
Mtunzi: George Iron Mosenya
SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
"Shangazi, sijui lolote kuhusu huu mpango unaousema, sijawahi kuzungumza na Inspekta juu ya lolote kuhusu Nguzu. Hii ni kweli ya moyo wangu..."
"Sawa kama haujui. Mimi naondoka..." alizungumza doktahuku akiyanyanyua mabega yake juu.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
Akauendea mlango na kutoweka.....
_______
LILIANZA kuwa saa moja, kisha likafuata la pili yalipofika matatu subira ikafikia kikomo. Inspekta Kobo akachukua simu yake na kujaribu kumpigia mkewe amuulize nini kinajiri hadi hajafika nyumbani hadi muda huo.
Simu iliita kidogo kisha ikakatwa. Alipojaribu tena haikuwa ikipatikana. Akajaribu kupiga ofisini wakaelezea kuwa Dokta Kobo alitoka kazini tangu saa mbili usiku, wakastaajabu kupokea simu usiku wote huo wa kuuliziwa kwake.
Inspekta Kobo ambaye tayari alijiona ni mtu ambaye ameandamwa na majanga ya ghafla akaingiwa mchecheto, haikuwa kawaida kwa mkewe hata kidogo kuchelewa nyumbani.
Akafikiria kuwapigia rafiki zake wachache aliowafahamu lakini mshale wa saa ulimfanya aone haya.
Saa nane usiku kumuulizia mke!
Hapana.... Akaendelea kungoja huku pepo la wivu likianza kumchokonoa, akajiuliza ikiwa yeye ameweza kuwa na mwanamke nje inashindikana vipi kwa mkewe?
Swali hili likamghadhabisha na kujiona hatendewi haki hata kidogo ikiwa ni kweli mkewe amediriki kufanya hayo.
Usingizi ulimsomba majira ya saa kumi na moja kasoro dakika chache.
Akagutuka saa moja na nusu asubuhi na bado mkewe alikuwa hajarejea nyumbani wala simu yake ya mkononi haikuwa ikipatikana.
Hofu ikatanda maradufu.....
LILIANZA kuwa saa moja, kisha likafuata la pili yalipofika matatu subira ikafikia kikomo. Inspekta Kobo akachukua simu yake na kujaribu kumpigia mkewe amuulize nini kinajiri hadi hajafika nyumbani hadi muda huo.
Simu iliita kidogo kisha ikakatwa. Alipojaribu tena haikuwa ikipatikana. Akajaribu kupiga ofisini wakaelezea kuwa Dokta Kobo alitoka kazini tangu saa mbili usiku, wakastaajabu kupokea simu usiku wote huo wa kuuliziwa kwake.
Inspekta Kobo ambaye tayari alijiona ni mtu ambaye ameandamwa na majanga ya ghafla akaingiwa mchecheto, haikuwa kawaida kwa mkewe hata kidogo kuchelewa nyumbani.
Akafikiria kuwapigia rafiki zake wachache aliowafahamu lakini mshale wa saa ulimfanya aone haya.
Saa nane usiku kumuulizia mke!
Hapana.... Akaendelea kungoja huku pepo la wivu likianza kumchokonoa, akajiuliza ikiwa yeye ameweza kuwa na mwanamke nje inashindikana vipi kwa mkewe?
Swali hili likamghadhabisha na kujiona hatendewi haki hata kidogo ikiwa ni kweli mkewe amediriki kufanya hayo.
Usingizi ulimsomba majira ya saa kumi na moja kasoro dakika chache.
Akagutuka saa moja na nusu asubuhi na bado mkewe alikuwa hajarejea nyumbani wala simu yake ya mkononi haikuwa ikipatikana.
Hofu ikatanda maradufu.....
Asubuhi akapokea ujumbe mfupi kutoka kwa mkewe.
"Nipo salama mume wangu, nipo kwa mama mdogo. Kuna jambo limenichanganya naomba uniache kidogo natafuta suluhisho. Watazame watoto..."
Inspekta akaufuta ujumbe ule. Alimjua vyema mkewe, haikuwa mara ya kwanza kuwa katika hali hiyo na kuamua kuwa mbali na mumewe.
"Nimemkwaza nini huyu?" alijiuliza lakini akipata ahueni kuwa mkewe yupo salama.
_____
Mwanaume mweusi sana mwingi wa misuli katika mikono yake alikuwa amejitwika mfano wa gunia katika bega lake, mwili wake ulitokwa jasho lililoufanya ung'are kana kwamba ametoka kuogelea katika dimbwi la mafuta ya kula.
Alijitutumua na gunia lile huku akitweta.
Lilionekana kumzidia, lakini hakuwa tayari kukubaliana na hali ile moja kwa moja.
Macho yake makali mithiri ya nyoka yalikuwa makini kutazama huku na kule ikiwa kuna kitu kibaya aweze kujihadhari.
