SEHEMU YA SABA
Basi nikajinyanyua na kwenda chumbani nilipo ingia
Madebe sikumkuta nikajiuliza labda katoka kwenda chooni au dukani tu nikawa nina hofu balaa hata hamu ya kula sikuwa nayo mawazo yakanisonga
usingizi nao ukanichukuwa nikaja kustuka usiku wa manane kucheki pembeni ya kitanda hakuna mtu “Hivi Madebe atakuwa kaenda wapi?"
SASA ENDELEA...
Siku huo kitanda nilikiona kama kina miba basi nikaichukuwa cm yangu na kumpigia Rahmaikawa inaita tu bila kupokelewa nikamcheki
Madebe yeye hapatikani dahaa,
hofu juu ya hofu ikanitanda zaidi nisijuwe nini kitatokea juu yangu
Usiku ulikuwa mrefu sana kwangu mie nikatamani kukuche haraka niweze kujuwa mustakabari mzima wa maisha yangu. Nikaitizama saa ndio kwanza saa tisa
kasorobo kidume nilikuwa natetemeka kama vile kifaranga cha kuku kilicho nyeshewa vua,
Taratibu nikajinyanyua na kutoka zangu nnje, Kitendo cha kutoka tu nikashitukia kama vishindo vya watu wakija eneo lile, Sikuweza kujuwa wala kufahamu ni
watu gani hao ila nikajihami mapema kwa kukimbia na kwenda kujificha sehemu ambayo nilihisi kabisa hawatoweza kuniona. Iwapo wamekuja kwa rengo la
kunifata Mimi, au Madebe nikiwa nimejificha nikaweza kushuhudia kikundi cha watu kama sita hivi wakiwa wameficha sura zao kwa vitambaa usoni mkononi
kila mmoja akiwa na dhana yani,
Nyundo panga chupa nikajikuta natumbua macho tu ghafla nikashitukia nakabwa kwa nyuma huku nikizibwa mdomo nisiweze kupiga kelele nikajikaza kujitoa
wapi nikaisikia sauti ikinisihi nitulie “Salumu kaka ni miee tulia basi, Kumbe alikuwa Madebe akaniachia na kunipa.
“pole sana kaka!"
nikamjibu
“usijali nishapoa,
Akaniambia
“sasa hapa naitaji tucheze mchezo wa kicommando!"
Nikauliza
kwa sauti ya chini
“tuucheze vipi huo mchezo?"
“si umewaona wale maboya wamekuja kwenye kumi na nane zangu, sasa ninacho kihitaji ni kuwafunza adabu maana nishaandaa kikosi cha Maafande watafika
hapa muda si mrefu!"
Nikamuuliza kwa shahuku kubwa ni kweli au?"
“ndio ni kweli ndugu naitaji niwachomeshe tu kisha nitubu dhambi zangu nianze kuswali swala tano zote yani niwe mtu safi kabisa!"
baada Madebe kusema vile akaniambia twenzetu,' tukawa tukinyata kuwanyatia wale vijana wawili waliobaki nnje wengine wameingia chumbani kupiga search
baada kuwafikia tu wote kwa pamoja kila mmoja akamrukia wa kwake na kwenda nae mpaka chini nilijitahidi kwa nguvu zote kumkaba yule jamaa huku
nikivutia hisia jinsi ninavyo sukuma, Mkokoteni wangu pindi ninapo pandishaga kirima jamaa akafurukuta mwisho akawa kimyaa tulicho kifanya baada ya hapo
ni kuvaa magwanda yao na vile vitambaa tukakaa nnje
Tukiwa na sura za ukauzu balaa. Ghafla mlango ukafunguliwa na kutoka wale jamaa wengine na kusema, “Oyaa hawa watoto wa Malaya hawapo humu ndani
sijui wameenda wapi kama vipi tutawatimbia kesho!" baada kusema vile wakatupita ikiwa ishara ya kwamba twenzetuni hawakujuwa kama wanafanya kosa
kubwa sana kitendo cha kutupa migongo tu kila mmoja akaandaa Rungu lake kwa nguvu ya ajabu tukaenda kukita kwenye vichwa vyao, Kila mmoja akayumba
na kwenda chini haraka haraka tukavua yale magwanda punde tu maafande hao.
“kazi nzuri vijana tena ongera sana kwa kuweza kutusaidia kazi ya kuwakamata hawa Nguchiro, ilikuwa kauli ya pongezi kutoka kwa Afande Mark basi, kwanza
wakawapima pumzi isije ikawa tumeuwa nikashusha pumzi baada kuonekana kumbe wazima ila wamezimia tu,
Kesho yake Asubuhi nikiwa dukani kwa mpenzi wangu Rahma kuna jamaa mmoja hivi akaja na kuanza kumsumbua sumbua Rahma kwa kumtongoza wakati
kidume ninae miliki mzigo niko hapohapo.
