
Mtunzi: Eliado Tarimo
SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
“Mpenzi mimi sijaelewa Yule mwanamke ni nani na mbona kila mtu alishtuka”Julieth alihoji.
“Jamani mpenzi mbona unpoteza kumbukumbu kirahisi hivyo huyu si ndo mke wa Lucas na hata jana si ndo huyu nilienda kumpigia simu”.
KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA NAYO...
Kimaro alijibu.
“Ohhh jamani kumbe ndo mzuri hivyo.. Pole shemeji yangu wacha tu upokonywe sio kwa uzuri ule” Julieth ilibidi ampe tu sifa zake.
Julian asasa hakuhitaji kuuliza tena maana alishajua mwanamke huo ni nani na kwa nini Lucas ana haki ya kuteseka. Alimuonea huruma sana na hakujuta kumpa faraja usiku wa jana. Alijiuliza mbona mwanume huyo anayajua sana mapenzi kitandani sasa inakuwaje mwanamke hamkimbie. Yaani wanawake sisi ni wajinga sana yaani kisa pesa mtu yupo radhi kumuacha mumewe aliendelea kuwaza Juliana. Walikunywa supu na dhairi Lucas Mnayama alionesha kuchanganyikiwa kabisa. Ilibidi washtuke na pombe kali kidogo walau kupunguza mawazo. Kimaro alimuonea sana huruma rafiki yake na akajikuta akiharsha ratiba zake. Waliendelea kunywa huku wakipiga stori mbalimbali. Wasichana hao walionekana kama na wao wameridhika na starehe za asubuhi maana hakuna hata mmoja ambaye alikuwa anasisitiza kuondoka na kusitisha kikao hicho.
Wakati wakiendelea na stori na vitu vingine mara simu ya Lucas iliita. Alipoangalia alikuwa ni Mama Vanessa mwanamke ambaye hakumfahamu na alikuwa akitaka waonane. Akakumbuka mwanamke huyo alimwambia kuwa ana mpango wa kusafiri hivyo ilimpasa kuonaa siku hiyo. Aliangalia saa ilikuwa ni saa sita mchana na kutoka Mwanza mpaka Musoma . Alimwambia kuwa yupo Mwanza ila atakuwa hapo baada ya masaa 3.
Walikubaliana kuwa wakutane saa 10 ili waweze kuonana na kujadili hicho alichokisema mama Vanesa. Ilibidi atafte njia ya kuga hapo na kuondoka. Alimwelza Kimaro kuwa inamps akuondoka ili aende kuoanana na mtua ambaye ansema kuwa anazijua habari za mke wake. Kimaro hakuridhika lalkini kwa kuwa alishapewa fununu juu y amwnamke huyo. Alaigana na Juliana na kumwambai kuwa watasiliana. Julaina alisangaa kuwa watawasilaina vipi hili hali hata namab za simu walikuwa hawajaombana. Ilikuwa ni ishu ya kufurahisha lakini alaiitiki akuwa watawasiliaana. Aliaga na kuondoka zake. Kimaro alimpeleka mpaka stend na kuhakikisha kuwa anapanda gari.Aliondoka na kuaza safari ya kuelekea Musoma. Alifika salama na moja kwa moja alielkea sehemu waliyopanga kukutana inayoitwa Dream Garden. Alivyofika hapo nje alinyanua simu na kumpigi amama Vanesa. Simu iliita mpka ikakatwa bila kupokelewa. Akasubiri kama baada y adakika akapiga tena na simu ikaendelea kuita bila kuokolewa.
Akawaza cha kufanya lakini hakupata jibu la haraka haraka zaidi aliamua kuingia ndani. Wanawake bwana ni watu wa ajabu sana huwa hawapendi muda kabisa sasa utakuta muda huu ndo kwanza bado yupo nyumbani. Mara kwa pemebni yake alioga gari la kifahari likipati na alishuka mwanamk mrembo sana amabye alikuwa akinukia marashi ya bei mbaya. Aliamua kuingi andani na liofika alikaa kwenye kiti ambacho ilikuwa ni rahisi kuona mtu yeyote ambaye angingia. Aliagaiz amaji na kuendelea kunywa. Aliangaza macho huku na kule lakni hakuona msichana aliyeingia. Hasira zilimpanda kwa sababu alishampigia simu mara mbili lakni hata hajamtafuta. Mara alimuona Yule mwanamke mrebo amabye alikuwa akimpigia simu akiingia. Hkauw ana mawazo kuwa huyo ndiye anayejihita mama Vanesaa maana yeye taswira aliyokuwa nayo kuwa mama Vanesa atakuw amtu wa makamo.
