KONSTEBO NGUZU (6)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA SITA ILIPOISHIA... Heri yako bado unanitii! akajisemea, huku akiukunja mguu wake na kujaribu kuvuta taswira ya kitu kilichomfanya ashtuke usiku wa manane na kuanza kubabaika. Moshi mnene! hiki nd'o kitu kilichokuwa kikitishia afya ya akili yake kwa wakati ule. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Akainyanyua simu yake na kujaribu kupiga katika nambari alizokuwa amepiga awali na hazikuwa zikipatikana. "Ni kweli Sule anavuta bangi tena sana tu, lakini sidhani kama bangi yake inaweza kumfanya akafanya upuuzi mkubwa namna hii..." Akajisemea huku akiketi. Alipoketi na kuwa kimya kwa muda kidogo akakumbwa na kitu ambacho kilimfanya ashindwe kuketi bali kusimama wima kabisa. Kuna vitu viwili vilikivamia kichwa chake, ulikuwa ni mfano wa picha ambazo zilikuwa gizani na sasa akabaini kuwa aliziona lakini pasi na uhakika. Picha ya kwanza ilikuwa ni …