“sikia binti mi binafsi nimetokea kukupenda nipo tayari kukupa chochote ukitakacho katika maisha yako!"
Rahma akamjibu
“sikia kaka naomba unikome kama ulivyo likoma ziwa la Mama yako kama pesa ninazo mpaka nashindwa kujuwa wapi pa kuziweka!"
“Nenda zako huko Malaya mkubwa tu wewe unazani nani asiyekufahamu ulikuwa unajiuza kule Temeke mwisho,' siku zote mwanaume akitongoza na
kukataliwa utamkuta lazima aponde nikashikwa na hasira kwa kitendo cha mpenzi wangu kuitwa Malaya hata kama ni kweli,
Nikaenda kumkunja yule jamaa nikamtandika kichwa kilicho mfanya abimbilike kwenye ngazi maana tulikuwa juu kidogo nikamshukia chini na kuanza
kumshambulia kwa mateke nikaja kushikwa na Madebe na kunisihi niache binafsi nikabaki kushangaa kwa jinsi Madebe alivyo vaa yani katinga kanzu kubwa
nyeupe na barakashia nzuri mkononi kashika tasbihi na Msahafu, akaniambia
“Salumu kaka huu sio muda wa kufanya matendo ya ajabu ajabu kama haya siku zote Allah (s.w.t) anasema katika Qur'an ya kwamba Na penye chukizo pasi jiepushe,
Ikiwa na maana kufanya hivyo itakuwa ni bora zaidi kwako kuliko ukaingia kwenye maasi wakati Madebe ananihusia hivyo kumbe yule jamaa akaingia ndani ya
gari yake na kutoka na bastora bila kuuliza akafyatua risasi iliyokuwa ikiitaji kunipata mimi, Madebe akaja kukinga ikampata moja kwa moja kwenye tumbo.
Yule jamaa akawasha gari na kukimbia eneo lile nikabaki kuita “Kakaa!"
Kakaa!!! kwa sauti ya chini iliyo ambatana na maumivu Madebe akasema “Salumu mdogo wangu huna haja ya kulia binafsi nakufa kifo cha kishujaa sana angali
nishatubu mazambi yangu Salumu naomba upiganie kuhusu ile Nyumba maana hati niliandika jina lako nilitambua sitoweza kuishi muda mrefu nitakufa tu,
Usijaribu kutaka kulipa kisasi"....
ghafla Madebe akatoa macho na kutulia kimya sikuweza kuamini kama nampoteza kamanda wangu,
Mkombozi wangu wa maisha yangu nililia sana na kuita “Kaka!!!kaka!!!
hakuweza kuamka tena police walifika na kufanya uchunguzi wakaondoka na mwili wa marehemu mkononi mwangu nikabaki na Tasbihi pamoja na Msahafu tu
nikajiapia kama sheria itashindwa kumnasa yule jamaa na kumchukulia hatua nitamnasa mimi nikajivika roho ya kishetani nikakodi boda boda kwenda kituo cha
police niweze kujuwa kinacho endelea taarifa za kifo cha Madebe zilisambaa kama umeme uliokatika ghafra Temeke nzima walistushwa kwa kifo cha mmbabe
huyo sio Temeke tu Tandika Buguruni hadi Mbagara na vitongoji vyake. Watu wakazidi kujazana kuja nyumbani kwenye msiba ule hapo nikaweza kuwaona
ndugu zake feki wakilia kwa uchungu machozi ya kinafiki tu,
Hatimae tukaenda kumzika Madebe kwa heshima zote za dini yetu ya Kiislamu kwenye makaburi ya mtoni mtongani, tokea Madebe azikwe ni siku ya nne sasa
eti ndugu wanajadili mari za marehemu.
“wewe tena usiongee kabisa wakati marehemu yupo hai si ulimfukuza nyumbani kwako kama mmbwa afu leo hii unaitaji ugaiwe gari upati kitu hapa!"
“nani amekwambia sipati nisipopata patachimbika tu!
“kwanza tambueni ya kwamba sisi tunajadili mari tu ila tukae tukitambua ya kwamba marehemu enzi za uhai wake kuna kijana alikuwa anaishi nae kama ndugu
yake ambaye ni yule pale!"
“bwana ee huyo Kijana sisi atatusaidia nini kama aliye mfadhili kuishi keshaondoka kama vipi amfate kaburini"
sio siri maneno aliyokuwa akiyatamka Dada yule yakazidi kuuchoma moyo wangu ila nikapiga moyo konde tu nisije kutenda kitu cha ajabu, wakaulizana “sasa
naona tunapanga tu kugawana mali je Hati miriki nani anazo?" kila mmoja akanigeukia mimi yule Dada mwenye maneno ya Nyodo akaniuliza “wewe mbwa tunaomba utupatie Hati miriki zote!"
