TUPEANE (10)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA KUMI
Nikakaa akaja kunikalia mmh mkomboti wangu ukaanza kupiga stata kila dakika inavyo yoyoma mimi nazidi kuwa hoi taabani hasa gari ikipita kwenye vishimo au matuta hivi ikidunda binti akawa anapetwa petwa na kujikuta anazidi kulikandamiza dudu langu mpaka likatamani kuchana zipu afakamie pangoSASA ENDELEA...
Ghafla buss
likafunga break huku abilia wakipiga kelele
tunakufaa!!!!!
wengine Mungu wangu!!!!! weee
Kitendo cha buss kufunga break gafla mpaka watu tukayumba yumba na kujikuta mimi na yule binti tukigusana lipsi zetu maana alinikumbatia asiweze kudondoka vilio vikasikika “tunakufa!!! eee Mungu baba!!!
maana buss likawa linayumba tu, nikazidi kukumbatiana na yule binti wakati nilitakiwa nitoe msaada mwisho gari ikasimama yani ile break ilikuwa kama ya trean kila mmoja akavuta pumzi zito kwa kuweza kunusulika kwa ajali ile pasipo kufahamu nini chanzo yule binti baada kutoka maungoni mwangu ndipo nikapata ufahamu ahaa kumbe namlinda mama,
nikanyanyuka faster na kumcheki mama si nikakuta siti aliyokaa ipo tupu khaa! nikanyanyuka nikiwa nishadata na kucheki dirishani nikapumua kidogo opsii, baada kumuona mama akiwa na baazi ya abilia wameshuka wakiwa wanaenda mbele sijui kufanya nini?
nikatupa macho vizuri na kuona kama mtoto hivi akiwa amelala barabarani huku damu zikimvuja kwa kitendo cha faster nikapima darubini yangu ya
macho nikagundua kumbe
yule ni mtoto ndio ila kategwa
pale awe kama chambo tu,
nikajikuta nasema “hapana!!!
msimguse huyo mtoto rudini tuondoke haraka sana!!!
kila mmoja akageuka kucheki kule
sauti yangu inapotokea kabra hawajafanya
chochote wakajikuta wamezungukwa
na kikundi cha maninja sema maninja hawa mikononi
wamebeba SMG na mapanga wakaja kulizunguka buss
na kujikuta wale walioshuka na na sisi tuliobaki kwenye gari tukiwekwa
chini ya ulinzi,
binafsi sikutaka kufanya chochote
nikahitaji kuona nini watatufanyia
majambaika haya,
mmoja wao akaamrisha kwa sauti ya kibesi “shuka!!!shuka!!! nyinyi panya buku kenge blue!
yani ukileta ubishi unapigwa panga moja tu kwa kutumia ubapa nikashuka huku nikiwa nimeweka mikono kichwani
tukaamrishwa tusonge mbele kwa kuingia porini “tembea wewe acha kutizama nyuma tukazidi kusongeshwa mbele zaidi nikawa najiuliza wanatupeleka wapi na je lile buss si litakutwa pale barabarani au?"
safari ikawa ndefu kidogo hatimae tukajikuta tunaingia kwenye kambi yao kuna watu wana sura ngumuu baada kufika tu kuna jamaa mmoja akaja mbio na kumnyanyua yule binti mwingine akaja kumnyanyua mama nikaweza kufahamu wanaenda kubakwa
dadeki umbake mama yangu Mimi
ogopa sana hii ikawa purukushani kwa kila mwanamke aliye bebwa, “niachee stakii!!! niacheni!!!!
nikacheza show moja ya kibabe zaidi
kwa kumshika ninja mmoja nikamtupa mbaali akaenda kujibamiza kwenye ukuta na kupasuka vipande vibande
yule jamaa ambaye alikuwa
analeta ubishi kwa kumkalia yule binti
kwenye gari ndio akaonekana
yeye ndio kafanya kitendo mile
ajabu hii kitendo bile kuchelewa wakamzunguka na kuanza kumtika mapanga amini usiamini jamaa akawa na nguvu za ajabu sana na kujitahidi kupambana mwisho akachoka na kupiga goti chini damu chapachapa “ili iwe fundisho kwa majinga kama hawa kila atakaye jaribu kupambana nasi lazima au mie kwakuwa kamuua mwenzetu nae hana budi kufa, ni moja kati ya maneno kati ya wale maninja,
jambia likainuliwa juu kwa ajili ya jamaa kuchinjwa nikainuka faster na kwenda kumpushi yule mchinjaji yani nae akarushwa mbaali na kupasuka vipande vipande hapo sasa ikawa ngoma inogire wakanizunguka mimi kumbuka wakati wa uhai wangu kupambana hivi ni kitu cha kawaida kwangu
ila sasa nimechanganya na nguvu za kuzimu ni sawa na kunywa maji tu
kuna wakanivamia basi kila alienigusa kwa upanga au jambia akajikuta anajichinja mwenyewe au kujichomeka nalo tumboni nikawasha moto zaidi kwa kuwatemea cheche za moto, nayafanya yote hayo nikiwa nishawapa hali ya sitofahamu abilia wote wasiweze kuona kama natumia nguvu za kijini wao wakawa wakiona napambana kiume tu ndani ya dakika kama kumi hivi kila kitu kikawa shwali
kila mtu alinipa pongezi kwa kazi nzuri niliyo ifanya tukaongozana kurudi kwenye buss cha ajabu pale tulipo liacha halipo sasa limepelekwa wapi?
ni swali ambalo kila mtu akabaki kujiuliza na kukosa majibu tukaanza kulisaka kwa kufata hatua za matair ya gari kwa bahati nzuri tukaliona deleva akapanda na kuchochea moto kila mmoja akaomba dua kwa imani yake maana dahaa
majanga matupu yule kijana aliyetaka kuchinjwa kusema kweli damu nyingi sana zilimvuja kuepusha asije weza kufa kwa kupoteza damu zaidi nikajifanya kutoa dawa flani hivi ndani ya begi nikaanza kumpaka paka haikuwa dawa ya kawaida bali ni kitu kutoka kuzimu ikawa inaziba majeraha na kuirudisha damu yake kimtindo tu
baada kumfanyia vile nikamuacha apumzike kwenye kiti akiwa hajitambui kabisa nikamcheki mama nae akanitizama na kutabasamu kila abilia alikuwa na furaha
buss baada kufika kimanzi chana ikabidi tumuwahishe jamaa hospital tukatoa maelekezo kituo cha police kitendo bila kuchelewa wakapanda kwenye defender zao na kuelekea eneo la tukio baada ya hapo tukaingia kwenye gari safari ya kwenda mjini ikaendelea mpaka tunafika mbagala rangi tatu yapata saa kumi na moja jioni kila mmoja abilia wote tukashuka nikabaki kushanga shangaa jiji la dar es salaam jiji la gharama watu wake hawaishi kulalama ukishindwa utahama,
nikiwa bado natafakar niende wapi wakati nimekuja kumrinda mama nikaja kuguswa begani nikageuka ni yule binti “mambo?"
poa tu niambie naona ndio tunaachana hapa,
ndio hivyo kwanza ningependa kufahamiana nawe mi kwa jina naitwa Swahumu naishi yombo vituka sijui wewe mwenzangu?"
“mmh! mimi naitwa geofrey naishi ilala bungoni, “ohoo una jina zuri sana kama ulivyo wewe mwenyewe, “silishindi jina lako nikiwa bado naongea na yule binti nikaweza kumuona mama anagombania kupanda daradara kama ujuavyo mbagala time za hasubuhi na jioni shida
tupu nikastuka baada kumuona
kijana mmoja hivi akichomoa kitu kutoka kwenye kipochi cha mama nikafahamu bila shaka ile ni simu tu
nikanyoosha kidole kumstua mama ya kwamba unaibiwa akageuka kama jinamizi vile na kumkwida yule kibaka na kuanza kumtia makofi huku akimuitia kelele za mwizi na laiya wa sasa hivi town hawana dogo wakamuungia tera na kuanza kumshushia kipondo moyoni nikaingiwa na huruma baada kuona jinsi kijana yule anavyo pigwa na siraha za kila aina kuna mwanamama akatoka mbiio huku akipaza sauti kwa kusema “pisheni!!! pisheni!!! watu wakapisha mkononi kabeba kalai la mafuta ya moto akaja kummiminia yule mwizi dahaa
ni maumivu kwa kiasi gani anayo yapata akawa anababuka kila maeneo ya mwili wake kama haitoshi wakamvisha pira na kummiminia petror kibiriti kikawashwa na kutupiwa yule mwizi akawa anawaka moto nikahisi maumivu makali sana moyoni mwangu kwa jinsi yule mwizi anavyo piga kelele ndio ni mwizi je adhabu aliyo pewa anastahili kufanyiwa hivyo nikaona hapana!
