MAUAJI YA KASISI (12)
Jina: MAUAJI YA KASISI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA KUMI NA MBILI ILIPOISHIA... kisha akayarudisha macho yake na kuyatuliza kule aliko Kamanda Amata na kuendelea kuona kinachojiri, huku akiendelea kunywa kinywaji chake. Mara alihisi, akipapaswa kwa nyuma maeneo ya kiunoni, akageuka na kukutana macho na mwanamke mshumami, aliyejiremba akarembeka, JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... yule mwanamka aliyeonekana ana kila dalili ya ulevi machoni mwake alizunguka na kusimama mbela ya Melchior, akamrembulia macho, Melchior hakuonesha hata kumjali kwani yeye alitaka kujua tu nini kitatokea kule ndani, “Mwanamke unataka nini? Kama kinywaji chukua uende, mi sihitaji mwanamke saa hii,” Melchior alimwambia yule mwanamke, akamnunulia kinywaji kisha kwa akapewa shukrani ya sonyo kali na refu, “Go fish!” yule mwanamke alimwambia Melchior. ˜˜˜ “Bado mnanifuata Kamanda!” Bill alimwambia Amata huku akimimina kinywaji kati…