Notification
Tidak ada notifikasi baru.

MY EVA (1)

JINA: MY EVA
SEHEMU YA KWANZA
Eva alikua ameingia darasani kwa siku yake ya kwanza baada ya kuripot kama mwanafunzi wa kidato cha tano mchepuo wa HGL Katika Kenna high school.

Alipoingia hakuna aliejali ujio wake maana wote walikua wageni hakuna aliekuana na mazoea na mwenzie.alitazama huku na kule akaona kiti kimoja kiko wazi.

Alisogea karibu na kiti kile kisha akavuta na meza iliyo karibu yake akaweka madaftari yake na vifaa vyake vingine akakaa na kushusha pumzi.

Akiwa amekaa mara aliingia kijana mmoja(danny) ambae nae pia alikua mwanafunzi wa darasa hilo..alipoangalia sana akamwona Eva pale kwenye kiti ambacho ni chake yeye

Alisoge pale alipokua Eva kisha akasema:

Danny: wewe mbona umenirithi kabla sijafa?

Eva aligeuka na kumwangalia anaemsemesha kwa sura ya uchovu halafu akanyamaza tu kama hajasikia lolote.

Danny akakasirika kisha akarudia tena kusema:
Danny: we mtoto mbona umekaa kwenye kiti changu?.. Hunisikii au kiburi?.

Eva: nani mtoto?.. Usinifanye nikatalir kwenye kiti hiki hata kama ni chako...alaaaa

Danny kwa hasira akasema:
Danny: nini wewe!!!...ukatalie hapa?..

Eva: ndio kwani inashindikana?

Danny: hahaaaaaah...hunijui wewe.. Nasema utatoka..labda kama sio mimi

Eva: tutaona sasa...sitoki hada kwa bunduki

Danny alikasirika na kumvamia Eva wakaanza kuzichapa....wanafunzi waliingilia kati kuwaachanisha huku wengine wakisema: zichapweee,,,zichapweee tuone nani mshindiiii

Wakiwa bado wanagombana mara aliingia mwalimu jema na wote wakaacha vurugu na kutulia:

Mwalimu: na nyinyi humu mbona kelele sana?.

Wanafunzi wote wakakaa kimya hakuma aliejibu.

Mwalimu: hamna midomo eee...sasa ngoja niagize fimbo na mtanijua mimi ni nani fumbafu nyie.

Baada ya muda viboko vya kutosha vilikua pale,danny kuona hivyo ilibidi aongee.

Danny: mwalimu huyu hapa (huku akimsonta eva) ndo mwanzilishi wa vurugu..amekatalia kiti changu.

Mwalimu: (kwa hasira) wewe,ulikuja na kiti hapa?...

Danny akakaa kimya.

Mwalimu: (huku alimwangalia eva) na wewe ndo umefika leo na kuanza vurugu!!!

Eva aliinama chini kwa woga.

Mwalimu:haya wote acheni hicho kiti mtafute vingine,ole nisikie vurugu tena...alisema mwalimu kisha akaondoka.

Baada ya hapo danny alimwangalia vibaya sana Eva na akasonya "msyuuuuuuu"""

Eva alicheka kwa dharau na kumkasirisha zaid danny.

Danny: (huku akiloloma)yaaan mijitu mingine bwana.

Eva alimpuza na kuendelea na mambo yake kama hakumsikia.

Walitafuta viti na meza mpya wakakaa.

Eva alivyo mkorofi akahama alipokua na kwenda kukaa alipokua amekaa danny.

Danny: (huku akimwangalia eva vibaya) umenifuata hapa tena.

Eva: ulikuja na darasa?

Danny: sawa sitak ugomvi mimi.

Baada ya siku kupita eva na danny walikua wameshazoeana kwakua walikua wakikaa karibu darasani.walitokea kua marafiki wa karibu sana kitendo ambacho kimuuma sana cathy ambae siku zote alitamani kukaa karibu na danny lakin haikua hivyo.

Taratibu walianza kupendana ingawa hakuana aliemtamkia mwenzie wazi.

Eva alikua mrembo sana,halafu alikua mwongeaji sana na mcheshi.alizoeana na wanafunzi wengi hasa wavulana..alikua akitaniana nao mara kwa mara.

Danny alikua akiona wivu sana lakini atafanya nini basi wakati hajawahi kumtamkia Eva.. Inabidi apambane na hali yake tu

Ilikua tarehe 24 ya mwezi wa tisa.siku hii ilikua siku ya visting day(siku ya wazazi na ndugu kuwatembelea watoto wao) pale shuleni.

Tofaut na wanafunzi wengine,eva alikua na huzuni sana,hakua na raha hata kidogo maana alijua hakuna atakae kuja kwa ajili yake maana shangaz yae alikua mgonjwa sana na hakua na ndugu mwingine alikukia akijali kuhusu yeye..

kiwa amekaa mwenyewe mara kuna mtu alikuja kwa nyuma na kumziba kwa macho kwa viganja..eva alijua tu huyo atakua ni danny maana alikua ameshamzoea sana.

Danny alitoa mikono yake na akakaa karibu na eva.. Danny alishtuka kuona akiwa katika hali ile.

Danny: vipi eva, mbona uko hivi?

Eva:hamna kitu danny.

Danny; amekuja nani kwa ajili yako?

Eva:(kwa sura ta huzuni)hamna aliekuja

Danny hakutaka kumuuliza sana kwa muda huo...alimshika mkono na wakaelekea walikokua wamekaa wazazi wa danny.

Danny alifanya hivyo ili kumpumguza mawazo eva.danny alipofika kwa wazaz wake akaanza kumtambulisha eva

Danny: Baba na Mama, huyu anaitwa eva...ni rafiki yangu mkubwa hapa shuleni.

Eva aliwasalimia wazazi wa danny huku akitabasam kwa jinsi danny anavyomjari.

Mama yake alitabasam na kusema: karibu sana mwanangu eva.

Victor alipomwangalia aeva alishtuka sana..mapigo ya moyo wake yalienda mbio sana...alitoka jasho jembamba na sura ikabadilika.

Victor alimfahamu vyema sana eva.

Miaka mingi iliyopita Eva aliwapoteza wazazi wake akiwa bado mdogo sana kwa kilichosemekana kua ajari ya moto lakini haikua hivyo.

victor na wenzake waliujua ukweli na wao ndo waliochoma nyumba ile kwa siri sana na ikaonekana ni ajari.

Wazazi wa eva wote walikufa pamoja na mfanyakazi wao wa ndani..eva peke yake ndie aliepona.

Danny alishangaa kumwona baba yake katika hali ile akaamua kumuuliza:
Baba ..kimetokea nini mbona una mawazo sana?

Victor kwa kujikanyaga kanyaga akajibu:aaah....ha..ha...hamna kitu mwanangu.

Eva, danny na mama yake danny(rachel )wote walikua wakimshangaa victor kwa jinsi alivyobadilika ghafla...NINI KITAFUATA?
HAKIKISHA UMEWEKA SAWA APPLICATION YETU ILI KILA SIKU UPOKEE SIMULIZI ZETU KILA SIKU
KARIBUNI SANA
UKIWA UNAELEKEA KATIKA MUENDELEZO BURUDIKA NA VIDEO HII
featured My Eva Simulizi Z
Jiunge kwenye mazungumzo (2)
Maoni 2
  1. Unknown
    9 Desemba 2019, 01:23
    Profile
    Unknown
    Said: Hey
    Hey