BABA KIUMBE WA AJABU (1)

Zephiline F Ezekiel
BABA KIUMBE WA AJABU (1)
Jina: BABA KIUMBE WA AJABU Mtunzi: Ally Mbetu SEHEMU YA KWANZA Katika dunia ya Mungu kuna mambo mengi ambayo ukihadithiwa unaweza kudhani ni simulizi za kutunga na za kusisimua. Lakini siku zote kila aisifiaye mvua basi ujue imemnyea. Dunia imezungukwa na siri nzito ndani ya majumba ya watu, kuna mambo mazito ambayo ni chukizo kwa Muumba. Si kila mwenye maisha mazuri au tajiri mali alizonazo kazipata kihalali. Wengi utajiri wao unatokana na nguvu za giza, utajiri anaoambatana na kutoa kafara ya kitu. Wapo wanaotoa kafara watoto, wake au waume zao, pia wapo wanaowageuza watoto, wake au waume zao kuwa mandondocha kama ‘chuma ulete’ wa kuwaongezea kipato. Nyumba nyingi huwa na vyumba vya siri ambavyo huwa havifunguliwi kutokana na masharti ya mganga na kufanya watu wabaki na maswali. Pia nyumba nyingine unakuta kuna mtoto ambaye akili zake si nzuri, akikaa yupoyupo tu, mate yanamtoka ovyo kumbe ni dawa ya utajiri. Ajabu huyo ndiye anakuwa kipenzi cha baba ambaye anajua siri yake. Wapo ambao hu…