BALAA (10)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA KUMI ILIPOISHIA... Wakati akiwaza hayo alisikia mlango ukifunguliwa kwa nje. Ukafunguka kidogo na mtu mpya alisukumwa kwa nguvu kuingizwa mle ndani. Dokta Yusha alimwangalia vizuri mtu yule walitambuana. "Wamekuleta huku Dokta" JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... "Nawe wamekuleta huku" Ilikuwa ni kushangaana tu. Mtu yule alikuwa ni mmoja wa askari wa kituo cha Polisi Masoko . Tena ndiye askari aliyemhoji dokta Yusha alipoenda Polisi ….. "Eeh imekuwaje ukafika huku" Dokta Yusha aliuliza kwa wahka mkubwa. Huku akiwa amesimama yule askari alianza kuelezea. "Ulivyoomba kutoka pale Polisi ili kwenda kwenye mazishi ya Mwanasheria tulikukubalia, lakini ulivyotoka tu tulikubaliana tukufuate kwa nyuma, na ni mimi ndiye niliyepewa jukumu hilo. Nilikufuata kwa nyuma kila ulikoenda. Mpaka wanakuingiza kwenye gari mimi nilikuwa nashuhudia. Lakini …