SHEREHE KUZIMU (21)
Jina: SHEREHE KUZIMU Mtunzi: Frank Silaa SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA ILIPOISHIA... Japokuwa pamoja na misukosuko mikubwa iliyokuwa inaikumba kuzimu, lakini bado waliendelea na vikao vyao kwa shida ili waweze kumuangusha mchungaji na kanisa lake. Maisha ya Nelson yaliendelea kama kawaida ingawa yalitawaliwa na upweke sana. KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA NAYO... Alizoea kupokea ushauri kutoka kwa mama yake. Wakati mwingine alipokuwa akikata tamaa kutokana na changamoto za dunia hii, mama yake alimtia moyo. Hata wakati alipokuwa akifiwa na watoto wake bado alihisi faraja ndani ya moyo wake kutokana na uwepo wa mama yake. Sambamba na hayo yote lakini pia alideka pindi alipokuwa anaiona sura ya mama yake ikitabasamu mbele ya macho yake. Kifo cha ghafla cha mama yake kilipelekea Nelson ahisi kama vile ametelekezwa peke yake jangwani. Muda mwingi alikuwa ni mtu wa kulia pindi anapokuwa anawaza mapenzi ya m…