Zaidi alililinda lile gunia kuliko alivyowaza kujilinda yeye mwenyewe.
Alipoufikia mlima aliliweka chini lile gunia akapumzika kidogo kisha akajitwika tena na kuendelea na safari ile ambayo mwisho wake haukuwa bayana ikiwa ni wa matumaini ama la.
Kilima kikamalizika akaanza kupita katika vichaka vya hapa na pale, mwisho akaufikia mto na kuanza kuogelea. Gunia likiwa juu kabisa, japo lililowana lakini haikuwa kwa kiasi kikubwa sana.
Mkondo wa maji ulikuwa una nguvu sana lakini bwana yule mwenye misuli mingi alifanikiwa kuwa imara zaidi akapenya na kutokea upande wa pili.
Huko akapokelewa gunia lile huku akipongezwa na wenzake wawili waliosaidiana lile gunia.
Hawa nao walikuwa imara sana mmoja akiwa mfupi na mwingine mrefu. Wote weusi miili yao, wakaendelea na safari ya gunia lile kuelekea pahali lilipohitajika kufikishwa.
"Hivi mali itakuwa salama kweli?" Mmoja akahoji wakati wa pumziko fupi la kubeba gunia lile.
Swali lile likazua ukimya wa muda, wakalitazama gunia kwa pamoja. Kisha wakaangaliana kana kwamba waliambiana sekunde za kulitazama na sekunde za kutazamana.
Ukafuata mguno kwa pamoja tena.
"Unahisi jamaa atakuwa amefanya madhara yoyote?" aliyeulizwa swali naye akauliza swali kabla hajajibu alichoulizwa.
"Au tufungue kidogo?" Swali tena kutoka kwa muulizwa.
Swali hili likawafanya tena walitazame lile gunia kwa muda, halafu bila kukubaliana wala kupingana wakalibeba lile gunia safari ikaendelea.
Hawakulifungua!
Ilikuwa safari ya masaa kadhaa hadi walipolitua gunia mahali lilipostahili. Wakatulia wakilitazama kwa takribani dakika moja kisha wakainama na kulifungua gunia lile.
Waliacha wazi kisha wakatoweka.
Zikapita dakika kadhaa akaingia bwana aliyebeba bakora mkononi mwake, akalifikia lile gunia bila kusema neno lolote akaanza kuishusha bakora yake mara kadhaa guniani.
Gunia lilikuwa limetulia tuli bado.
Akazidisha juhudi kuliadhibu gunia lile na chochote kilichokuwa ndani yake huku akizungumza maneno mengi ya kulifokea na mengine ya kusihi. Jasho lilikuwa limemlowesha mwili mzima na alikuwa anatetemeka sana.
Baada ya bakora ya kwanza kuonekana haitoi adhabu ipasavyo akabadilisha bakora, akachukua ndefu zaidi.
Akaizungusha kwa ghadhabu zote akaitua katika gunia.
Gunia likatikisika!
Mchapaji akatulia tuli asiamini kile alichokuwa anakiona, akaanza kupiga mayowe akiwaita wenzake kutokea katika giza.
Kelele zile zikawa tishio kwa mali iliyokuwa katika gunia lile.
Kilianza kidole kutikisika na kisha macho yakaanza kulazimisha kuiona nuru.
Akajaribu kugeuka lakini akahisi maumivu makali yanamwandama na kuna kitu kizito kilikuwa kimeuegemea mwili wake.
Akajaribu kuongea akahisi koo limekauka sana huku kiu kikuu kikimwandama.
"Nini hiki?" alijiuliza baada ya kugundua kuwa ile si ndoto bali ni kweli tupu.
Akatuliza akili na kujaribu kufikiri tena na tena lakini hakuna jibu alilopata.
Akatumia nguvu ili aweze kujigeuza tena ikashindikana. Alipovuta pumzi zake akagundua kuwa hapumui vizuri sana. Kuna kitu kingine kilikuwa kimebana katika kifua chake.
"Hakikisheni amekufa aisee! Ishu sio nyumba ishu ni yeye..." Masikio yake yakazisikia sauti zikihimizana.
"Kina nani hawa Mungu wangu!" alihamaki akiwa palepale katika wakati mgumu.
Akajikuta anaijiwa na fikra mbili za ajabu zilizooana, akajihisi kuwa muda si mrefu alisikia shangwe na maneno ya kuhimizana huku akiwa amefunikwa katika kitu asichokijua na sasa anasikia maneno mengine akiwa mahali tofauti kabisa.
Ni nani hawa watu? alijiuliza.
Na nipo wapi hapa sasa eeh!
