
Mtunzi: Davis Nyandindi
SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Wakati inapigwa ile ng'oma mzee sube pamoja na mke wake walibahatka kuisikia ile sauti na moja kwa moja wakahisi kuwa labda Yule nyoka wao mwenye jina la YOKA alikuwa kafanya kazi yake ambayo alikuwa ametumwa, mzee sube akamuomba mke wake abaki pale nyumbani na yeye aende huko kwa mfalme.
KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA NAYO...
MZEE SUBE : Mke wangu hiyo ng'oma inayopigwa huko nahisi kunatatizo limetokea kwa mfalme alafu kichwani mwangu naona hilo tatizo kama kalisababsha Yoka.
BIBI SUBE: Yani kama ulikuwa kichwani mwangu hivi maana hata mimi ninmehisi hivyo hivyo
MZEE SUBE: Sasa tufanye kitu kmoja mimi ngoja niende alafu wewe baki hapa nyumbani chochote kitakachotokea kule nitakuja kukuambia.
BIBI SUBE: Sawa safari njema ila kuwa makini.
MZEE SUBE: Wala usijari mke wangu.
Mzee sube akatoka nje na kuanza safari ya kwenda nyumbani kwa mfalme, alijtahi kutembea haraka sana na hatimae akafika na kuwakuta watu wengine wameshafika pale uwanja ndipo mfalme akasimama akawasalimia wanakijiji na kuanza kuongea juu ya jambo ambalo limfanya awaite pale.
MFALME: Jamani wananchi wa hiki kijiji cha mbaka nimewaita hapa kwa ajili ya jambo moja na ninahitaji msaada wenu juu ya jambo hili.
Mfalme baada ya kusema vile ndipo wanakijiji wakaanza kutazamana huku wengine wakiwa wananong'ona wakiulizana Ila kwa upande wa mzee sube moyo wake ulikuwa unaenda mbio na hakutaka kuongea na mtu yoyote bali alikuwa makini kusikiliza anachokisema mfalme, wanakijiji waliponyamaza mfalme akaendelea kuongea.
MFALME: Jambo lenyewe ni hili , hapa kuna kijana ameletwa ameumwa na nyoka na alipewa ile dawa ambayo huwa tunaitumiaga kuuwa sumu ya nyoka ila bado hali yake mbaya .Kwahiyo mimi sipo tayari kumpoteza huyu kijina kama kuna mtu anadawa ya kumsaidia naomba ajitokeze ila iwe tofauti na ile dawa ya kijiji iliyotengenezwa na mababu zetu.
Mzee sube aliposikia vile moyo wake ulilpuka kutokana na furaha ambayo alikuwa nayo, haraka bila uwoga akapita mbele na kumueleza mfalme kuwa yeye anaweza kumsaidia yule kijana, Mfalme alifurahi sana kusikia vile mda huo wananchi walikuwa wakinong’onezana kutoka na mzee sube kujitokeza.
MZEE SUBE: Mtukufu mfalme mimi ninaweza kumsaidia huyo kijana.
MFALME: Kweli mzee?
MZEE SUBE: kweli mtukufu mfalme.
MFALME: Aya mzee anza kazi na endapo utafanikiwa kumsaidia huyu kijana nitakupatia zawadi.
MZEE SUBE: Sawa mtukufu mfalme ila naomba uniruhusu nikachukue dawa yangu nyumbani ninakuahidi huyu kijna atakuwa mzima kabisa.
MFALME: Sawa fanya haraka kabla hatujampoteza huyu kijana.
Baada kuruhusiwa akakimbia haraka na akafanikiwa kufika nyumbani kwake na kumkuta mke wake akiwa amekaa kwenye mkeka ajui hili wala lile linaloendelea kwenye mkutano kule kwa mfalme. Alipofika alikuwa anahema haraka haraka kutokana na kukimbia kwa speed { haraka } Baada ya kukaa sawa ndipo akamsimulia mke wake kwa ufupi kilchotokea kwa mfalme.
Alipofika alikuwa anahema haraka haraka kutokana na kukimbia kwa speed { haraka } Baada ya kukaa sawa ndipo akamsimulia mke wake kwa ufupi kilchotokea kwa mfalme.
MZEE SUBE: Mke wangu tumefanikiwa tena kwa asilimia elfu kumi maana mia ni ndogo.
BIBI SUBE: Kwanini maana umenishtua sana ulivyokuwa unakuja nilihisi unakimbizwa.
MZEE SUBE: Sio nakimbizwa ila hii ni furaha maana mfalme amekubalia nikamtibu mtu ambae kang'atwa na yoka.
BIBI SUBE: Heee! Mume wangu kweli ?
MZEE SUBE: Kweli Hivi hapa unavyoniona nimekuja kuchukua dawa na kuondoka.
BIBI SUBE: Kama ndio hivyo na mimi ninakuja huko huko.
MZEE SUBE: Yani hata kama utataka kuibeba mpaka nyumba uje nayo wewe beba twende, Kwanza ngoja nikachukue dawa ili twende kabla sijachelewa.
Akaingia ndani na kwenda kuichukua ile dawa yake, alipotoka bibi sube na yeye akaenda chumbani akuchelewa akatoka wakaanza safar yao ya kwenda kwa mfalme. Kutokana na mwendo wa haraka waliokuwa wanatembea wakafanikiwa kufika mapema nyumbani kwa mfalme na kuwakuta watu wakiwa wanasubiria. Ndipo mzee sube akamuweka vizur yule mgonjwa huku akisaidiwa na mke wake, akachukua ile dawa yake na kumtia kwenye kidonda na nyingine akamnywesha. Walikaa kwa dakika kadhaa wakisubilia yule kijina apate afadhali ila cha ajabu hali yake ilizidi kuwa mbaya jambo ambalo lilimshangaza sana mzee sube.
Bibi sube alipoona vile akatoa ile dawa yake na kumpatia mume wake ili amnyweshe yule mgonjwa, Sube akachukua ile dawa na kumnywesha zikapita dakika kama mbili yule kijina akazinduka maana alikuwa kama mtu aliezimia. Jambo lile llmshangaza sana mzee sube na kujikuta akimuangalia mke wake kwa jicho la mshangao kumaansha kuna kitu alihitaji kumuuliza lakini alishindwa kutokana na kuwepo kwa watu karibu yao. Wanakijiji pamoja na mfalme walifurahi sana kuona yule kijana amepona, ndipo mfalme akaanza kuongea na wanakijiji huku akiwa anamshukuru sana sube pamoja na mke wake.
MFALME: Wakijiji kwanza nina furaha sana juu ya uponyaji ambao kaupata huyu kijna pia napenda kutoa shukrani zangu nyingi kwa huyu mzee pamoja na mke wake maana jambo ambalo wamelilifanya sio kwamba limemsaidia huyu kijana tu bali na wanambaka wote. Maana huyu kijina anaweza kuwa askari au mfalme na akasaidia hiki kijiji chetu huko mbeleni. Kwahyo jambo alilolinya huyu mzee la kupongezwa sana na kila mtu.
Mfalme aliposema hivyo wanakijiji wakaapiga makofi kwa ajili ya kumpongeza mzee sube, Lakini wakatii wanakijiji wanapiga makofi, Sube alikuwa mbali sana kimawazo kutokana na kile kitendo ambacho amekifanya mke wake. walipoacha kumpongeza, mfalme akamtangaza rasmi mzee sube ndie atakaekuwa tabibu mkuu pale kijijini kutokana na ule msahada ambao alikuwa ameufanya.
MFALME: Sasa baada ya kumpongea kwa maneno na kwa kumpigia makofi, mimi nataka nimpe zawadi nyingine nampa cheo cha kuwa tabibu mkuu hapa kijijini kwetu maana inaonesha anazijua dawa nyingi ambazo zitaweza kutusaida.
Maneno ya mfalme yalimfanya mzee sube afurahi sana maana aliona malengo yake yamekwisha timia. Mfalme alihailisha ule mkutano na kuwaambia watu wakaendele kufanya shughuli za zingine za kuleta maendelea pale kijini kwao, Wanakijiji baada ya kuondoka ndipo akamuita mzee sube na kuanza kuongea nae.
MFALME: Mzee wangu kutokana na cheo ambacho nimekupa unatakiwa ukae karibu na hapa nyumbani kwangu ili wanakijiji wakipatwa na matatizo iwe rahisi kukupata.
Wazo la mfalme na maneno yake yalikuwa ni mazur sana ila kwa upande wa Sube alikuwa wazo zuri hata kidogo maana aliona kama angeamia karibu na mfalme ingekuwa rahisi kumgundua kuwa yeye ndio msababishaji wa yote maana asingekuwa na sehemu ya kumtunza yule nyoka wake.
MZEE SUBE: Ni wazo zuri mtukufu mfalm ila mimi ninaona bora nibaki kule kule maana ni karibu na msituni kwahiyo nitakuwa napata dawa kwa urahisi kuliko nikija kukaa huku itakuwa mbali na msituni.
Sube baada ya kupinga wazo lile, mfalme alimlazimisha lakini haikuwezekana alizidi kupinga na kutoa sababu zake nyingine ambazo zilifanya mfalme akubali kumuacha aendelee kukaa kule nyumbani kwake.
MFALME: Sasa kama ukihitaji dawa utakuwa unawatuma vijana ambao watakuwa wakikusaidi.
MZEE SUBE: Sawa ila kwa hizi kazi sio rahis kumtuma mtu akakuchukulie dawa msituni na akakuletea kama unayohitaiji wewe. Kwahiyo usijari mtukufu mfalme nitafanya kazi kwa ufasaha zaidi japokuwa nitakuwa naishi mbali na eneo lako na mda wowote utakao nihitaji haraka nitawaslii.
MFALME: Sawa nimekuelewa.
Walipomaliza maongezi yao sube akamchukua mke wake na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwao, wakiwa njiani ndipo akaanza kuuliza kuhusu ile dawa.
MZEE SUBE: Ehe mke wangu nimekumbuka kitu nataka uniambie ile dawa wewe uliipata wapi?
BIBI SUBE: Hahaha wewe unajifanya kujua dawa sasa ilikuwaje ukashindwa kuigundua ile, tena bila mimi leo ungeumbuka. { Aliongea kwa kumdhihaki huku akiwa anacheka }
MZEE SUBE: Yani bila wewe mwanamke leo mimi sijui ningekuwa mgeni wa nani sijui na jinsi kijijini wasivyo tupenda mh.
BIBI SUBE: Na ndio maana nimekuwa mke wako ili endapo utakwama na jambo lolote nikusaidie.
MZEE SUBE: Mmmmh mwanamke una maneno mazuri wewe ila shida yangu kubwa nataka kujua ile dawa umeipata wapi?
BIBI SUBE: Nliipata kule msituni na ilitokana na ule mti mwingne.
MZEE SUBE: Haaaa kumbe sasa uliujuaje ule mti ni dawa.?
Bibi sube baada ya kuulizwa vile ndipo akaanza kutoa histori juu ya kuufahamu ule mti na kazi yake.
BIBI SUBE: Bibi kabla ajafariki siku moja alinchukua kule msituni kwa ajili ya kumsaidia kuchimba dawa zake, tukiwa msituni kwa bahati mbaya mimi nikang'atwa na nyoka ambae aliniambia kuwa ana sumu kal,. Akaniambia kuna mti mmoja tu ambao mizizi yake ndio itaweza kunisaidia kupona. Kutokana na uadimu wa ule mti ilfanya bibi kuangaika huku mimi hali yangu ikizidi kuwa mbaya zaidi. Alijitahidi kuutafuta ule mti bila ya kukata tamaa maana akupenda aone mimi nikipoteza maisha nikiwa bado mdogo tena mbele macho yake, Katika kuangaika sana akafanikiwa kuupata ule mti na kunitengenezea dawa, nilipoitumia mda mfupi mbele nikaanza kurudi kwenye hali ya kawaida.
MZEE SUBE: Mh! Sasa ikawaje baada ya hapo maana hiyo hstoria yako nimeipenda.
BIBI SUBE: mmmh na wewe kwa kupenda hadithi. {akaendelea kusimulia} Mda ukivyozidi kwenda na mimi nilizidi kupata uafadhari na hatimae nikapona kabisa, ndipo bibi akanichukua na kunipeleka kwenye ule mti na kuniambia ndio ulio nsaidia endapo nitapata ugonjwa wowote au kuumwa na mdudu wowote awe wa kutumwa au sio wakutumwa lazima nipone na hiyo sio kwangu tu bali kwa watu wote. Ila aliniambia kuwa ule mti una kawaida ya kupoteapote na huwa unaletwa na mzimu kwa mda fulani na hatimae unatoka pale ulipo na kwenda sehemu nyingine na tangu niuone wakati nipo mtoto ndio nimeuona tena ile siku na nilishindwa kukuambia chochote kutokana na sheria za pale msitu.
MZEE SUBE: Hapa nilipo kichwa chote kinawaka moto maana huo mti kama una kawaida ya kupotea sasa itakuwaje na wakati ule mti ndio dawa ya kuzuia sumu ya YOka ?
BIBI SUBE: Ndio hivyo ila nakumbuka aliniambia kitu kingine kama unataka uupate ule mti kwa urahisi inabidi uende usiku tena ukiwa umevaa zile nguo za kazi na unatakiwa uombe ile mzimu ikuonyeshe ule mti ulipo kwa mda ule.
MZEE SUBE: haaa! Kama ndio hivyo basi leo usiku inatakiwa twende kule msituni kwa ajili ya kuutafuta huo mti Maana Isije Yoka akamng'ata mtu tukashndwa kumsaidia kwa sababu dawa tayari imeisha.
BIBI SUBE: Sawa mume wangu.
Waliendea na safari yao huku wakiendelea kuiongelea ile dawa na hatimae wakafanikiwa kufika nyumbani kwao na kuanza kupanga dhana ambazo watazitumia hapo usiku kule msituni.
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Share App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi