KONSTEBO NGUZU (12)

Zephiline F Ezekiel
KONSTEBO NGUZU (12)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA KUMI NA MBILI ILIPOISHIA... "Ni akina nani hawa? na wanataka nini?" Alijiuliza huku akiendeleza bidii katika kupapasa. "Mamaaaaaa!" kelele kubwa zilisikika ghafla mbele yake na hapo akasikia vishindo vikiambaa kwa kasi. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Mungu wee! nini hiki? alijiuliza huku kwa mara ya kwanza akianza kupatwa na wasiwasi moyoni. Akatulia tuli katika giza lile akisubiri kitakachojiri. Hakuna aliyesogea, akasikia gari likiwashwa na kisha akauona mwanga kwa mara ya kwanza. Mwanga ulipenya katika mboni ya macho yake katika namna ya kumsumbua. "Tulia hapohapo mwanga mkubwa wewe!" sauti ikamuamrisha. Akatulia tuli huku akikumbuka nidhamu ya kunyoosha mikono yake juu. Hatua zilizizidi kusogea hadi alipokuwa. "Toa hicho kitambaa" Akaamrishwa. Akaanza kujitazama. "Toa kitambaa usoni!!" sauti ikaamr…