Mara simu yake iliita na alipoipokea swali lilikuwa amekaa wapi. Akamweleza na alishangaa kumuona Yule mwanamke akiongoza moja kwa moja mpaka pale alipokuwa amekaa. Lucas macho yalibaki yamemtoka na kuduwaa. Alipigwa na butwaa maaa na alaishindwa kuolewa kuw ahuyo ni mmama au mdada.
“Samahani sana kwa kuchelewa na kutopokea simu yako kwa wakati..Nikiwa naendesha gari huwa sipendi kupokea simu.
“Sawa karibu mama Vanessa” alisema Lucas huku akiendelea kumkagua hasa sehemu za kifuani. Kwa mawazo yake ya kupenda ngono tayari alishaanza kuwaza vitu ambavyo hakustahili kabisa..
“Kama nilivyojitambulisha mwanzo mimi naitwa mama Vanessa mwanamke maarufu hapa mjini na ni mke wa boss wako..
“Mke wa Boss wangu?”
“Ndio mimi ni mke wake na ndoa yetu ndo kwanza ina mwaka mmoja alinioa mimi mara baada ya mke wake wa kwanza kufariki..Nafikiri kipindi hicho wewe ulikuwa bado hujaja.
“Ni kweli hata mimi nilishasikia kuwa boss alifiwa na mke wake”.
“Kwa hiyo nimekuita hapa kwa ajili ya mpango wa kulipa kisasi. Nakuomba unisikilize kimakini sana maana tunaweza kuwa rika moja. Kwanza boss wako ana mtoto anayeitwa Vanesa mtoto huyu alikuwa mdogo wakati mama yake anafariki kwa hiyo usijefikiri mimi ni mkumbwa. La hasha mimi ni mdogo ila nimejikuta nikiingia kwenye maisha ambayo sikuyatarajia. Pesa na upendo wa uwongo umenifanya niolewe na boss wenu. Kwa sasa sina amani kabisa na sina furaha aninipa kila kitu isipokuwa mapenzi.
Hana mapenzi ya kweli amekuwa Malaya yaani anabadilisha wanawake kama nguo. Yaani huyu baba ana mtoto wake mkumbwa ambaye ndo ameingia chuo huwezi amini huyo motto na baba yake ni kitu kimoja. Mtoto anadiriki kumtafutia baba yake wanawake. Yaani anawaunganisha na rafiki zake.Nanyanyasika sana mimi na uzuri wangu huu baba Vanesa anatembea mpaka na wasichana wadogo ambao hata hawana mvuto kunizidi mimi. Ninajua kila kitu kuhusu wewe najua jinsi gani ulivyonyanyasika mpaka ikafikia kusimamishwa kazi na mbaya zaidi amemchukua mke wako. Nasikia amempa moja ya nyumba zake ambazo amejenga kwa siri ambazo hata sisi wanafamilia hatuzijui. Kwa nini huyu mwanaume anafanya hivi tena kwa vijana wadogo kama ninyi?”
Mama Vanessa aliongea kwa uchungu sana huku akifuta machozi. Alikuwa na hisia ambazo kwa kweli Lucas hakutarajia.
“Pole mama Vannesa na mimi naumia sana, naumia kuliko hata unavyoweza kufikiri, embu tazama hizi picha kisha ndo utagundua kuwa huyo mumeo sio mwanadamu kabisa, hana utu ni mnyama aliyepitiliza”
Lucas alimpa simu yake na kuanza kumuonesha picha zile ambazo alimpiga akiwa na mkewe huko Mwanza. Mwanaume huyo hakuamini na badala yake alianza kulia kwa nguvu. Alilia kama mtoto jambo lilomfanya Lucas aanze kumbembeleza…
Katika kitu ambacho Lucas huwa kinamnyima raha ni kuona mwanamke akilia mbele yake. Yaani yeye mwanamke akijilIza basi huwa anamwamini kupita kiasi. Alimbembeleza mpaka Mama Vanesa akanyamaza. Kwikwi zilimkaba sana na alikuwa akiona kabisa kijana huyo ameonewa. Mwanzo hakuwa na ushahidi wa moja kwa moja lakini zile picha zinazomuonesha mme wake akiwa na mke wa Lucas zilimuuma kupita maelezo.
“Kwa hiyo haya yote yametokea nini sasa kifanyike” Lucas alihoji mara baada ya mama huyo kubembelezwa na kurudi katika hali yake ya kawaida.
“Ndo maana nimekuita hapa ili tupange mambo na ikibidi tumkomeshe”
“Wewe unataka tumfanyeje hili hali yeye ni boss mwenye fedha. Nikikuruka na kujifanya mjuaji sana ndo nafutwa kazi kabisa.”
