KONSTEBO NGUZU (5)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA TANO ILIPOISHIA... Akapanga kukabiliana na hili jambo kabla halijakomaa, akasimama imara akapiga saluti na kujiapiza kuwa hatalala tena na kulialia kama mtoto badala yake atapambana kiume. Hakujua kuwa wakati yeye akiamua kusimama, kuna ambao walikuwa wakikimbia mbio kali kwa nia ya kumzamisha katika shimo lenye kiza kinene. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... "WAKATI mzuri zaidi wa kufanya mabadiliko katika maisha yako ulikuwa ni miaka kumi iliyopita..... WAKATI mwingine mzuri zaidi ni SASA! Usije ukathubutu kusema kuwa umechelewa kufanya mabadiliko katika maisha yako......fanya SASA" ALIJARIBU kujiaminisha kuwa huenda amesikia vibaya, akazidi kujikunja kitandani ili asinzie vizuri. Lakini mlango ulipiga kelele tena, kuna mtu alikuwa anaugonga. Akiwa na mawenge ya usingizi aliufikia mlango na kuufungua bila kuuliza ni nani alikuwa anahitaj…