TUPEANE (11)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
“Yaani siamini kama unaweza kunitendea unyama kama huu yani nimeeondoka juzi tu leo hii unaingiza mwanamke ndani tena juu ya kitanda changu unafanya unyama kama huo,!!!"SASA ENDELEA...
Kwa sauti ya kubabaika baba akatamka “hapana!! mke wangu ni shetani tu kanipitia nisamehe mama Hafidhi,' “hapana siwezi kukusamehe kwa hili mangapi mabaya umenitendea unakunywa mipombe yako bange unavuta nikikwambia acha unanipiga ukaona haitoshi umeamua kuzini nnje ya ndoa bora huo uchafu wako ungeufanyia huko sio kwenye kitanda changu mimi,nikamtupia jicho yule binti na kuweza kuusoma wasifu wa maisha yake maana mzimu una uwezo wa kufahamu kila ulicho kifanya nikamtolea sauti ya ukali “wee!!! malaya mkubwa mshezi sana mpumbavu wee usiekuwa na haya naomba upotee haraka sana ndani ya nyumba yangu huku akitetemeka akatoka na viwalo vyake mbio ile anatoka tu akapishana na mama,
mama akajikuta anajisemea “mbona Habiba yuko mbio vile anatokea wapi?" akabaki kusikitika tu nikamwambia baba nimekusamehe kwa kitendo ulicho kifanya iwapo utaniahidi kufanya hiki nitakacho kuomba, huku akiwa kapiga magoti kwa kuomba msamaha akasema “ndio mke wangu nipo tayari kufanya chochote kile uniambicho niambie hata sasa hivi nitatenda,
“kwanza kabisa uache kunywa pombe na kuvuta bange kingine urudi kazini kesho yake hasubuhi haraka sana mwisho kabisa mwili wa mwanetu Hafidhi mdogo ufukuliwe haraka sana,
sawa mke wangu nimekusikia nitafanya hivyo, jamani usiombe kufumaniwa ni shida sana unakuwa mdogoo kama kidonge cha pilitoni vile nikafahamu mama ndio yupo getini anaingia usiku saa mbili sasa nikatoka ndani ya chumba na kujigeuza njiwa nikapaa na kwenda kukaa juu ya geti kama nilivyo panga mama akapita ule mzimu au jinamizi likabaki pale pale getini,
sikutaka kufahamu kitakacho endelea ndani nikashuka kutoka juu ya geti ule mzimu ukastuka baada kuweza kuniona mimi nikamshika na kusepa nae safari moja kwa moja mpaka daraja la sarenda nikatua hapo na kuanza kumuhoji “wewe ni nani?"
“naitwa figisu,
“ahahaha unaitwa figisu unatokea wapi?"
kikanijibu nyodo kwa kusema natokea utotoni, nikamshika na kumminya zaidi kwa kumuunguza na moto akabaki kupiga kelele nimuache, “aiiii!!! inaumaa!!!
“ukitaka nisikutese na nikuache ukiwa mzima nijibu maswali yangu kiufasaha staki upindishe swali hata moja, “sawa mkuu niachie basi!!!
nikamuachia na kumuuliza “eheee unatokea wapi?"
“natokea handeni, “handeni ndio wapi?
“ni tanga, “oky sasa kwa nini ulikuwa unamfatilia mama yangu?"
nilitumwa na mkuu, “mkuu wako ni nani na yuko wapi kwa sasa?"
