KONSTEBO NGUZU (15)

Zephiline F Ezekiel
KONSTEBO NGUZU (15)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA KUMI NA TANO ILIPOISHIA... Baba yangu mzazi ambaye alipigana vita ya Majimaji huko Songea alikuwa akiniongezea ujasiri, ni kweli alikuwa akinyanyaswa na wazungu na aliwaogopa kweli lakini alikuwa akinieleza kuwa katika vita ile kwa mkono wake wa kuume akiwa na rungu kubwa aliwauawa wazungu watano. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Kwake ulikuwa ni ushindi mkubwa sana kumtandika mkoloni na bunduki yake mkononi. Ni kweli watanganyika wengi walipoteza maisha lakini hii ilikuwa alama kubwa sana kuwa waliutaka uhuru kwa namna yoyote. Baba alinieleza kuwa baba yake ambaye ni babu yangu alipoteza maisha kwa kunyongwa, na ni yeye ndiye alikuwa mmiliki wa jina la Nguzu ambalo maana yake ni NGUVU. Jina Florian nilipewa na hawa ngozi nyeupe waliojifanya miungu katika ardhi yetu, silipendi jina hilo. Naitwa Ngengekuzenza Nguzu . Yaani ‘ Aliyerithi Nguvu ’. Baba yan…