MAMA MWENYE NYUMBA (42)

Zephiline F Ezekiel
0
Mwandishi: Mbogo Edgar

SEHEMU YA AROBAINI NA MBILI
Hapo mke wa bwana kazole akastuka kidogo “wifi kwanani?” aliuliza hivyo maana yeye anakaka mmoja tu! na kaka mwenyewe ni Edgar

SASA ENDELEA...
“Tulia basi, utambulishwe, wifi kwa nani kwaniwewe huna kaka?” aliongea mzee Haule wote wakacheka, kisha mama Edgar akaendela, “ni rafiki wa wifi yako wa dar es salaam, anafanya kazi benki ya wananchi pale mjini...” “wifi wa dar yupi?” alidakia tena mke wa bwana kazole, “heee! hivi ujaha tu tabia ya kudandia dandia kwambele, aya jitambulishe mwenyewe basi” aliongea mama Edgar akisusa kuendela na utambulisho, hapo Selina alicheka kidogo,kisha akaendeleza utambulisho,”mimi ni rafiki wa mchunba wa mdogo wako Edgar, anaitwa Suzan, nilisomanae chuo, bahati nzuri yeye amepangiwa hapo hapo dar” utambulisho huo nusu umdondoshe mke wa bwana kazole, maana moja kwa moja, alifahamu chanzo cha fedha inayo wapa jeuri wazazi wake, pia akakumbuka uongo wa mume wake kuwa alimtumia Edgar pesa za matumizi, maana ni kipingi kile kile ambacho baba yake aliibiwa simu ya gharama na fedha taslim, na ndizo siku ambazo hakuwai kupokea simu ya mdogo wake, ataakipokea ilikuwa ni matusi kabla haja sikiliza chochote, hapo mke wa bwana kazole akajiona mjinga sana

Ilikuwa saa tau na robo ndio muda ambao mama Sophia alikuwa akisimamisha gari nyumbani kwa mwanae Sophia, alishuka kwenye gari akiwa na shahuku kubwa sana juu ya jambo alilo libaini jana kwenye simu ya mumewe, “yani mtu una mchukulia kama mwanao, anatembea na mume wako” alijiwazia mama Sophia akipiga atua kuufwata mlango wa nyumba ya mwanae “karibu mama” alipokelewa na binti wa kazi, “asante mwanangu ujambo?” alisalimia huku akivua viatu yake vya mikanda ‘sendo’ “sijambo mama za nyumbani?” “hukosalama tu, vipi yupo huyu?, maana atasimu yake aipatikani” aliuliza mama Sophia akiingia ndani, bado yupo chumbani kwake hajatoka toka asubuhi,” alijibu binti wa kazi, na mama sophia akapitiliza sebuleni na kuelekea chumbani kwa mwanae, akausukuma mlango wa chumba cha mwanae nakuingia ndani, alimkuta sophia amelala bado, mezani kuna chupa ya bia ipo nusu na chini vyupa vingi vya bia zilizo tumika

Mama Sophia akajikuta akitikisa kichwwa kwa masikitiko huku anaemdela kutazama madhari ya chumba cha mwanae, ambacho uingia mala chache sana, katia kuangalia angalia, macho yake yalituwa kwenye meza ya vipodozi, ambapo aliona kipande cha limao na vipande viwili vya udongo ule unao uzwa, mmoja ukiwa ume megwa na kubakia kidogo, na pia cheti cha doctor “mh, huyu vipi tena” aliongea mama Sophia akinyoosha mkono kuchukua lile kalatasi la hospital, akalisoma kidogo nauamulia maneno machache, pregnance posteve, “mh inamaana..” hapo mama sophia akatazama tarehe iliyo andikwa kwenyeile card, akajikuta anatabasamu “wewe, mtoto ebu amka” aliongea mama sophia huku ana mtikisa binti yake kitandani, Sophia nae akaamka, akimkuta mama yake mwenye uso wa furaha huku amekamata kile kikaratasi

“Ahsante mungu kwa kunijaria mjukuu karibu naitwa bibi, ongra mwanangu,” alisema mama Sophia huku akinyoosha mikono juu, Sophia alielewa mama yake anamaanisha nini, baada ya dakika kumi natano za Sophia kuoga na kupiga mswaki, walikaa mezani nakuanza kupata supu, nandio mda ambao mama Sophia alitumia kumsimulia mwanae kuhusu mchezo wa baba yake na rafiki yake suzan, ambpo Sophia akamwambia ata yeye amegundua jambo ilo jana, nakupanga kwenda kuongea nae ili ahache mchezo huo mala moja, Sophia na mama yake wakakubaliana hivyo, “henhe niambia mwanangu, uomzigo ni wanani?,” aliuliza mama Sophia uku tabasamu likichanua usoni kwake, “mh! mama nae, yani nikikumbia uwezi kuamini,” alisema Sophia huku akijichekesha, “niambie nimjuwe mkwe huyo, au ni yule wakipindi kileeee, uliniambia nimfanyakazi mwenzio” aliuliza mama sophia akimkumbuka bwana mmoja ambae Sophia aliwai kumtambulisha

“Hapana mama, ni mwanamume wa Suzie,” baada ya kusema hivyo Sophia aliushuhudia uso wa mama yake uki badirika rangi toka kwenye weupe wakawaida na kuwa weupe wa kung’aa, “yupi huyo?” aliuliza kwa hamaki mama sophia, “si yule kijana alie mtambulisha sikuile alisema ni rafiki yake amepanga nyumbani kwake” alisema Sophia hapo mama yake aka ganda kidogo kama anaye shangaa meli ikipita nchi kavu huku akinong’ona, “Edgar” “ndiyo mama, kwani kuna ubaya?” aliuliza Sophia, pasipo kujuwa anacho kiwaza mama yake, kumbe mama Sophia baada ya kumjuwa alie mpatia mwanae mimba, alipata kumbukumbu ya kuwa na yeye anamwezi mmoja haja pata siku zake, hapo Sophia akamshuhudia mama yake akiyumba kama mtu mwenye usingizi au alie lewa pombe kali, na kisha aka anza kwenda chini akiwa hana fahamu, kwakuwa alikuwa nae karibu, Sophia akamdaka na kumkokota pembeni, kisha aka mlaza chini, akimwita mdada wakazi amsaidie

Mzee Mashaka alikuwa kimara akikamilisha mambo ya kibiashara na wafanya biashara ambao walitokea mwanza, baada ya kupewa fedha yake na kuwa taarifu vijana wake waliopo miji wapakize mzigo kwenye gari, ndipo alipo mpigia simu Suzan akimtaka wakutane kama walivyo panga, wakakubariana saa tano asubihi, hapo mzee Mashaka akaamua kusogea mitaa ya luguruni maana akuweza kwenda mbezi Full dose, kutokana na inshu ya jana usiku, ambapo mpaka sasa hakujuwa ni nani alie mtwanga chupa yule mwanamke wake, lakini wakati anajindaa kuondoka, akapigiwa simu na sophia kwa simu ya mama yake, nakupewa taarifa ya mke wake kuzimia, na kwamba wapo hospitari ya Dr Sterah pale mbezi kwa Yusuph, hapo mzee Mashaka aka ghairi kwenda luguruni akaelekea Hopital, ambako alimkuta mke wake ndo kwanza amepata fahamu, na madoctor wakiendelea kumchukuwa vipimo mbali mbali

Huku kibamba mambo yalikuwa bam bam, Edgar na Suzan walikuwa wame kaa Sebuleni wakipata chai, nguo walizovaa sasa ni balaha tupu, wakati Edgar alikuwa ame vaa kibukta kidogo sana Suzan alikuwa ame vaa chupi na sidilia tu! “Edgar utanisindikiza nikamwone mzee Mashaka?” aliuliza Suzan wakati wanaendelea kunywa chai, “tena hapo umeongea la maana, ujuwe ninge jisikia wivu sana ungeenda mwenyewe” alijibu Edgar huku wote wakicheka, “Edgar bwana, akuna lolote mume wangu, nitafanya nini wakati kiu yote unaimaliza” alisema Suzan akichukua kipande cha chapati na kumlisha Edgar, “alafu mume wangu uta nikumbusha malimao, wakati wakurudi” aliongea Suzan wakati huo huo simu yake ikaita, alipo tazama alikuwa Selina, akaipokea

“Niambie wangu za Songea?” alisalimia Suzan, baada ya hapo ikafwatia “ndiyo .... weeee... jamani... sasa imekuwaje ..... ok! poa nita mjulisha... haya wasalimie” aliongea suzan huku usowake ukibadilika kila sekunde, kiasi Edgar akahisi kuna taharifa mbaya huko Songea, “vipi kuna jambo lime tokea Songea?, aliuliza Edgar baada ya Suzan kukata simu, “ni dada yako mkubwa, amepigwa na mume wake” hapo suzan akamwelezea kama wlivyo elezewa, “akome yani anamwende keza huyo mwanamume mpaka anamzarau baba” alisema Edgar akiinuka na kuanza kukusanya sahani pale mezani, “hacha mume wangu, nitatoa” alisema Suzan akimnyang’anya vyombo Edgar, “hapana pumzika maana bado ujakaa sawa” alisema Edgar akielekea jikoni na vyombo mkononi, huku Suzan akimfwata nyuma

