SHEREHE KUZIMU (23)
Jina: SHEREHE KUZIMU Mtunzi: Frank Silaa SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU ILIPOISHIA... Benedict aliendelea kufanya mambo mengi mazuri kwaajili ya msichana ambae alitokea kumpenda kwa moyo wake wote. Kwa kadiri siku zilivyozidi kwenda ndivyo ambavyo moyo wa Adela ulivyozidi kulainika. KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA NAYO... Adela ni msichana mrembo, tena bado bikira. Hata yeye mwenyewe anafahamu kwamba amejaliwa ulimbwendwe haswa. Achilia mbali uzuri aliojaliwa lakini pia amejaliwa utashi wa hali ya juu. Jamii nzima iliyokuwa inamzunguka ilikuwa inamuheshimu kwasababu yeye pia alikuwa anajiheshimu. Nguo zake zilikuwa ni za heshima, na pia marafiki zake walikuwa ni wa heshima pia. Alikuwa na malengo marefu ya kufika mbali kielimu. Hakuwa msichana wa kupayuka payuka kama walivyo mabinti wengi wa siku hizi. Lakini pia hakuwa mtu wa kupenda njia fupi ya mafanikio kama ambavyo wasichana wengi wa karne hii ya 2…