipigana ngurumo kali zilisikika,kitendo kilicho mfanya Mele kuogopa. Vita juu vita..hatimae kengere ilisikika kengere ya kuashiria kwamba muda wa chakula umekwisha amabapo viumbe hao wawili walijikuta wote wako sawa hakana bingwa. Na hiyo ikawa bahati kwa Mele,kwani baada kulia kingere.. yule mtetezi wake ambae ndio mwenyeji wake..aliweza kumwambia Mele afumbe macho na baada ya dakika kadhaa akamwambia afumbue..

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

  Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)