MAMA MWENYE NYUMBA (40)

Zephiline F Ezekiel
0
Mwandishi: Mbogo Edgar

SEHEMU YA AROBAINI
Hapo kitendo bila kuchelewa, Sophia aliinuka na kuisogelea ile meza aliyo kuwepo binti wa jana, kisha haraka kama umeme, aliinua chupa ya bia iliyo kuwepo mezani na kumpiga nayo binti wa jana usoni, ika sikika sauti ya puuu!

SASA ENDELEA...
Chupa iki tawanyika vipande vipa na damu zika aanza kumwagika usoni kwa binti wajana, ambae aliachaia kilio chamaana, Sophia hakisubiri akashika njia yake na kuondoka zake, kuanzia mlio wa chupa na kelele za kilio cha binti wajana, zili mfikia mzee Mashaka ambae hakuwa amefika mbali ile kugeuka akamwona binti wajana akiinuka toka chini, mikono usoni huku analia, akuona kitu kingine zaidi ya watu waliokuwa wana sogelea pale alipo kuwepo binti wa jana, hapo mzee Mashaka akakumbuka uwepo wa begi lake la mamillloni pale mezani, akarudi haraka sana kulichukuwa, akimtazama binti wa jana ambae aliendelea kulia akivujwa na damu usoni

Hapo kama hakuwa nae mzee Mashaka akajindoa taratibu akijichanganya na mashuhuda watukio lile, kisha akatoko mea kumwai Suzana akayajenge yaliyo bomoka, kumbe suzan baada yakutoka kule nje, akatembea moja kwa moja mpaka kwenye gari lake akamkuta Edgar akiwa ametulia anacheza game kwenye simu yake, “vipi nishuke?” aliuliza Edgar akitaka kufungua mlango wagari, “hapana hapa hapajakaa vizuri twende turudi kibamba”aliongea Suzan akifungua mlango wa gari na kuingia kwenye gari, akambusu Edgar busu la mdomo kisha akawasha gari na kuondoka, kiukweli Suzan akuonyesha kama kuna tatizo lolote limetokea mle ndani ya full dose, alionekana katika hali yake ya kawaida huku tabasamu ilikishamili usoni kwake

Kiukweli Suzan alijiona kuwa ni mshindi, kwa kitndo cha kumfumania mzee Mashaka kinge muweka huru yeye, kufanya lolote akiwa amesha achana na mzee huyu, huku nyuma Sophia akiwa amejibanza kwenye gari lake alimwona baba yake akiingia kwenye gari lake nakuondoka kwa mwendo wa haraka sana, lkini hakuwa ameliona gari la Suzan, lilikuwa limesha ondoka, mzee Mashaka alikamata uelekeo wa kibamba lengo likiwa ni kwenda moj kwamoja nyumbani kwa Suzan akayamalize na kuyaweka sawa na Suzan, lkini wakati huo hakuelewa kilicho mtokea binti wa jana akapanga kuto tembelea tena ile bar, Sophia yeye aliona amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, akapanga kuwa kesho yake akutane na Suzan amsomee mashitaka yake kisha mpe faini ya malipo ya kumkabidhi Edgar mikononi mwake, hapo alitabasamu menyeweeeeee, kisha akawasha gari na kuelekea nyumbani kwake mbezi kwa msuguri

Njiani Edgar na Suzan waliongea mawili matatu mala sma ika ingia kwenye simu ya Suzan, Suzan akasimamisha gari kwenye kituo cha dala dala na kuifungua, akaisoma kimya kimya huku akicheka, “huyu mtoto mjinga nini” aliongea Suzan huku akicheka na kumtazama Edgar, “vipi ni Sophia nini huyo” aliuliza Edgar na suuzan hakujibu kitu akanyoosha simu kumpatia Edgar, “au mlikutana pale bar maana nilimwona anakukimbilia wakati una ingia ndani,” aliongea tena Edgar huku akipokea simu, “eti Sophia alikuwa anani fwata pale bar?” aliuliza Suzan kwa msangao mkubwa sana “yaaa nilimwona anakufwata mtakuwa mmepishana, ila alikuona” Edgar huku macho yake kwenye simu, hakuona jinsi Suzan alivyo hamaki, “mh! huyu nani tena” aliuliza Edgar akimaanisha yule mtumaji wa sms, akujibiwa akamtazama Suzan huku akimgusa kwenye bega, “eti Suzie huyu monica ndiyo yupi?”

Hapo Suzie alistuka kidogo toka kwenye lindi la mawazo, maana kama Sophia alikuwepo pale kuna uwezekano wakuwa ame sikia kila kitu nakushuhudia jinsi alivyo mfumania baba yake, kwahiyo fumanizi kwenye fumanizi, “niyule tulie kuwa ne mchana pale bar” alijibu Suzan akijitaidi kujiweka sawa, sms ilisomeka hivi “ dada Sizie nitumie namba ya Edgar nichati nae, maana naona nimekosa usingizi kabisa, tena ikiwezekana, mshawishi anitongoze” wote wakacheka kidogo, “hivi Edgar unaweza kunisaliti kwa kutembea na huyu monica?” alongea Suzan akipitisha mkono wake shavuni kwa Edgar, “mama nikuambie kitu,” aliongea Edgar kwasauti tulivu kabisa uku anamwangalia Suzan usoni, suzan akaitikia kwa kichwa, kwamba aambiwe

“Yani kama kuna zambi nilisha wai kuifanya sitokaa nnikutendee kwa sasa, nita kupenda na kwaakika sito kaa niruhusu mtu akukoseshe amani,” hapo Suzan akaachia tabasamu pana huku aki sogeza modomo yake kwenye midomo ya Edgar na kumpiga busu zito sana, “asante mpenzi, asante mungu kwa kunipa mwanamume wa maish yangu” alisema suzani akiendelea kupapasa masavu ya mpezi wake, kisha akaingiza gia na kuanza kuingia barabarani, akisubiri magari mawili matatu yaliyo kuwa yakipita kwa speed, “hooo! gari la boss wako lileeee” alisema Edgar akionyesha gari la mzee Mashaka ambalo lilipita kwa kasi ya hajabu, likielekea upande ambao wao walikuwa wanaenda, ..

Suzan alipo liandagalia lile gari kweli lilikuwa la mzee Mashaka, akajuwa moja kwa moja mzee huyu atakuwa anaelelea nyumbani kwake, sezan akaingiza gari barabarani na kuendelea na safari, safari ambayo iliishia kwenye ile bar, wanayo pendaga sana kupaa chakula kama awajaandaa chakula nyumbani kwao, Suzan akapaki gari sehemu ambayo aliona mzee Mashaka atoweza kuliona gari hilo, kisha wakatafuta sehemu nzuri wakaa na kuagiza chakula navinywaji, kama kawaida yao waliagiza mvinyo mwekundu, huku Edgar akiagiza mchemsho wa samaki, na Suzan akaagiza kuku wa kukuchoma na ndizi, muda wote Suzan aliwaza juu ya Sophia kumfwatilia pale Full Dose, pasipo yeye kumuona

“Inamaanisha Sophia ameshuhudia kila kitu” aliwaza Suzan kabla haja stuliwa na Edgar, “simu yako inaita” hapo Suzan akaitazama simu yake, nikweli ilikuwa inaita, na mpigaji alikuwa mzee Mashaka, Suzan akamtazama usoni Edgar, ambae alikuwa busy na chakula, kisha akakata mlio wa simu na kuiweka simu kwenye mkoba wake, kisha akaendelea na chakula, japo waliendelea kusemeshana na Edgar lakini mawazo ya Suzan yalikuwa mbali sana, maana aliona mda wowote mambo yake yanakuwa azalani, akichukulia kuwa Sophia anatambuwa wazi mausiano yake na Edgar, pia kuna uwezekano, kuwa leo amesha fahamu kuwa anatembea na baba yake, “itabidi nimweleze Edgar, ila sijuwi ata nichukuliaje?”aliwaza Suzan “lakini hakuna namna itabidi nimweleze tu!” aliendelea kuwaza na kuwazua, kabla Edgar ajakatisha mawazo yake

“Suzan nikuambie kitu” Suzan alistuka, utazani labda Edgar alifahamu alicho kuwa anawaza, “niambie tu mume wangu” aliongea Suzan akiidhibiti offu ya ghafla ilito mjia, “yani najishangaa sana, ujuwe kula siku nakuona unazidi kuwa mzuri machoni mwangu, tena unazidi kung’aa mke wangu, najivunia kuwa na wewe” wote wakaachia tabasamu, asa suzan ambae maneno yale yalimliwaza sana, “asante sana, nakupenda pia mume wangu” aliongea Suzan akichukuwa kipande cha nyama kwenye sahani yake na kumlisha mpenzi wake kisha akamalizia kwa busu la shavu, “asante sana mama leo nimesaau kuku lisha” alisema Edgar akichukuwa kipande cha samaki na kumsogezea Suzan mdomoni na Suzan akisogeza mdomo wake ilikupokea mnofu wasamaki

Lakini kabla ata ajaweka mdomoni ghafla Suzan aka jiziba mdomo kizuwia kitu flani ambacho kilitaka kutoka bila iyali yake, kisha akakimbilia chooni haraka sana, huko chooni alikaa kwa dakika kadhaa akitapika, kisha akatoka “pole sana mama, vipi malaria?” Suzan alistuka baada ya kundua kuwa Edgar alimfwata nakumsubiri kwenye mlango wa choo cha kike, “hoooo! kumbe umenifwata, asante kwa kunijali mpenzi” aliongea Suzan wakarudi mezani kwao, ambako Edgar alikuwa ame muomba muhudumu awatazamie meza yao, “samahani Eddy naomba hiyo mcemsho wako huuweke mbali kidogo, yani hiyo arufu imenishinda” aliongea Suzan mala tu baada ya kukaa mezani, “kesho inabidi ukacheki malaria” alishauri Edgar, huku akisogeza sahani yake ya mchemsho wa samaki sato, “haa wapi unazani ni malaria, utakuwa ni uchovu tu!, maana sisikii dalili yoyote ya malaria” aliongea Suzan akichukuwa kipande cha limao na kukilamba kidogo

“Eddy, niombee malimao mengine, yana saidia kukata kichefu chefu” aliongea Suzan akiendelea kulamba kile kipande cha limao, “chukuwa na hiki chakwangu,” aliongea Edgar akimpatia kipande cha limao toka kwenye sahani yake, “hapana bwana icho kitanuka samaki” alikataa Suzan, hapo Edgar akaiuka mwenyewe na kuelekea upande wa jikoni, Suzan akatumia muda huo kuitazama simu yake, ilikuwa na missed call zaidi ya ishilini, na sms mbili, kati ya izo messed call, tatu zilitoka kwa Monica, moja kwa Sophia, na nyingine zote zilitoka kwa mzee Mashaka, akaachana nazo nakufungua sms, yakwanza ilitoka kwa mzee Mashaka, “naomba upokee simu yangu nataka tuongee”

Hapo suzan akapigia kabisa, akatumia dakika moja kuongea na mzee Mashaka, wakipanga kesho wakutane ili waongee kuhusu tukio la leo kule full dose, “nitakuambia mahali pakukutana na muda wa kukutana” aliongea suzan na kukata simu, kisha akafungua sms yapili, ambayo ilitoka kwa Sophia, “mambo best, naona kimya, vipi kesho utakuwepo home?,” japo Sophia aliandika sms iliyoonyesha kuwa yupo kawaida tu! lakini Suzan alisha juwa kuwa kimenuka, “kesho naenda bagamoyo” aliandika Suzan nakuisend ile sms kwenda kwa Sophia, kisha akarudisha simu yake kwenye mkoba, maana Edgar alikuwa anarudi na saani iliyo jaa malimao kibao, kitendo kilicho sababisha Suzan aanze kucheka

Baada ya kumfukuzia Suzan mpaka kibamba na kumkosa, mzee Mashaka akaeudi zake mbezi, aliogopa kupitia Full dose, akanyoosha moja kwa moja mpaka mtaani kwao karibu na nyumbani kwake, ambako ata jana alikuwepo maali pale, aka tlia na kuagiza pombe, alizifakamia kiasi kwamba akajikuta akilewa sana huku mda wote akijaribu kupiga simu kwa Suzan pasipo mafanikio, adi baadae sana ndipo alipoona suzan mwenyewe akimpigia, baada ya kuongea na Suzan kidogo mzee Mashaka moyo wake ulitulia

“Dawa ya kumtuliza huyu mtoto nimoja tu, tena sasa hivi na mtupia fedha ya kutosha kwenye account yake” alisema mzee Mashaka huku akitoa simu yake toka mfukoni, “ngoja kwanza nicheki salio mobile bank” mzee Mashaka alibonyeza simuyake akiingiza namba za kufungua huduma ya kibeki kwenye simu, kisha akafwata taratibu za kuanagalia account yake kuwa ina kiasi gani, alipo lizika na kiasi kilichopo, akafungua begi lake ambalo siku zote uwa ana tembea nalo, akatoa note book na kutafuta namba ya account ya Suzan, kisha akaanza fubonyeza simu yake kufwata utaratibu wa kuamisha salio

Baada ya kukaa sana pale bar Edgar ana Suzan wakainuka na kuelekea nyumbani kwao, safari hii gari aliendesha Edgar, awakuwa wamelewa sana

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA AROBAINI NA MOJA

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)