HATI FEKI (4)
Jina: HATI FEKI Mtunzi: Hassan S. Kajia SEHEMU YA NNE ILIPOISHIA... Walitumia dakika ishirini tu kufika Njiro nyumbani kwa kina John. Walikuta watu watatu wakiwa wamesimama nje ya geti. Mlinzi aliwafungulia na kuingia. John alikuwa bado hajawatambua hadi alipofikia geti kabisa. Mlinzi alifungua geti kubwa na kuliruhusu gari la John kuingia. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... John sasa alimtambua mmoja kati ya wale wageni. "Hawa ni wachimbaji wa mgodi wa baba,” John alimwelezea Aminata . "Namkumbuka mmoja tu, aliyevaa kapelo. Sijui wanataka nini.” John alishuka kwenye gari na kumfungulia Aminata mlango, alimkaribisha kisha kuwafuata wale wachimbaji. "Mbago bila shaka," John aliuliza. "Ndiyo mkuu, ni mimi, habari za siku nyingi bosi?" Antony naye alikuwa akitoka nje baada ya kusikia gari likiingia na watu wakiongea. Alisimama mlangoni. Aminata alimwangalia sana kisha kumgeukia John…