Milango ya fahamu yote ilikuwa imefanya kazi yake kwa ukamilifu, macho yaliishia kuona giza, masikio yakisikia sauti za ajabu, ngozi ilikuwa imebanwa na kitu asichokijua, ulimi ulibaini kiu kikali kutokanana ukavuu wa mdomo na koo, pua yenyewe ilikuwa imelala huku ikisahau wajibu wake.
Ikakurupuka na upesi baada ya kugundua kuwa bosi wake ameamka.
Ikanusa na kumweleza bosi wake kuwa kuna harufu ya petroli na moshi.
Moto! Akili ikaungana na pua kutoa majibu.
Mungu wee! nilichomewa ndani mimi! akajisemea na ili kuhakikisha kama haoti akajaribu kujipapasa.
Alikuwa uchi wa mnyama.
Ndio, mara ya mwisho alivua nguo zake harakaharaka baada ya kugundua kuwa hawezi kuukwepa moto ule upesi lakini angeendelea kubaki na nguo moto ungemvamia upesi kulikoni alivyokuwa mtupu.
Inspekta amenichoma moto! alijaribu kutoa sauti.
Akaishia kunong'ona, zile sauti alizozisikia nje zikawa zimetoweka kwa wakati huo.
"Mzee Majenga ni nani kwani?" alijiuliza swali lile, ilikuwa mara ya kwanza kabisa jina lile kuja katika fikra zake lakini alihisi amelisikia sehemu wakati akihangaika katika moto ule.
"Zile shangwe ndani ya lile gunia ina maana ilikuwa ndoto?" alijiuliza huku sasa akiutumia uimara wake wa jeshini kukinyanyua kile kifusi kilichokuwa kimemgandamiza.
Akafanikiwa.
Hamadi! Nyumba yote ilikuwa imeteketea. Kuta zilizoanguka ndizo zilisalia pamoja na bati.
"Nimeponaje mimi" alijiuliza huku akijaribu kusimama wima.
Mguu wake ulikuwa una maumivu makali sana. Kutokana na lile giza hakuweza kuona kilichojiri katika ule mguu.
Akatembea uchi vilevile, akitafuta muafaka wowote usiku ule.
Akaelekea hadi lilipokuwa bomba la maji, akafungua na kunywa maji ya kutosha.
Karibu na bomba palikuwa na kamba ya kuanika nguo. Akachukua nguo ambayo haikuwa yake, kumbukumbu za kuanika nguo zilikuwepo lakini angeutoa wapi muda wa kuitafuta?
Nguo ile ikamvaa lakini hakujali.
Akatoweka eneo lile huku jina Majenga likigoma kukimbia katika kumbukumbu zake.
_______
"KONSTEBO ALIYECHOMEWA NDANI YA NYUMBA, Mengi yamejificha!"
Vichwa vya habari vya magazeti matatu vilisomeka katika namna ya kutatanisha, ni nani ajihusihe na kifo cha konstebo iwe amekufa kifo cha kawaida ama ameuwawa?
Wachache sana, hata makonstebo wenzake wasingejihusisha.
Lakini vichwa hivi vya habari viliwashtua watu watatu kutoka pande tofauti lakini wawili kati yao walizungumza lugha moja huku muhusika wa tatu akiwa katika sintofahamu..
wawili wale walizungumza lugha ya biashara...
Wa kwanza kupagawa alikuwa ni Juma Kimbelembele muhariri wa gazeti la SIRI KALI, alichanganyikiwa kabisa kwa sababu ni yeye pekee aliyejiona ana umiliki wa habari kuhusu kifo cha Konstebo Nguzu kwa kuchomewa ndani huku akikihusisha na masuala ya mapenzi.
Penzi kati ya Konstebo na Inspekta Kobo.
Ajabu sasa anatazama gazeti linaizungumzia habari kwa kuhusisha yaleyale aliyoyaita siri.
Mbaya zaidi siri hii alikuwa ameiuza tayari na pesa ilikuwa ikitembea katika miradi yake mingine.
Upande wa pili, Dokta. Kobo mke wa Inspekta alikuwa anaelekea kurukwa na akili, kwa ajiri ya mume wake na familia kwa ujumla alikuwa ametokwa na pesa nyingi sana kwa ajili ya kumziba mdomo Juma ili asiandike habari zozote juu ya mume wake hasahasa skendo la kuwa kimapenzi na Koplo Zubeda.
Hata siku tatu hazijapita anaziona habari zile.
"Nimetapeliwa au?" alijiuliza akiwa katika chumba cha hoteli aliyojihifadhi mpaka pale ghadhabu zake juu ya mumewe zitakapomalizika. Alihofia kulala kitanda kimoja na mume wake ambaye amemsaliti, aliogopa sana shetani mpenda kifo asije kumwingia kichwani na kumsababisha amdunge mume wake sindano ya sumu.
Aliijua hasira yake hasahasa ambapo mumewe angejaribu kumwongopea zaidi.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi