MAMA MWENYE NYUMBA (24)
JINA: MAMA MWENYE NYUMBA Mwandishi: Mbogo Edgar SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE ILIPOISHIA... Mida hii ilimkuta mzee Mashaka akiwa naegesha gar lake mbezi , kwenye bar moja anayo ipenda sana, Full dose pub , akashuka kwenye gari nakwenda ku kaa kwenye ile sehemu anayo ipendaga siku zote, yeye anaita mafichoni SASA ENDELEA... Kisha akaagiza kinywaji na chakula, hii ni baada ya kutoka kwa Suzan alipitiliza mjini kwenye bihashara zake, alipiga mishemishe zake kisha akaingia benk nakuifadhi pesa, kiasi cha Tsh 20 million, kuhusu fedha mzee Mashaka alikuwa ana miliki pesa ya maana, baada yakutoka benk akaelekea kimara akachaua bar moja na kutulia akipiga mtungi, kiukweli ile bar licha ya kukaa kwamda mrefu lakini haikumflahisha maana haikuwa na wahudumu wengi wakike, akaona bora aende zake full dose anawezakuokota chochote, muda wote aliwaza sana juu ya mke wake, jinsi alivyo mjibu kiukaudhu jana usiku, wakati anawaza hayo mala akamwona binti mmoja akija kwenye eneo lile, nakukaameza ya tatu kutoka pale…