Nikainuka pale nilipokuwa nimekaa nikiitaji kwenda kumfumua zinga la teke yule Dada nikakumbuka aya aliyo nisomea Marehemu kabla hajafa nikashusha
hasira na kuwaambia hivi “binafsi hakuna hata mmoja wenu ninae mtambua hapa sasa basi Hati zote ziko katika mikono yangu na mimi ndio mrithi halali wa
mali hizi.
Nyie toeni mimacho tu binafsi alicho kizungumza huyu Mama ni ukweli mtupu ya kwamba lazima mnishilikishe mimi!"
Yule Dada akasema
“nadhani wewe kijana unijui sio sasa nakupa masaa 24 tu uwe tayali ushatoa Hati zote vinginevyo utakufa siku si zako!"
kwa nnje nikamuona yule Bibi muokota machupa ya maji akiniita nikatoka kwenda kumfata,
“Shikamoo Bibi!"
“marhabaa Baba yangu kwanza pole sana kwa kufiwa na ndugu yako!"
Hasante Bibi nishapoa ukizingatia wote njia yetu ni moja tu mbele yake nyuma yetu!"
“Ni kweli kijana ila jiandae na vita vilivyoko mbele yako ni vizito sana, “Bibi unasema!?
“ni ukweli mtupu ninao kwambia yule binti mwenye kidomo domo ni Mchawi mwanga mkubwa tu usipokuwa makini atakupoteza ila kwakuwa mi nipo
nitakusaidia usijali!" baada Bibi yule kusema maneno yale akaondoka zake huku akiokota makopo tu nikarudi na kukuta mzozo tu,
Zile vurugu hazikuweza kunitisha kwa chochote kile. Nikabaki kuwatizama tu jinsi wanavyo tukanana.
Kisa mali za marehemu dahaa,
“Ndio nishasema vyovyote itakavyo kuwa na iwe tu zile gari tatu ni za kwangu mimi!"
“wee tena ishia hapohapo yani uchukuwe gari zote tatu peke yako alafu sie wengine tugawane nini?"
“hilo mtajuwa nyie wenyewe nikiwa kama mtoto wa kiume na Kaka wa marehemu nastahiri kuchukuwa kila kitu!"
“endelea kujidanganya hivyo hivyo eti mtoto wakiume kama kidume kweli uliye kamilika utachukua ila nikiwa kama Mwanamke ninaye jielewa tena
nasimamisha kama unavyo simamisha wewe Yale magari tunagawana!"
Wakazidi kuzozana tu mpaka kufikia hatua ya kurushiana makonde dahaa aibu hii jamani ndio kwaanza. Marehemu kazikwa siku si nyingi kidonda kwenye moyo
wangu kikiwa bado kibichi nawaona ndugu zake sijui feki au original wana dundana.
Nilicho kifanya ni kuingia chumbani na kuchukua panga nikatoka nalo kwa kasi ya ajabu na kupangusa ukutani huku nikipandisha sauti
“kila mmoja atoke apotee ndani ya nyumba hii.
Wakataharuki na kuanza kukimbizana yule aliyekuwa anataka magari matatu akawa mbishi kutoka akasema “wee boya acha kunitishia panga Niko hapa kudai haki yangu siogopi kitu!"
Ahaa kumbe aogopi ehee kwa kasi ya ajabu nikamtandika panga la mgongo ila nilitumia ubapa akapiga yowe la. Uchungu.
“jamani nakufaa akatoka mbio mpaka nnje nikawa namkimbiza wale ndugu wengine wakajuwa kumbe jamaa hatanii kila mmoja akatokomea zake na kuahidi
kunionyesha si najifanya mjanja nitaona tu.
Baada kupita siku kama tatu hivi tokea tukio la kuwatimua wale ndugu nikaanza kuotaota ndoto za ajabu usiku some time nakula mavi au nyama mbichi za
binaadamu nikiamka Asubuhi nakuwa nimechoka vibaya mno naweza nikawa nimelala upande huu wa kitanda nikija kushituka Niko chini ya kitanda au
uvunguni kabisa.
Nikaitaji kumtafuta Bibi baada kufahamu vita ndio vimeanza hivyo.
Hakika nilianza kuwa mnyonge sana, furaha sikuwa nayo
kabisa, Rahma akajitahidi kuniuliza nini tatizo sikuwa na jibu la kumpa.
“Salumu kipenzi changu mbona umeanza kukonda ghafla,
Au ndio kumuwaza ndugu yako
Madebe?"
Nilimtizama Rahma huku nikiwa nimeshika tama"......
akaniuliza tena,
“Sasa baby ukikaa kimya utakuwa unitendei haki niambie nini tatizo
Ehee!"
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA NANE
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com