SHEREHE KUZIMU (28)
Jina: SHEREHE KUZIMU Mtunzi: Frank Silaa SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE ILIPOISHIA... Baada ya kufika ghorofa ya tatu, Nelson alikuwa akihema kwa kasi sana kwasababu ngazi zilikuwa zimemchosha halafu maumivu bado yalikuwa yanamuandama. Kwa jinsi alivyokuwa anajihisi vibaya, aliinama akiwa ameshika magoti kwa uchovu huku akisikilizia jinsi moyo ulivyokuwa ukimwenda mbio. KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA NAYO... Mwili wake ulikuwa unavuja jasho jingi ambalo lilipelekea shati lake kulowa jasho mithili ya mtu aliyenyeshewa na mvua kubwa. Hata hivyo kwasababu alikuwa na siku ya pili mwili wake haujagusa maji, makwapa yake yalikuwa yanatoa harufu kali. Baada ya dakika tano akiwa ameinama anahema juu juu, alinyanyua kichwa chake na kisha macho yake yakakutana na kibao kidogo kilichobandikwa kwenye mlango uliokuwa mbele yake. Ukiwa umeandikwa namba 7 kwa rangi nyeupe. Moja kwa moja akaanza kutembea kufuata korido …