JAMANI DADA MARTHA... LOOO! (5)
Jina: JAMANI DADA MARTHA... LOOO! Mtunzi: 2jiachie SEHEMU YA TANO ILIPOISHIA... Ulikuwa mchana wenye mawazo kwa Martha...akiwa ametulia tuli huku wachache wakiendelea kulia, aliwaza... “Hivi kweli yule ni kaka yangu au mume wangu? Ina maana anaweza kunijali kiasi hiki kweli?” JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... alijiuliza Martha huku akiiangalia meseji ya pesa aliyotumiwa na Roi. *** Wiki moja ilikatika tangu mazishi ya mume wa shangazi yake Martha, siku hiyo Martha alikaa kwenye mgahawa mmoja akimshukuru Roi kwa ushirikiano wake katika msiba... “Wala usijali dada yangu. Tuko pamoja.” “Yaani bro kusema ukweli umenipa kampani kubwa sana.” “Usijali dada yangu.” “Asante sana,” alisema Martha huku akimwangalia Roi, wakakutana macho, wote wakajikuta wakisisimka... “Brooo,” aliita Martha kwa sauti iliyojaa mahaba . “Yes sista...” “Uko sawa?” “Yeah! Nipo sawa sista, wewe je?” “Mh!” aliguna Martha bila kusema kama yuko sawa a…