akashindwa kujibu swali hili nikamshika tena na kuzidi kumuunguza akapiga kelele tu “niachee!!! nikutajie mkuu wetu ni Nipe nikupe, baada kutaja jina la Nipe nikupe nikajikuta namuachia haraka sana na kusema “shit! pumbavu zake huyu mwana haramu kumbe kote kote yupo nikiwa nimegeuka nikasikia kivumbi tu nyuma nikageuka kucheki kumbe kile kimzimu kinakimbia kwa kupaa juu,
nami nikapaa na kuanza kukakimbiza ni kiumbe kidogo sana kwangu ila ni hatari kwa maisha ya wanaadamu kusema kweli kina mbio kama kishada tukajikuta tunatokea bahari ya hindi akajitosa kwenye maji ya bahari nami nikazama humo humo ndugu mpenzi msomaji iyache bahari iitwe bahari ndani yake kuna viumbe vya ajabu sana
tukawa tukikimbizana kupitia balabala za majini huku tukikoswa koswa kugongwa na magari mwisho tukafika sehemu akaingia kwenye mjumba mkuubwa wa gorofa hivi kabra sijachukua uamuzi wa kuingia ikaibuka midudu aina ya Godzilla inawaka moto nikarudi nyuma kwanza niweze ku fightng nikajivuta nyuma zaidi na kuanza kujibadirisha nikawa Godzilla mkubwa zaidi yao sasa vita vikaanza chini ya bahari ikawa patashika nguo kuchanika nikapambana yani nang'ata natikisa natupa kule vile viumbe vibishi hivyo mpaka kero na wao wakazidi kujibu mashambulizi cha ajabu gorofa linatembea ndio nishaona vitu vingi vya ajabu ila sio gorofa kutembea bwana kama uchawi huku majini kumezidi baada kupambana takribani maasaa 6 hivi hali ikawa shali ila tumeleta maafa makubwa kwa viumbe wengine kama samaki n.k nikaibuka kutoka chini ya maji na kupanda juu nikaona hali ya sitofahamu coco nzima usiku ule imechafuka kwa samaki waliokufa na kusikia sauti za walio jeruhiwa wakiomba msaada “ehee Mungu baba saidia mimi kiumbe chako niweze kurudi majini nisije nikafa hapa angali nina watoto nawanyonyesha ni baazi ya samaki mmoja akiongea
hivyo nikasimama na kupuliza upepo mkali sana vitu vyote vikarudi majini hali ikawa shwali
nikatoka na kuingia kwenye ukumbi wa coco siku hiyo kulikuwa na wasanii wakitumbuiza sijui kina j.t na nyimbo yake ya kidato kimoja kuna Mr blue yani wengi tu nikaweza kutambua katika umati ulio jazana mule kuna mchanganyiko wa viumbe yani binaadamu na majinni kama jamaa mmoja anayanyonya matiti ya binti mmoja wa kijini kufahamu akizani binaadamu mwenzie nikajikuta naguswa begani kucheki ni muhudumu akaniambia huku akininyooshea kidole “samahani wee kaka unaitwa kulee, nikacheki sehemu ambayo naitwa macho yangu yakagongana moja kwa moja na binti mrembo matata sana nikajinyanyu na kumfata kitendo cha kufika likasikika zinga la yowe kutoka kwa yule Dada aliye niitaa “mama weee!!!
nakufaa! akaenda chini
Nakufaa yule mwana dada akaenda chini huku akiwa anavuja damu tumboni nikaona mpini wa kisu ukiwa una ning'inia tumboni kwake nikainama faster na kukichomoa kile kisu huku akiwa anagugumia kwa maumivu hata aliye mtendea kitendo kile sikuweza kumuona ni nani na kwa nini kamchoma kisu mrembo kama huyu nikiwa bado nimeinama nikajikuta nashikwa na kutupwa mbaali na kudondokea kwenye meza ya vinywaji nikainuka haraka sana kumcheki aliye nifanyia kitendo kile dahaa ni mmoja kati ya majini akiwa kainama na kuinyonya damu ya yule binti kusema ukweli ndani ya ukumbi hali haikuwa shwari ni mkimbize mkimbize kuwai kutoka nnje wakati walioko nnje wakatamani kuingia ndani kuja kushuhudia kunani mbona vurugu,
nikaenda kwa kasi na kumzoa yule jini nikam bamiza ukutani akabaki kuganda tu kutoka hawezi nikamnyanyua yule binti na kusepa nae nikaenda nae moja kwa moja mpaka hospital ya taifa muhimbili na kukuta madocto na manesi wameuchapa usingizi wakati pale four hours 24 inakuwaje wana lala kizembe hivi si kuna shift au vipi?
nikanyanyua mdomo wangu na kutoa sauti ambayo kila mmoja akastuka kutoka usingizini kama una ndugu yako yupo ICU andaa turubai tu maana ile sauti itamuuwa tu,
wakaja kunipokea mwili wa yule Dada moja kwa moja akapelekwa wodini nikabaki kusubili huku nikiwa situlii tulii binafsi japo mimi ni mzimu ila nina roho ya kibinaadamu pia
kila nikimuona doctor au nesi akitoka nasimama na kumuuliza vipi anaendeleaje?"
mara nyingi huwezi kupata jibu la moja kwa moja zaidi ya kuambiwa subili kwanza,
nikawa nimekaa kwenye bench na kucheki jinsi watu walivyo laliana katika hospital ile amini usiamini usingizi ukanipitia hata sisi mizimu tuna lala ikumbukwe ya kwamba katika jamii tunayo ishi vitu vingi sana binaadamu wanashare na majini au mizimu kuoga kula swala la mapenzi n.k
nikaja kustuka baada kusikia sauti ya kama mtu anafagia hivi nikajinyanyua kisha kupiga miyayo kazaa ila nikahisi pembeni yangu kuna mtu kani simamia nikageuka kumcheki ni bibi kakunja ndita na kunikazia macho vibaya mno baada kutizamana akaniomba nimfate,
nikamfata kikawaida tu baada kufika sehemu ambayo pako kimyaa hakuna watu watu akaniuliza, “wee Hafidhi hivi unaujuwa wajibu wa kazi uliyo tumwa au?"
