NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI (3)
Jina: NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI Mtunzi: Nyemo Chilongani SEHEMU YA TATU ILIPOISHIA... Bila kunificha akaniambia kwamba hanipendi, tena nisifikirie kuwa naye hata kidogo. Unadhani niliumia, walaaa! Shamila alikuwa msichana mrembo, kusema kwamba sikustahili hata kutembea naye kwangu mimi ilimaanisha kuwa nitafute pesa, nikipata nimtafute. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Kulipa kisasi kwa Issa ilihitaji nguvu kubwa, haikuwa kirahisi kama ilivyokuwa ikionekana, ilikuwa ni lazima nipambane kuhakikisha napata maisha mazuri kama watu wengine, halafu ndiyo nimfuate. Wanawake waliendelea kufurika Kariakoo , walikuwa wengi mno tena waliokuwa wakipendeza kupit kawaida. Sikuacha kuwasalimia, kila siku niliamini kwamba ili uwapate wanawake wazuri basi hukutakiwa kuwahofia hata kidogo. Siku ziliendelea kukatika, niliendelea kuwasiliana na Aisha na kuonana naye sana. Alinipenda, si kwamba nilikuwa mzuri ni kwa sababu nili…