MAMA MWENYE NYUMBA (42)

Zephiline F Ezekiel
MAMA MWENYE NYUMBA (42)
JINA: MAMA MWENYE NYUMBA Mwandishi: Mbogo Edgar SEHEMU YA AROBAINI NA MBILI ILIPOISHIA... Hapo mke wa bwana kazole akastuka kidogo “ wifi kwanani?” aliuliza hivyo maana yeye anakaka mmoja tu! na kaka mwenyewe ni Edgar SASA ENDELEA... “Tulia basi, utambulishwe, wifi kwa nani kwaniwewe huna kaka?” aliongea mzee Haule wote wakacheka, kisha mama Edgar akaendela, “ni rafiki wa wifi yako wa dar es salaam , anafanya kazi benki ya wananchi pale mjini...” “wifi wa dar yupi?” alidakia tena mke wa bwana kazole, “heee! hivi ujaha tu tabia ya kudandia dandia kwambele, aya jitambulishe mwenyewe basi” aliongea mama Edgar akisusa kuendela na utambulisho, hapo Selina alicheka kidogo,kisha akaendeleza utambulisho,”mimi ni rafiki wa mchunba wa mdogo wako Edgar, anaitwa Suzan , nilisomanae chuo, bahati nzuri yeye amepangiwa hapo hapo dar” utambulisho huo nusu umdondoshe mke wa bwana kazole, maana moja kwa moja, alifahamu chanzo cha fedha inayo wapa jeuri wazazi wake, pia akakumbuka uongo wa mume wake kuwa alimtum…