KONSTEBO NGUZU (17)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA KUMI NA SABA ILIPOISHIA... Majira ya saa sita usiku aligutuka kutoka usingizi huku jasho likimtoka sana. Majenga ! jina hili likakivamia kichwa chake, akaketi kitako na kuanza kukumbuka juu ya maneno yale aliyokuwa akiyasoma yule mzee. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Akatamani asubuhi ifike upesi aweze kuendelea kusikiliza ni kipi ambacho kitakuwa na faida kubwa sana kwake. Akamaizi kuwa licha ya kushtuka vile na kuandamwa na jina hilo lakini pia alikuwa pia amebanwa na haja ndogo. Na choo kilikuwa mita nyingi kutoka chumba alichokuwa amelala. Akapatwa na uvivu sana huku akijilaumu kwa kukataa kunywa maji mengi baada ya chakula cha ili asije kupata shida kama hizi usiku na sasa amezipata shida zilezile. Akajivuta taratibu kuelekea choo kilipokuwa. Nje palikuwa kimya sana, walisikika wale viumbe wanaopenda kulala mchana kisha usiku wanazurura kusumbu…