MZOA TAKA (8)

0

JINA: MZOA TAKA
Mwandishi: Hafidhi J Ikram

SEHEMU YA NANE
Nilimtizama Rahma huku nikiwa nimeshika tama"......
akaniuliza tena,

“Sasa baby ukikaa kimya utakuwa unitendei haki niambie nini tatizo
Ehee!"

SASA ENDELEA...
Akakishika kichwa changu kwa mikono yake miwili, mikono
rainii kisha akakiegemeza kichwa changu kifuani kwake.
Utasema mtoto ambaye anataka kunyonya"......
Nikajikunyata maana Rahma
ndio mwenye kunipa faraja kwa matatizo haya yanayo nisibu,
Washikaji nao hawakuacha
kunipa moyo na kuahidi watakuwa bega kwa bega pamoja nami katika vita hivi,
Siku hiyo nikiwa nafua nguo zangu nikiwa sina hili wala lile nikahisi kama mlango wa chumbani umefunguliwa na mtu kuingia ndani nikaacha kufua na kuingia

ndani kwa kunyata ajabu sikuweza kuona mtu. Nikasonya na kutoka zangu nnje ajabu nikamkuta Bibi kakaa kwenye kisturi nilipo muona nikafurahi sana.

Shikamoo Bibi!"
“marhabaa mjukuu wangu kijana wangu mwenzako wiki hii yote nilikuwa naumwa kutwa kucha nipo ndani nikashindwa hata kujinyanyua niweze kutoka nnje!"
“Dahaa pole sana Bibi yangu unaumwa nini?"

“Maralia ndio inayo nisumbua unionapo sijala chochote tokea juzi naishia kunywa maji tu!"
“Duhuu pole sana lakini hospital si umeenda au umemeza dawa tu?"
“mmh! uwezo tu wakununua chakula sina nitawezaje kwenda hospital au kununua dawa nilikata mualuvera nikaukamua nikanywa!"
Binafsi ni kweli Bibi hakuwa katika hali nzuri kihafya nikaingia ndani na kuandaa chai baada kuandaa kila kitu nikamkaribisha aweze kunywa chai akaingia ila

nikamsikia kama ameguna hivi kisha akasonya.
Nikataka kumuuliza ila nikanyamaza nisije kuzua mambo yasio nihusu.
Nikaenda nnje kuendelea kufua dakika kama tano hivi nikasikia ananiita.
"Wee Salumu"
Nikaenda kumsikiliza anasemaje baada kufika akaniambia kitu ambacho kilinistua sana

“Salumu mjukuu wangu ni kheri uishi makaburini kuliko ndani ya nyumba hii!"
“kwa nini bibi unasema hivyo?
“Siku zote usilolijuwa ni sawa na usiku wa Giza binafsi ndugu wa marehemu washaanza kukutupia makombora mazito mazito nia yao ni kukupoteza kabisa

hapa duniani. Ndani ya nyumba hii kuna vitu vya ajabu ajabu tu kinacho wazuia wao kukuondoa haraka ni kile kitabu.
Nikaangalia hiko kitabu anacho nionyeshea Bibi kumbe ni msahafu japo msikitini siendi kuswali ila kusoma Qur'an nakumbuka.
Bibi akaendelea kusema usipokuwa makini na hiki ninacho kuambia utaona matokeo yake ushaanza kulishwa vitu vya ajabu ajabu usiku.
Wakati Bibi anaongea yote hayo Mimi mwili unatetemeka vibaya mno nikahisi baridi maana kumbe nyumba haifai hii.
“Usiogope Salumu kumbuka wewe ni mtoto wa kiume utakiwi kuwa hivyo jikaze pambana naimani utashinda tu!"

“sasa bibi nitapambana vipi wakati sijui wapi pakuanzia na sina fani yoyote ya uchawi mie!"
Nilizungumza hivyo huku mchozi ukinitoka binafsi asikwambie mtu uchawi unatisha vibaya mno utakuta unabebwa kitandani usiku pasipo kujitambua ukaenda

kulimishwa ukiamka Asubuhi umechokaa mwili wote unauma hapana chezea mchawi.
Bibi akanistua kutoka katika dimbwi zito la mawazo kwa kuniambia.
Embu twende nyumbani kwangu nikakupe kitu ambacho kitawakomesha hawa wajinga wote!
Tukaongozana hadi nyumbani kwake ni kijumba kidogo hivi kilicho jengwa kwa kugandika udongo juu kaezeka makuti tu nikajiuliza hivi inapo nyesha vua iliyo

