KONSTEBO NGUZU (25)

Zephiline F Ezekiel
KONSTEBO NGUZU (25)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO ILIPOISHIA... Juma Kihwele akajihesabia kuwa amekutana hatimaye na mtu ambaye atamuelewa na kumwokoa. Hakujua kuwa amekutana na anayewatuma wale aliowaona kama mashetani yanayoishi. "Haujambo?" JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Jeremiah aliuliza kifedhuli. "Sija... shkamoo... sijambo.." alijiumauma katika kujibu. "Martin Nguzu alikufa ama hakufa? na kama hakufa nataka kujua ni nani aliyehusika katika kumwokoa..." Sauti kavu ya Jeremia ilihoji. "Sijui lolote muheshimi..." kabla hajamaliza kumjaza cheo alipokea kofi kali katika shingo yake. Yowe la hofu likamponyoka. "Nahitaji jibu tofauti na sijui." "Muheshimiwa mi naapa haki ya..." Hata hii kauli pia haikumalizika kabla hajapokea kofi jingine, hili la sasa liliuchana mdomo wake. "Umeona biblia ama msaafu humu ndani? Sihitaj…