“Sijakaa sawa kivipi?” aliuliza Suzan akimkumbatia Edgar kwa nyuma huku wakiendelea kutembea kuelekea jikoni, “ume sahau jana usiku pale bar” alikumbusha Edgar, “mh! ndomaa leo ujanipa, sababu jana nili tapika?” aliuliza Suzan wakati Edgar akiweka vyombo kwenye sink na kuanza kuviosha, “ha! kuna kitu tuliaidiana?” aliuliza Edgar akigeuka kwa mshangao kumtazama Suzan, ambapo alikutana na kikofi cha shavu, “mi staki bwana, si hii hapa” aliongea Suzan akipeleka mkono kwenye dudu ya Edgar na kuibinya kidogo, huku akijiegemeza zaidi mgongonikwa Edgar, hapo kazi ya vyombo ika badirika, na kugeuka inshu nyingine kabisa, kule kule jikoni

Baada ya kujilizisha na hali ya mke wake huku akipewa sababu za kuanguka mkewake nimstuko wakawaida tu, wakati huo Sophia akificha sababu za mama yake kupata mstuko, na kiukweli nayeye alikuwa anahisi tu, kuwa ni kitendo chake cha kutembea na mwanaume wa rafiki yake, mzee Mashaka alimwagiza mwanae Sophia, kumpeleka mama yake nyumbani atakapo ruhusiwa kutoka, kisha yeye akaondoka zake na kuelekea luguruni akipanga kuwai akawai kunywa pia kadhaa ata atakapo kutana Suzan aweze kuongeanae vizuri, ikiwa na kulainisha kwa kumwongeza donge nono, sikuzote mzee huyu aliamini kuwa hakuna mkate mgumu kwenye chai

Bwana kazole leo alichelewa kuamka, kutokana na uchovu wa pombe za jana, anakumbuka jana alikuja na hakumkuta mke wake, na sasa ndio akapata kumbukumbu ya alicho kifanya jana kule bar, akavuta kumbukumbu ya pesa aliyo itumia jana, aka simama na kwenda kuisachi suluali yake, haikuwa na kitu, akajikuta akichoka mpaka miguu, akajikalisha kitandani pwaaa! “nimeumbuka” alijisemea bwana Kazole huku akijikuna kichwa, hapo ikamjia tena kumbukumbu ya kule bar, jinsi alivyo mchapa vibao mke wake, na hawala yake alivyo mtwanga mkewake na chupa kichwani, akakumbuka aliona kama mkewake alikuwa anavuja damu kichwani, “sijuwi hali yake ipoje” alijiuliza bwana Kazole, akapata wazo la kumpigia simu mke wake, akaikamata simu yake na kutafuta namba za mke wake, lakini kabla haja piga akajiuliza kuwa ata mwambia nini amuelewe, maana bado ni mapema sana, aka jiinua kitandani na kuelekea bafuni, wazo likiwa moja tu! kwenda dukani kwa bwana Kalolo, kukopa japo fedha ya kumsaidia kwa siku mbili tatu

Sophia alimpeleka mama yake nyumbani ni baada ya kuwa amesha pata majibu ya vipimo vya mgoniwa ambavyo vilionyesha mgonjwa amesha kuwa sawa, njiani mama Sophia alikuwa kimya kabisa, akione kana mwenye mawazo mengi sana, japo Sophia alijaribu kumweka sawa mama yake, “lakini mama kuna ubaya gani, kwanza yeye Suzan ni mwizi wa waume za watu, na mimi nime paga kumchukua Edgar moja kwamoja,” lakini mama ndo kwanza alitazama nje ya gari kwa kutumia kioo cha mlango wa gari, “ange juwa huyu mshenzi ata asinge ongea upuuzi wake,” alijisemea mama Sophi, safari iliishia nyumbani kwa wazazi wake Sophia, mbezi kwa msakuzi, mama akashuka kwenye gari na nakuingia ndani akimtaka Sophia aondoke mala moja pale nyumbani, kwamba wata tafuta siku ya kuongea juu ya jambo lile, pamoja na kumsisiiza kumletea gari lake, ambalo aliliacha nyumbani kwa Sophia, Sophia aliondoka nyumbani kwao huku njiani maswali mengi yaki mvuruga kichwa chake, maana mama yake ameonekana kustushwa na kitendo cha yeye kupewa mimba na Edgar

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA AROBAINI NA TATU

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)