“Siku zote usikubali kupoteza haki yako kisa kuogopa kufukuzwa kazi. Usikubali kunyang’anywa mke au hata uhuru wako kisa pesa. Nakuambia tukiungana mimi na wewe tutafanikiwa kwa hili. Dawa ya moto ni moto na hivi tunaushahidi, hiyo kazi huwezi kufukuzwa. Mimi ndo Emmy hilo jina la mama Vanessa ni la heshima tu.
“Sawa Emmy ingawa nitapenda kukuendelea kukita mama Vanesa ni jina zuri linatamika vizuri. Ingawa mtu anavuta taswira laba ni mama kweli”.
“Kila mwanamke ni mama maana hata kama bado hajazaa ipo siku atakuja kuzaaa”. Sio mbaya ukiiita hivyo maana hata Vanesa mwenyeewe anajua kuwa mimi ndo mama yake. Alifafanua mama huyo.
“Sawa lakini bado sijajua mpango mkakati ni upi?
“Ni mdogo tu ukitendwa tenda, ukipendwa pendwa”.
Maneno hayo yalikuwa bado yanamuacha njiapanda Lucas Manyama hakujua mwanamke huyo alikuwa akitaka nini hasa kutoka kwake. Maneno hayo kwake yalikuwa yakiahshiria kuwa mama huyo alikuwa akitaka alipe kisasi kwa wao kuwa wapenzi. Kuna vitu vilikuwa vikimtatiza kwanza kwa nini mama huyo alichagua njia hiyo ya kulipa kisasi kwa nini wasipeleke ushahidi a idara ya kazi na kueleza kuwa alikuwa akisimamishwa kazi kwa sababu ya hujuma za boss wake ambaye alitumia uboss kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe. Hili jambo lilimuumiza sana hasa akikumbuka ni mbali sana alipotoka. Alifikiria jinsi alivyomsomesha mke wake tena kwa tabu mpaka akafanikiwa kupata elimu na baadaye kazi. Alifikiria tukio la yeye kusimamishwa kazi na kuona kabisa haikuwa sawa. Wakati Lucas akiwaza na kuwazua mara simu ya mama Vanesaa ikaita.
Mama Vanesaa aliangalia na kusita kupokea maaana aliyekuwa akipiga ni baba Vanessa. Simu haikukukoma maana ilivyokata ikapigwa tena na safari hii mama Vanesaa alipokea.
“Upo wapi mke wangu maana ndo nimerudi kutoka Mwanza kwenye semina nimefika nyumbani sijakukuta?”
“Nimetoka kidogo mme wangu na si muda mrefu nitakuwa hapo kuna vitu tu nilienda kuvinunua kwa ajili ya safari yangu ya kesho.”
“Sawa huwai kurudi basi maana nimekumisss sana na nimekuletea zawadi nzuri mke wangu..
“Usijali honey nakuja”.
Lucas Manyama alikuwa ametega sikio na kusikiliza kila kitu kilichokua kikzungumzwa. Aliisikia vyema sauti ya boss wake. Roho ilimuuma na hakutarajia kwa picha zile zikimuonesha mke wake na boss wake wamekumbtaina wakicheza musiki Mama Vanesa angeweza toa majbu ya kukera yenye hasira. Na mama Vanesa hasingeongea hivyo kama vile hakuna kitu kibaya kilichotokea. Alitarajia mwanamke huyo atamtukana mwenyewe.
“Samahani boss wako amepiga na usiumie kwa mimi kuongea naye vizuri. Cha msingi tambua namtafutia dawa ya kumkomesha na mimi siku zote maishani mwanangu huwa sipendi kukurupuka na iktokea tatizo huwa natafuta njia ambayo itamuumiza muhusika. Kwa hiyo mkakati upo hivi mimi naenda Dar nitakaa kwa muda wa wiki moja kisha nitardi. Baada ya hapo tutakutana lakini nakuomba kwa wakati huu tuwe makini sana usikurupuke katika maumivu tufanya kama hakuna kibaya cha kuumiza moyo kilichotokea.
Mama Vanesaa baada ya kusema hayo alifungua pochi yake na kutoa burungutu la pesa na kumkabidhi. Alitabasamu na kumuaga. Lucas alitamani amwambie hasiondoke lakini tayari ilikuwa ni hatari kama mme wake alishakuwa mjini. Mme wake licha ya kuwa boss katika benk ambayo alikuwa akifanya Lucas pia alikuwa ni mfanyabiashara hapo Musoma na nadiriki kusema alikuwa tajiri. Mama Vanesaa kazi yake kubwa ilikuwa kusimamania biashara hizo. Kwa hiyo ni mwanamke ambaye alikuwa akikutana na pesa karibu kila siku.
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Share App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi