TUPEANE (2)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA PILI
"Ni swali zuri sana mjukuu wangu kwa kuuliza kwanza kabisa huyo nipe nikupe ni shujaa wa kijiji hiki enzi za uhai wake alikuwa ni kama mfalme wa himaya hii yote katika uongozi wake akatunga sheria yani mira na desturi na atakaye vunja mira hizo lazima afe watu wengi sana wakawa wakiuwawa kwa kuvunja sheria hizo lakini baada ya kifo chake wazee kwa vijana wakasema tuko huru kumbe walijidanganya ikawa yeyote akivunja mira tu anakufa gafla kumbe mzimu wake umetumwa kuendelea kuifanya hiyo kazi"SASA ENDELEA...
"Sasa bibi mira zipi hizo ukizivunja lazima ufe?"
ya kwanza ni kutoingia kwenye mashamba yake kuchukuwa chochote kile cha pili ni kutofanya zinaa yani kufanya mapenzi na binti wa kijiji hiki ikiwa bado hujafunga nae ndoa "what bibi hiyo nayo sheria au?
"ndio hiyo nayo ni sheria ya kijiji hiki ndio ambayo watu wengi wanaangamia kuhusu sheria hiyo,
"sasa anajuwaje kama umefanya mapenzi bila ndoa?"
kwanza kabisa mjukuu wangu naomba utambuwe ya kwamba nipe nikupe kijiji hiki choote kipo kiganjani kwake chochote kibaya ukifanyacho anakiona vijana wengi sana kutoka mjini wanaangamia kutokana na ubishi wao yani kama unamuitaji binti wa kijiji hiki fata taratibu zote kisha ufunge nae ndoa muishi raha mustarehe basi, "sasa bibi kama mambo yenyewe ndoa haya mi naona kesho tu nirudi zangu town nisije kufa kizembe hapa, "wewe huwezi kufa kwani hujafanya makosa yeyote cha umuhimu ni kuzingatia sheria nilizo kwambia basi tukageuza macho yetu baada kuona kundi la watu kama 6 hivi wamefika pale huyu akiweka jembe pembeni mwingine katua mzigo wa kuni mwingine kiroba kina damu damu bila shaka zitakuwa nyama tu nikamcheki yule babu na vijana wakiume wa tatu wa kike mmoja "afu bibi mi kule shambani siendi tena,' "kwa nini tena Rukia hutaki kwenda tena?" ahaa kazi za kule ngumu tu, ndio kujikomaza huko mjukuu wangu ili baadae usije kuteseka kwa mumeo, "aku mi kesho siendi ng'oo akawa anaingia ndani bibi akamwita "wee Rukia, abee bibi, "embu njoo huku, akaja, "kwanza kabisa naomba niwatambulishe huyu ni ndugu yenu anaitwa Hafidhi j ikram kutoka huko mjini "ahaa kumbee yulee ukasema ipo siku atakuja, "Hafidhi huyu ndio babu yako au mme mwenzako na yule pale ni mtoto wa mama yako mkubwa basi baada utamburisho tukapeana salamu usiku kigiza kikaingia bibi akaanza kutuhadithia story za kale sijui kulikuwa na watoto saba mama mmoja baba mmoja wakawa wakiishi kwa faraha na amani tu siku ya siku wazazi wakagombana na kupeana talaka baba akaondoka na kwenda kuishi mbaali
kwakuwa watoto walipafahamu
anapoishi baba yao wakawa na kawaida ya kwenda kucheza basi siku moja wakamuaga mama yao "mama..mama, abee wanangu,' "sie leo tunaenda kwa baba kucheza, "haya nendeni wanangu ila msikawie kurudi kingine ninacho waomba mkikutana na mtu yeyote njiani msiongee nae, "sasa mama hata salamu tusimpe au akitusalimia tusiitikie?"
ndio musiitikie nyie endeleeni na safari yenu tu,
sawa mama tumekusikia, haya safari njema watoto wale wakatoka njiani wakipiga story za hapa na pale huku wakitaniana kufika sehemu moja hivi njia panda wakakutana na mtoto akiwa anaimba imba yule mtoto baada kuwaona wale watoto wenzie akawapa salamu "jamani mambo vipi?"
wale watoto kiimyaa, "hivi jamani hamnisikii au? vile vitoto saba kufika sehemu vikasimama mmoja akasema "oyaa washkaji eee sio ishu tunavyo fanya kumchunia mtoto mwenzetu, "hivi wewe hukumbuki mama kasema nini?"
ndio nakumbuka lakini yule ni mtoto mwenzetu na istoshe kwa baba tunaenda kucheza mpira sasa tumchukuwe na huyu twende nae tuwe wanne wanne basi wakafanya ujinga wa kumuitikia na kwenda nae mpaka kwa baba yao wakacheeza mpira mpaka jioni wakarudi nyumbani kwa mama yao basi kumbe nyumbani kwa mama kuna desturi kabra hujaingia ndani kuna nyimbo unaimba ukipatia unaingia ndani ukikosea ndani huingii wakwanza akapatia wa pili akapatia watatu yule mtoto waliekutana nae njiani, " sasa embu nikukatishe kwanza nikutwange swali hivi huyo mtoto ameongozana vipi mpaka hapo wakampa ruhusa ya kuimba nyimbo single ndani?"
"ni hivi wakati wanaongozana nae mmoja kati ya watoto saba alimuuliza "wewe mbona uendi kwenu unaenda kwetu kufanya nini?" akajibu kiu kimembana basi wakaenda nae kwa shart ajuwe kuimba nyimbo tu ya kuingia ndani "weweee naniii? "mimi mwanao eheee, ainda ainda teteee "watoka wapiiii? "kwa baba eheee ainda..ainda teteee.. "kufanya niniii? "kucheza eheee ainda....ainda..teteee, basi ukipatia unaingia yule mtoto mgeni mara ya kwanza akakosea ikabidi akae pembeni je mpaka wakaingia watoto wanne akaja kujaribu tena akapatia akaingia kumbe ni mzimu sio mtoto alipoingia tu akawatafuna wote mule ndani, "khaa! bibi kumbe hakuwa mtoto ni jini? ndio, mama akasema "afu wee Hafidhi tumechoka na maswali yako subili hadithi iishe ehee mama ikawaje kwa wale watoto watatu waliobaki nnje?"
ehee naendelea, nikanyanyuka na kwenda zangu ndani kulala hadithi yenyewe inatisha sikutaka kuendelea kuisikiliza Rukia akaja kunionyesha sehemu ya kulala kitanda cha kamba tu juu umetandikwa mkeka nikajilaza na kuanza kumfikilia nipe nikupe nikajiuliza ni Mwenyezi mungu pekee ndio kaweka sheria za kutozini mpaka siku yakufunga ndo atakaye zini ni motoni tu sasa huyu nipe nikupe ukizini adhabu yake kifo dadeki nitapambana tu kama yeye nipe nikupe mimi ninyime nikunyime pumbavuu...
Mawazo yakanisonga juu ya kumuwaza huyu nipe nikupe, usingizi nao ukanichukuwa nikaja kustuka baada kusikia sauti za majogoo wakiwika nikaitoa shuka mwilini mwangu na kushuka kitandani nikatoka nnje yani kuna baridi sana ukungu umetanda kila maeneo dahaa nikaingia chooni kujisaidia kwanza nikatoka na kumkuta babu anakoka moto tupate kuota "shikamoo babu, "marhabaa mjukuu wangu za hasubuhi?" nzuri tu sijui wewe? "mi sijambo, baada kufika kama saa tatu au nne hivi familia nzima tukawa tupo kwenye mkeka tukipanga hili na lile bibi akasema "Hafidhi mjukuu wangu sasa leo ndio nafasi nzuri ya mjomba ako kukutembeza katika kijiji hiki akuonyeshe mazingira yote hasa mashamba ya nipe nikupe na kaburi lake kwa ujumla, Ankor akatamka "sasa mama unataka nimpeleke akalione kaburi la nipe nikupe kwa lipi hasa?"
"mwenzako jana kaulizia habari za huyo nipe nikupe wee nendeni na wenzako mkamuonyeshe tu, tukainuka kujiandaa na safari ya kwenda huko, tukapita sehemu mbali mbali na kukutana na vitu ambavyo sikuwai kuviona kwa macho zaidi ya kuvisoma tu kwenye somo la history nakumbuka siku hiyo jioni kulikuwa na mechi ya mpira wa miguu kati ya kijiji chetu cha kilwa kiwawa na kijiji cha jirani kinacho itwa kilwa kivinje tukafika mapema uwanjani na kushuhudia ngonjera ngonjera na mabinti wa kijiji chetu watoto wakike wakiyakata mauno katika kigoma cha mdando yani full raha Ankor akaniuliza "Hafidhi vipi unacheza au?"
hapana Ankor nyie chezeni tu time yote macho yangu kwa binti mmoja matata sana yani kwa jinsi anavyo yazungusha mauno mawazo yakanipeleka mbali ya kwamba nipo nae kwenye bed ananikatikia asssssssssss,,,ooohoooo,,,mmmmh,,nikastuka baada kupigwa kikumbo na binti mmoja hivi na kuniambia "samahani kaka yangu, "bila samahani mrembo, "khaa kumbe wewe Hafidhi mi nilijuwa nani?"
wee Khadija kama sio nani basi ni Rooney, "wewe nawe huyo Rooney ndio nani sasa?"
usimtaje nani ni mchezaji huyo wa Manchester united, "mi sijui bwana, "hivi Khadija yule binti anaitwa nani?" anaitwa Rooney, "pumbavu zako, nawe si umemtaja nani?"
tukacheeka sio siri tulizoena sana kumbuka jana tu ndio tumeonana mimi na yeye kule kisimani "ahaaa yule anaitwa Mwajuma ni binti wa mwenye kiti wa kijiji, "oky kaolewa au?"
hapana bado hajaolewa vipi unataka kutangaza nia au? kabra sijamjibu kitu tukasikia goooo...kucheki team pinzani wanashangilia "weweeee na kigoma cha cha Kissinger....mpira ukawekwa kati tukawa busy sasa kucheki kabumbu kusema kweli vijijini kuna vipaji balaa tatizo hawajapata nafasi ya kuonekana tu gafla tukapigwa cha pili jamani team ikaanza kupoteana yani hadi kuukotro mpira mpira mtu anashindwa na kuishia kudondoka tu kidume nikaomba number aliyekwambia mtoto wa town kijijini ananyimwa number nani tena wanakunyenyekea kama vile c.ronaldo nikazama uwanjani kipindi cha pili hiko nikawa nacheza wingi ya kulia na guu langu la mavi tokea niingie mpira ukabadirika tukawa tukifanya mashambulizi ya ajabu "oyaaa wee mkude muangalie huyo dogo katoka town ni hatari sana, nikajisemea moyoni kama kunikaba labda team nzima mtaweza lakini kama wewe peke yako utaumia tu basi ikija mipira ya juu akitaka kuruka tu namkanyaga juu ya vidole anashindwa kuruka na kuishia kuchuchumalia tu mi kiulaiini najipigia vichwa au kuutuliza gambani nikajitahidi kupiga vyenga na kufumua mishuti kikwazo kipa wao kama de gea vile anadaka mbaya mpaka dakika ya 75 washkaji urimi nnje nnje kwani kasi tuliyokuja nayo shida tupu kipa wao si akaumia na kutoka nnje ikawa kona Ankor akaenda kuichonga nikajipinda na kuruka edar kitu goooal....nikaubeba mpira na kuuweka kati 2-1 watu weweee speed ikazidi kabra ya Abasi yule jamaa hadi akataka kukata mti kule kisimani kuchezewa rafu kipenga kikapulizwa fauro kama David Beckham vile nikauweka mpira vizuri na kuuchonga zinga fauro kitu kikaenda tisini gooooal...nikaja kukumbatiwa na wachezaji wenzangu kwa furaha kuna moja nikapiga vyenga kwa kumtoka beki wa kwanza wapili nikaipiga R2 wanao tumia pray station 2 wataelewa nini maana yake ikawa 3-2 mbili "wee Mkude boya sana unamuachaje dogo huyo mpaka ana piga hat trick kizembe hivyo? akamjibu kocha wake boya mwenyewe kama unaweza njoo umkabe wewe hapa tunacheza mpira sio michezo ya kukabana, "embu toka nnje aingie Frank, "poa kiroho safi natoka ila dogo anajuwa yule, mara kipyenga kikapulizwa na mpira umekwisha shamra shamra na vifijo na mayowe nikaingia kati kucheza mdando yani kijijini some time raha sana Mwajuma akaja kunikumbatia dahaa dodo kitu sindano mpaka nikasimamisha mkomboti wangu kwa hasira akawa yeye mbele mimi nyuma akiwa ananikatia viuno mpaka saa 4 usiku shelehe ya kuchukua kombe siku hiyo ikaisha kumbe vijiji viwili waliwekeana dau la ng'ombe wawili wawili midume iliyo shiba mshindi anabeba mzigo nilifurahi sana kuweza kukisaidia kijiji chetu kupata heshima njia nzima tukawa tukipiga story na kucheka tu,
tukafika home bibi babu wala mama hawakulala mpaka mida hiyo bado wapo nnje tu wakipiga story nikaenda kuoga na kupata msosi, nikiwa nimelala kama kawaida nikaanza kumuwaza Mwajuma binti ambaye ametokea kuuteka moyo wangu gafla mpaka nikajisemea moyoni kabra sijarudi town lazima nimuonje,
asubuhi ndio kuna pambazuka nikasikia sauti ya vyuma vyuma vikigongana nikaitoa shuka kucheki babu akiwa na jembe begani anatoka wakafatia watoto wa mamkubwa binafsi sikuwa na mazoea nao kiviile zaidi ya kuzoeana na Mjomba Mwichande tu nae nikamuona akitoka nikamwita
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni