HATI FEKI (8)
Jina: HATI FEKI Mtunzi: Hassan S. Kajia SEHEMU YA NANE ILIPOISHIA... Hawakuona lolote zaidi ya miili ya askari wenzao. Ghafla John aliwatokea na kuwamiminia risasi ambazo ziliwashtua Mosses na wenzake. “Wafuateni,” alifoka Mosses akiwaamuru askari waliobaki wawafuate wenzao. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Huko yaliwakuta yaliyowakuta wenzao. Yeye pamoja na walinzi wenzake wligeuza gari na kuanza kuondoka. Antony alikutana na Mbago pamoja na wachimbaji wengine. Walivamia migodini na kuwatoa watu wote na kuhakikisha hakuna askari yeyote wa Mosses aliyesalia. Antonuy alitaka kuwajulisha juu ya kilichokuwa kikiendelea. Usiku huohuo ambapo hali ya mji wa Mererani haukuwa tena shwari ilisikika tu milio ya risasi. Msafara ulivurugika. hali ilizidi kuwa mbaya zaidi. Mashambulizi sasa yalihamia barabarani. Mosses na watu wake waligeuza na kuanza kukimbia wakielekea mjini. John na Aminata waliwaona na hivyo hawaku…