SHEREHE KUZIMU (26)

Zephiline F Ezekiel
SHEREHE KUZIMU (26)
Jina: SHEREHE KUZIMU Mtunzi: Frank Silaa SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA ILIPOISHIA... Miongoni mwa wagonjwa wanaoonekana kuwa na hali mbaya zaidi ni pamoja na Benedict . Hivyo basi hali yake mbaya inapelekea jopo la madaktari kukusanyika kwa pamoja ili waweze kuokoa maisha yake. KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA NAYO... Mapigo yake ya moyo yanadunda kwa mbali sana. Hivyo matumaini yanazidi kuwapotea madaktari wanaomuudumia kwa nguvu zao zote. Kiukweli hali ya kijana huyu ni mbaya sana kwasababu madaktari wanajaribu kubusti mapigo yake ya moyo bila mafanikio. Hali ya Adela nae bado ni mbaya sana kwasababu, fahamu bado hazijamrejea. Kwa mujibu wa madaktari, wamebaini kuwa binti huyu ameumia zaidi kichwani. Kwahiyo wanaendelea na jitihada za kuokoa maisha yake. Hali tete aliyonayo, imepelekea sura yake ya mvuto kuonekana kama vile ya kikongwe. Ule uzuri wake ambao ulikuwa ukimchanganya Benedict hauonekani tena…