nikanyoosha mikono juu na kuishusha vua kubwa ya mawe ikiambatana na upepo mkali watu wakaanza kukimbizana huku na kule nikajifanya na mimi kwenda kujibanza kwenye kiduka flani hivi na kuona kila mmoja anachezea cm yake
“hallo!! kaka vipi huko buguruni vua inanyesha au?" akajibiwa upande wa pili hapana huku pako shwari tu hata wingu hakuna, “ee bwana ee huku mbagala kuna bonge la vua ya mawe,
nikamtizama mama
simuoni kumbe kashapanda gari na kuondoka zake nikacheki kwenye kiganja cha mkono
niweze kufahamu je kwa sasa yuko wapi kucheki nikastuka baada kuona siti aliyo kaa mama kuna mtu pembeni yake si kiumbe cha kawaida nikaizima ile vua na kumpoteza yule mwizi kimazingara nikatoka mbio mpaka kwa madereva boda boda na kumwambia je anaweza kuniwahisha kinondoni mkwajuni maana ndio sehemu wanapo ishi wazazi wangu nikaitaji kuwai kabra kile kiumbe hakijafika ndani ya nyumba hiyo,
“Oyaaa kimbiza pikipiki hiyo mbona speed ndogo hivyo, “ahaa brother hii sio ndege bwana mbona tuko mwendo kasi hapa, binafsi nikawa na kitete sana moyoni mwangu hakuna kitu kibaya kama kumruhusu yule jinamizi aweze kuingia kwenye nyumba ya wazazi wangu kwani itakuwa hatari kuliko moto wa petroleum japo speed ya boda boda ilikuwa kubwa kwangu niliona kama mkokoteni tu,
nikajikuta namwambia yule kijana wa pikipiki “kama huwezi kuendeesha kwa speed nikabizi mimi, akafunga break na kunitizama kwa macho yake mekundu bila shaka atakuwa anavuta bange nikajisemea moyoni nikizubaa hapa na huyu bwege nitamkosa mama,
nikafanya tukio ambalo hata yule kijana hakuamini baada kumsukumiza na kuondoka na pikipiki kuna baazi ya madereva wa pikipiki wakaniungia tera kwa kunikimbiza kusema kweli kila nikichochea moto nao hao, kufika ilala boma kuna msururu wa magari yani hiyo foreni si yakitoto kibaya zaidi upande ninao tokea mimi huku uwanja wa taifa kitendo cha faster nikachenji pikipiki na kuichukua yangu, kama ushawai kuicheki muvi flani hivi ya jann dushman ni yaki hindi utakuwa umenipata hiyo pikipiki imetokaje nikapita kama upepo trafik akaruka kama kule na kuacha hali ya mshangao maeneo yale,
mpaka nafika magomeni hospital sikuweza kuliona gari alilo panda mama nikacheki kwenye dira yangu kumbe lipo mbele yangu tu nikamcheki mama kwenye ile gari hayupo khaii nikazidi kuscani niweze kumsaka hii kumbe yupo kwenye bajaji,
mbona majanga nikaja kutambua yule jinamizi kashamuingia mama mwilini anamperekesha anavyo taka yeye ndio kamsurutisha ashuke kwenye coaster apande bajaji ili wawai mapema wakati some time bajaji inakaa katika foreni nikaifikia ile bajaji,
nikaweza kuifikia ile bajaji nikawa nayo beneti zaidi huku nikimtupia jicho mama akiwa anasinzia sinzia nikapata akili ya kwamba niwai mimi kufika nyumbani kwa wazazi wangu nikaipita ile bajaji na kuzidi kusonga mbele zaidi nikafika kinondoni mkwajuni sikupata shida kuifahamu nyumba yetu iko wapi nikajibadirisha na kuwa kimjusi nikatambaa na ukuta wa nyumba mpaka nikatokezea ndani nikaenda getini na kutega mtego wangu,
mama akifika pale atapita kama kawa ila lile jinamizi litanasa nikazama nikaweza kusikia mighuno ya kimapenzi ikitokea chumba kimoja wapo ndani ya nyumba ile nikiwa vile vile mjusi nikaingia ndani ya chumba hiko nilicho kiona nikabaki kutoa macho tu, ni baba yangu mzazi anafanya kitendo cha kumsariti mama why?"
nikajigeuza faster nikajivika katika umbo la mama na kufungua kitasa cha mlango nikatoka kwa nnje na kujifanya nausukumiza mlango baba na yule mwanamke wakastuka na kuangalia kule mlangoni wakabaki kuduwaa tu nikakaza macho na kuanza kudondosha mchozi na kusema “Yaani siamini kama unaweza kunitendea unyama kama huu yani nimeeondoka juzi tu leo hii unaingiza mwanamke ndani tena juu ya kitanda changu unafanya unyama kama huo,!!!"
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni