BABA KIUMBE WA AJABU (2)
Jina: BABA KIUMBE WA AJABU Mtunzi: Ally Mbetu SEHEMU YA PILI TULIPOISHIA... “Masalu utajiri wetu una siri nzito.” “Siri! Siri gani hiyo?” “Masalu utajiri wetu una siri nzito ambayo mimi ndiye niliyeibeba na sasa hivi nimeitua.” “Una maana gani kusema hivyo?” “Masalu kuna mambo huwezi kuyajua kutokana na umri wako, JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 SASA TUENDELEE... lakini kutokana na ukaribu na kuelewana kwetu sina budi kukufunulia yaliyojificha ili ujue nini kimetuzunguka. Mwanzo nisingeweza kukuambia kwa vile nimeelezwa kuwa maisha yangu hayatakuwa marefu hivyo leo nimefurahi sana kuja hapa. Haya nitakayokueleza leo si ya kutunga na kila ulilokuwa na swali nalo leo nitakupa jibu lake. “Masalu mdogo wangu maisha yetu kabla hujazaliwa yalikuwa ya kawaida tu, baada ya baba kustaafu kazi pesa alizolipwa alinunua nyumba mnayoishi sasa hivi na pick up moja ambayo alifanyia kazi zake za kutuingizia kipato na kufungua duka a…