ambatana na upepo mkari huyu Bibi analala kweli. Akaniambia niingie ndani nikawa naogopa ila nikaingia nikiwa na hofu tele moyoni.
Niliweza kukitasimini kile chumba pembeni kuna kitanda cha kamba juu kimewekewa mabox tu. Nikazidi kushangaa shangaa tu.
“Mmh naona unashangaa mjukuu wangu hapa ndio nyumbani kwangu ninapo egemeza ubavu wangu. Kaa hapa wala usiogope!"
“hivi Bibi kwa nini unaishi maisha ya tabu hivi"..... hukuzaa au huna watoto ndugu jamaa marafiki wote hao wamekuacha uteseke kwa nini Bibi?"
Niliuliza maswali kwa mkupuo
Akaniambia
“Salumu kumbuka nilikwambia jambo usilo lijuwa ni sawa na usiku wa Giza kwanza kabisa ni story ndefu kidogo nahisi nikianza kukusimulia unaweza kulia

kabisa watoto ninao ndugu ninao tena kama ushawai kusikia jina la Wahida Tarq?
“ndio nishawai kumsikia hadi kumuona kwenye TV akizitangaza kampuni zake ni mmoja kati ya matajili hapa Nchini anamiliki viwanda maduka na mabasi ya

mikoani kibao tu!"
“Basi huyo Wahidi ni mmoja kati ya watoto wangu wanne niliowazaa kwa uchungu nikateseka miezi Tisa"...
Nikastuka na kuuliza Bibi unasema?"

“ndio huwezi kuamini kwa hiki nikwambiacho ila embu kaa hapa nikupake dawa kisha nikupe story ilikuwaje mpaka nikawa hivi"...

Nilikaa vizuri ili niweze kupata history ya Bibi. Akaanza kusema
“Kwajina naitwa Asma Salehe ni mtoto wa kwanza kuzaliwa kati ya watoto sita wa Mzee salehe na bibie Zulfa.
Nilizaliwa huko mkoani
Dodoma kusema kweli maisha kwetu yalikuwa mazuri sana hatukuweza kuijuwa nini shida
Wala tabu na mateso tulikula
kulala na kuvaa vizuri wazazi wangu wakatokea kunipenda Mimi kuliko wenzangu sikuweza kujuwa sababu hasa ni nini.
Nakumbuka tukio moja
Siku hiyo nilikuwa natoka shule
Nikakutana na kijana mmoja akaniita
nilitaka kumpuuza ni kheli ningefanya hivyo kuliko kuitikia wito wake
Msemo wa kubali wito kataa maneno ndio ulioniponza Asma Mimi nikaenda kumsikiliza yule kijana baada kufika
Ghafla nikajikuta nazibwa kwa nyuma. Nilijitahidi kujitoa nikashindwa
nikaanza kuona Giza totoro mbele
yangu sikujuwa nini kilicho endelea.
Nikaja kustuka na kuhisi maumivu
kila maeneo ya mwili
wangu hasa sehemu zangu za siri
nyuma na mbele macho nilifumbua kwa shida sana nilikuwa
nimefungwa kamba mikononi sikujuwa hapo nilipo ni
wapi na kwanini nimetendewa unyama kama huu nikajitahidi kupiga kelele kuomba msaada sauti haikutoka
damu zikawa zinanitoka sehemu za mbele bila shaka nimebakwa
na kutolewa bikira yangu nililia sana mpaka machozi yalikauka hakuna wa kunisaidia.
Nilikata tamaa nikajuwa ndio basi tena
Asma mimi nakufa bila kukamilisha ndoto zangu za siku moja kuwa mwana Shelia wa kujitegemea
Nikiwa nimejiinamia nikahisi kama mtu hivi kaingia kwenye kile chumba
nilicho fungiwa.
Nikainua uso wangu nikastuka kwa kile nilicho kiona mbele ya upeo wa macho yangu. Nilimuona binti
mmoja hivi akiwa kanisimamia
mkononi kashika kisu akaja mbiombio
na kukata kamba nilizofungwa akaniambia.
“fanya haraka ukimbie kabla Kaka hajarudi kutoka kazini!"
Kuna kitu niliitaji kumuuliza ila sikuweza kutamka
chochote akanisaidia kuninyanyua
nikajikaza hivyo hivyo japo
nilikuwa na maumivu kila mahali
kwa mwendo wa kuchechemea nikapiga hatua huku mabonde ya damu yakinimwagika"
“Salumu siwezi siwezi kuendelea naumia sana moyoni mwangu!"

Huku machozi yakimtoka Bibi akaniambia hivyo. Nikamfuta machozi na kumwambia pole sana!"
Akaitikia “Asante"
Akaendelea kusimulia
“Basi nikajitahidi kutembea huku nikitafuta njia ya kuelekea nyumbani hatimae nikafika nyumbani. Mama na ndugu zangu wengine waliponiona wakaja mbio

mbio nikadondoka chini na kupoteza fahamu.
Nikaja kustuka na kujikuta niko hospitali nimelazwa huku nimetundikiwa dripu ya damu nikatizama kushoto kwangu nikamuona Mama nikafumbua mdomo

wangu na kumwita.
“Mama"
akainua kichwa chake na kuja kitandani haraka huku akiniuliza
“Asma mwanangu uu mzima?"

Nimjibu nini zaidi ya kulia tu.
Siku wiki miezi ikatimia hafya yangu ikatengemaa huku police wakiwa tayari washamnasa mtuhumiwa
Kesi ikawa ipo mahakamani
Nikiwa najiandaa kufanya mitihani ya kumaliza form four
Shuleni kwetu kuna kawaida ya kupimwa mikojo kila baada ya miezi sita basi sikuwa na hili wala lile nikapeleka mkojo wangu
Majibu yakatangazwa tena mbele ya wanafunzi wote sikuamini pale Headmaster aliposema wanafunzi kama nane au tisa hivi wameitia aibu shule hii kwa kubeba

mimba pasipo kumaliza masomo yao"....
Akaanza kutaja majina
Wakwanza ni Faudhia Eva Prisca Pendo Asma. Nikastuka
kwani kila jina unatajwa na mzazi wako nguvu zikaniishia miguu ikawa mizito nikaona kizunguzungu nikaenda chini kwa Mara nyingine nikapoteza fahamu
Nikaja kuzinduka nikiwa mikononi mwa Mama akiwa analia
Baba akiwa pembeni kajiinamia baada kugundua nimeweza kurudisha fahamu zangu akanyanyuka na kuanza kufoka kwa hasira
“Wee nyau pusi kenge blue Malaya mkubwa yani Mimi napoteza pesa zangu kukusomesha wewe leo hii unakuja kunitia aibu katika familia yangu kwa kubeba ujauzito!"

Nitamjibu nini Baba zaidi ya kubaki kimya tu ndio ana haki ya kuongea hivyo ila atambuwe mwanae nilibakwa mie!"

Akaingia ndani punde tu akatoka na begi langu.
Akanitupia huku akizidi kuongea
“Sasa kuanzia leo sitaki kukuona ndani ya nyumba yangu nenda kwahuyo aliyekupa mimba shenzi zako!"
Mama akaingilia kati na kuanza kunitetea.

“Hivi wewe Mwanaume unaakili kweri yani unajuwa kabisa binti yetu alibakwa ndio kimepelekea kushika mimba afu wewe na bange zako unataka kumfukuza

mtoto!"

“Nishasema sitaki kumuona ndani ya nyumba hii icho kisingizio cha kubakwa Mimi sikijui usikute ana Wanaume zake huko ndio wamempa hicho kitumbo

kisingizio kabakwa
Naingia ndani nikitoka nisikukute
wee Malaya
Machozi yakanitoka. Mama nae akajitahidi kunitetea ghafla Baba akatoka na panga nikatoka mbio na begi langu nikaamua kwenda kwa Shangazi nae akanitimua

kwa
madai ya kwamba asije akakatwa kichwa na Baba.
Nikaenda kwa shogaangu Zurekha nikashukuru baada kunipokea vizuri tu nikawa naishi hapo kwao wazazi wake wakatokea kunipenda na kunijali kwa kila kitu

hasa Baba yake Zulekha
Kuna siku alikuja mgeni ni Mwanamama mtu mzima hivi Zulekha aliniambia ni Mama yake mdogo basi akaonekana kunifurahia mwishoe akaniomba aondoke

na Mimi kwenda jijini Dar es salaam.
Sikuwa na jinsi zaidi ya kukubali tu
Baada siku kazaa nikawa nipo ndani ya jiji hili maeneo ya Kawe ukwamani
Nikapokelewa vizuri na familia yake
Nikiwa kama mwanae wa kunizaa vile
Nikaweza kupata marafiki wengi tu huku kitumbo changu kikiendelea kukua
Nakumbuka siku moja usiku nikiwa nimelala ghafla nikahisi kama vile kuna mtu ananishika shika nikafumbua macho yangu taratiibu hamadi ni Baba mwenye

nyumba tena akiwa uchi wa mnyama akijiandaa kuniingilia
Nikastuka na kupiga kelele akaniziba mdomo nikamng'ata
ajabu taa ikawashwa nikamuona yule Mama akiwa kashika mwiko
Na kuja kunitandika nao huku mumewe akiniacha napigwa yeye akaondoka kwa kicheko
Kumbe siku zote akufukuzae akwambii toka atakufanyia visa tu
Nikafukuzwa kama mbwa usiku wa manane Asma nililia sana sikujuwa wala kufahamu Usiku kama huu nitaenda wapi
Nikafikia hatua ya kukufuru kwa kulaani kwa nini nimezaliwa
Nimeletwa duniani kuja kuteseka why?
Mpaka kufikia hapo story ya Bibi ikanitoa machozi nikampa pole kwa mitihani aliyo pitia.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA TISA

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)