“ndio bibi naujuwa! “kama unaujuwa sasa mbona unafanya kazi ambazo ziko nnje ya makubaliano yetu kule kuzimu?"
“ndio bibi nafahamu kwani vipi mpaka unaniuliza hivyo?"
huku dar es salaam umekuja kufanya nini?"
“huku nimekuja kumlinda mama yangu!
“aliye kwambia wewe una mama hapa duniani ni nani?"
“ina maana yule sio mama yangu sio?"
“sikia nikwambie kitu Hafidhi kila dakika unazidi kuwapa gadhabu wakubwa wa kuzimu kazi uliyo tumwa ni nyingine wewe umekuja kufanya nyingine sasa basi tambua usipo jilekebisha tabia yako mizimu
itakutenga,
baada bibi kusema vile akapotea kabra ya kusikia naitwa
“wee kaka!!! nikageuka kucheki naitwa mimi au,
nikamuona nesi wa kike akiniita nikaenda kumsikiliza akaniambia naitajika chumba cha doctor
hata hakunielekeza wapi nikaondoka moja kwa moja mpaka ndani ya chumba hiko nikabisha hodi na kumkuta mzee wa makamu hivi amekaa akiwa ametinga koti lake kuubwa jeupe na miwani ya macho shingoni kaning'iniza kidude cha kupimia joto
nikakaa kwenye kiti na kupeana nae salamu
“kwanza pore sana kijana,
“hasante doctor!
“kwanza napenda kukwambia ya kwamba hari ya mgonjwa wako sio mbaya sana
usiku kucha tulijitahidi katika kutibu jeraha lake na chakushuru ni kwamba kisu alicho chomwa hakikugusa utumbo time a kulishona jeraha lake,
shukrani doctor tena hasante sana huku nikimpa kiganja cha mkono tena akanipokea
“hivi katika tukio kama hili japo limetokea usiku sana je ushatoa taarifa police?"
“ndio nishatoa na maafande wapo nnje hapo ngojea niwaite,
“sawa waambie waingie maana hili tukio si la kawaida kijana wangu usije jikuta unaingia matatizoni bure,
kuna maneno nikayasema
moyoni na kutengeneza
maafande wa uwongo kama watatu hivi kisha nikatoka nikafungua mlango na kujifanya nawaita
“afande Nyemo, mnaitwa hofisini kwa doctor basi wakaingia wakiwa nazifu maana hata doctor alipo waona ikabidi asimame kwanza basi tukahojiwa pale na kutoka kwenda kumuona mgonjwa nikampa pumzi aweze kuongea akatoa maelezo yote akawataja baazi ya watu anao hisi ndio wamemtendea unyama ule akataja na familia yake kwa ujumla
baada kuandika andika baazi ya maelezo wale
maafande vivuli wakaondoka
nikaenda kwanza kupiga cm kwa familia ya yule binti maana usiulize number zao nilizitoa wapi kama robo saa hivi magari yaka jazana kila aliyekuwepo kwenye gari akashuka mbio mbio na kwenda mapokezi nikatabasamu na
kusema,
“shukrani sana Cristina nazani ushapata msaada wacha mimi niende zangu nikajongea mpaka wodi aliyo lazwa Christin kupia nnje ya mlango nikamtizama
kwa ndani na kuona jinsi ndugu
zake hasa mama yake akilia
nikamsikia baba yake akiuliza
“doctor yuko wapi huyo kijana aliye msaidia mwanangu kumleta hapa?"
akamjibu “yupo nnje huko,
“embu twende nikaonane nae!"
wakiwa wanajiandaa kutoka nnje nikajivika kivuli sitoweza
kuonekana na mtu wa kawaida
hata kidogo wakatoka nnje na kuanza kunitafuta kila kona hawanioni mwisho doctor akasema “labda atakuwa katoka kwenda kunywa chai maana muda mrefu tu alikuwa pale amekaa"
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni