SEHEMU YA SITA
“Kijana umekiangamiza kijiji kwa kuleta kiumbe haramu sasa basi itabidi ulipe utanyang'anywa hicho kipawa cha kushika vitu na kuchapwa mijeredi 1000 na kuingizwa kwenye tanuri la moto utakaa humo takribani miezi sita au miaka miwili"SASA ENDELEA...
Nikiwa najiandaa kujibu kitu gafla nikajikuta nabebwa na mijitu mireefu hata mwisho wa shingo zao sikuweza kuziona kitendo cha kuchukuliwa msobe msobe sikuweza kufahamu wapi napelekwa safari ilikuwa ndefu nikiwa nimebanwa kama kifaranga cha kuku kilicho bebwa na mwewe, tukafika sehemu wakaniachia nikawa nadondoka kwa kasi ya kimbunga nikatoa sehemu ambayo kuna mafuvu tu ya watu kuna tisha balaa nikawa naweweseka gafla nikaanza kupapaswa na yale mafuvu kudadeki kumbe walikuwa ni wazima ni viumbe gani hawa hawana hata nyama zaidi ya mifupa tu nikikumbuka nilishawai kuangali muvi moja ya night of the dead au army of darkness yani jeshi la wafu sasa leo nawaona live nikahisi labda ndoto nitakuja kustuka tu lakini haikuwa hivyo mateso yakawa zaidi ya mateso Hafidhi j nikakosa raha na kutamani kufa sasa nife mara ngapi wakati nishakufa dahaa kila kukicha nachapwa mijeredi ambayo ilikuwa ikiondoka na nyama za mwili wangu nikakonda kwa kukondeana nikabaki kama zezeta yani kufa sifi cha moto nakiona kula nikawa sili zaidi ya kupewa unga ukichanganywa na maji eti unaambiwa kunywa huo ndio uji usiombe kwenda Kuzimu kuna tisha mwisho wa siku nikaja kutupwa mbele ya nyumba ya bibi nikiwa sijitambui kabisa nikaja kupata fahamu baada kuhisi maji yakinimwagikia kufumbua macho hivi kumbe ni Rukia anaosha vyombo bila kufahamu akamwaga maji ya ukoko sehemu niliyokuwa nimelala nikajisikia maumivu kila maeneo ya mwili yangu yani kama mtu aliyeunguzwa na moto nikabaki kulia tu ni nani wakunisaidia ukicheki siwezi kushika chochote tena nikaja kufahamu ushapita mwaka mmoja tokea nipelekwe kuteswa kwani niliweza kumuona Mwajuma akiwa na mtoto wa kiume tena kinajifunza kutembea nikabaki kutabasamu siku basi siku moja kulikuwa na sherehe inafanyika uwanja wa shule sherehe itaanza saa mbili usiku nikatamani kwenda japo kushuhudia ila nikashindwa kwani mwili wangu haukuwa na nguvu ya hata kupiga hatua moja mbele nilipo kaa ndio hapo hapo juwa vua vyote vyangu basi familia ikajiandaa na kutoka nikabaki nadondosha chozi nikijalibu kuita “jamaniii nisaidieni mimi niko hapaa, tokea siku hiyo nipe nikupe sikuweza kumuona tena usiku ukazidi kuingia giza totoroo walioenda kwenye sherehe bado kurudi gafla nikiwa nimejiinamia nikastuka baada kuguswa begani, nikageuka na kukutanisha macho yangu na sura ngeni machoni mwangu kwa mshangao nikamuuliza “wee nani?"akatabasamu kabla ya kunijibu kisha akatamka “mimi ni kaka yako naitwa Hafidhi j ikram nimetumwa na bibi kuja kukusaidia,'
Kitendo cha yule mtu kusema eti yeye kaka yangu tena anaitwa Hafidhi j ikram kikanifanya niduwae zaidi, akaniambia huku akinipiga piga begani, “sikia bwana mdogo kuanzia sasa hutakiwi kuwa na hofu ya aina yoyote ile mimi nipo kwa ajili yako sasa basi itabidi wewe uwe mimi na mimi niwe wewe, “hapana wewe sio kaka yangu utakuwa nipe nikupe tu kwanza kaka yangu amekufa kabra mimi sijazaliwa, niliweza kumwambia hivyo kwa sauti ya kilio, Hafidhi mdogo wangu au wajina wangu amini mimi ni kaka yako ndio nimetoka kuzimu na nimekuja hapa kukusaidia mbona wewe umekufa na ushazikwa au hujafa?" nikatikisa kichwa kuashilia hapana sijafa, akanyanyuka kisha akaangaza macho kushoto na kulia mwisho akanitizama mimi na kunikazia macho taratiibu akaanza kubadilika na kuwa mimi afu mimi nikawa yeye nikiwa smart nimenenepa mwenye hafya kisha akaniambia potea...poteaa ile sauti ikanifanya nipaee na kwenda sehemu isiyo julikana dahaaa
mambo vipi?" wapenzi wa mtaa wa tatu nazani mnanikumbuka japo nishakufa kitambo sana nimetumwa kuja kumpa mdogo wangu msaada katika kijiji cha nyumbani kwa mzaa mama kijiji ambacho mambo ya ushetani yametawala sana wananchi wanaishi kwa hofu kubwa kila kukicha watu wanapotea katika mazingira ya kutatanisha sasa basi nimekuja kuwakomesha, nikiwa nimekaa pale pale alipokuwa amekaa mdogo wangu kabra mimi sijaja nikawa nasikia sauti ya vigoma kwa mbaali nikajuwa bila shaka kuna sehemu kutakuwa na sherehe tu nikajinyanyua pale chini na kujigeuza kutoka katika umbo la mdogo wangu na kuwa katika umbo langu kipindi niko hai nikasepa kama upepo kama sec 3 tu nishafika eneo la sherehe faster kusema kweli ilikuwa sherehe ya kijiji kizima wazee kwa vijana wamejazana huku misufuria ya pombe za kienyeji na togwa zikinywewa kwa wingi, wengi wamekuja hadi na watoto wao wakiwa wamewabeba migongoni kijiji kilipendeza usiku huo nikiwa katika kushangashanga nikaweza kusikia sauti kama ya kilio ya binti akiomba msaada yani nilikuwa mwepesi sana wa kunasa hisia iwapo kuna tatizo sehemu yeyote ile nikafika faster na kumkuta msichana akivuja damu tumboni mikono yake yote miwili akiwa kashikilia kitovu chake nikajivika kivuli nisiweze kuonekana na mtu yeyote, yule binti akaenda chini hakuna mtu wa kuja kumsaidia nikajivua kivuli na kuwa mtu wa kawaida binti akaenda chini nikawai kumshika na kuanza kumwita, “binti...binti amkaa...akayatoa macho pima kuniangalia usoni japo eneo tulioko ni Giza tupu, kwa sauti ya mkato mkato akajitahidi kuongea, “nii liku jaaa huuku..kukojooa..gaaaflaa niiipe niikupe.. nikaona bora nimpe pumzi aongee vizuri haya maneno ya kukata kata mi simuelewi, baada kumpa pumzi akazungumza, “nilikuja huku kukojoa gafla akanitokea nipe nikupe na kunivutia gizani zaidi, “kwa nini amekuvuta gizani?" akajibu “kwa sababu nilipoenda mjini kuna mwanaume nilifanya nae mapenzi, baada kusema vile tu mikono ikafutuka pale tumboni utumbo ukatoka kwa kasi ya ajabu dahaa midamu tu uchungu na hasira zikanishika zaidi kwa kuona ni jinsi gani yule binti kafa kikatili vile nikamlaza chini kisha nikainyooshea kidole cha shahada ile maiti kivuli chake kikanyanyuka na kuanza kushangaa shangaa tu, kikatoka mbio kwenda sehemu ya sherehe nami nikamfata nimuone nini anataka kufanya nikamuona anaangaika kumgusa kila mtu na kumuongelesha wenzake hata hawana abari nae akabaki kujishangaa macho yetu yakagongana akaja mbio kwangu na kuniuliza “wee mkaka mbona kama unanicheka mimi?" nikawa natabasamu tu, “hivi kaka yangu mbona kila ninae ongea nae anijibu chochote sikumjibu kitu, akaona bora aondoke tu sio siri binti aliangaika sana kupaza sauti yake kwa kuongea na kila anaemfahamu mpaka akachoka na kuamua kukaa chini akiwa analia usiku ukapita hatimae kesho yake hasubuhi, nikiwa nimekaa mbele ya nyumba ya bibi kila mmoja akiwa na kikombe cha uji kwenye sinia kuna ming'oko sijui ndugu msomaji unaipata, nikainuka pale nilipokaa na kwenda walipokaa wao gafla kila mmoja akastuka baada kusikia sauti za vilio vikitokea nyumba ya jilani tu kila mmoja akaacha kula na kwenda huko kufahamu nini kimetokea, nikiwa nimebaki pale nikavishika vikombe vyao nikanywa uji wote mpaka wa kwenye sufulia ming'oko nikaitafuna hakuna nilicho bakisha, “khaa! vyakula nani kavila vyote?"
ni Rukia mtoto wa mamkubwa ambae ameshafariki kitambo watoto wake wanalelewa na bibi baada baba yao kuowa mke mwingine kama ujuavyo baazi ya mama wakambo wengine si watu wazuri watoto wakashindishwa njaa kuanzia hasubi mpaka usiku ikafikia kipindi Rukia akawa analazwa kwenye banda la kuku na kupewa machicha ya nazi ale sababu alikuwa na njaa akawa anayafakamia baba yao hakuwa na taarifa yeyote sijui kafanywa ndondocha au?"
mateso yalipozidi sana ndio siku moja wakaamua kutoroka na kuja kilwa kwa bibi mzaa mama yao ambae mimi namwita mama mkubwa, baada Rukia kushangaa na kuuliza vyakula nani amekula akatoka mbio kurudi kule kwenye vilio nikamuona anakuja akiwa na bibi pamoja na kaka zake nilicho fanya nikanyoosha mkono kwenye sufulia uji ukajaa kwenye sinia ming'oko ikarudi kisha nikajikausha kama vile sio mimi, “hivi wee Rukia ndio nini kuniangaisha yani kunitoa koote kule mwenzako nawapa pore wafiwa unakuja ohoo bibi uji umenywewa wote huu nini sasa, akatishia kama kumwagia hivi, akaweka sufulia chini na kuondoka zake “afu Dada rukia siku zote nakwambiaga acha wenge,' wakakaa kuendelea kula “hivi kaka Issa imekuwaje Fatuma afe gafla tu wakati jana tulikuwa nae kwenye sherehe?" hata mimi nashangaa nilicheza nae akanikatikia miuno mpa nikatamani kwenda nae vichakani, “ahaa! kaka hujitaki wewe, “humjui nipe nikupe mfano ndugu yetu Hafidhi j ikram ndio kwaanza ametoka mjini ndani ya siku tatu tu akafa, “unajuwa nini Dada mi nahisi Hafidhi hajafa kisa katembea na mwanamka itakuwa labda kavamia shamba la nipe nikupe, “wee unasema shamba lilee?" ndio itakuwa hivyo, nikageuza shingo yangu kuangalia ni shamba gani Rukia anaonyesha, baada kuweza kuliona nikanyanyuka na kuanza kulifata baada kulikalibia nikafungua mdomo wangu na kuanza kutema moto kama mdudu aina ya dragon moto ukawa mkubwa sana shamba likaanza kuteketea ni moja kati ya vitu vya kumtafuta nipe nikupe tu, "jamanii..motooo motooo huku kama dakika 4 hivi wanakijiji wakajazana na kuanza kuangaika kuuzima moto ikawa ni kazi bure kuweza kuzima moto ule gafla bonge la vua likashuka na moto ukazimika cha ajabu hakukuwa na dalili ya hata majivu ya kitu kuungua nikasikia vicheko vikitokea kwa juu ni mimi pekee ndio niliyeweza kusikia nikainua macho yangu juu na kukutana na sura zenye kutisha vibaya sana sikuweza kuhofia kwani hata mimi naweza kuwa kama wao kumbe haikuwa vua kama nilivyo zania ni maji yaliyokuwa yakitemwa na ile mijitu hata idadi yao sikuijuwa wako wangapi, nikacheka saana
“hahahah!hahaha! nikajisemea hii vita si yakitoto kidume nikajisifia kukaa kuzimu takribani miaka 18 nimepambanishwa na kiumbe cha kila namna na kuibuka mshindi sembuse hawa vinyamkela nikaupata usemi ya kwamba nisijisifu nina mbio nimsifu na anaenikimbiza, nikajuwa bila shaka nina vita kikali sana kumbuka wakati wa uhai wangu nilipambana na wanaadamu na kuufanya mji uwe sawa sasa napambana na majini kwa mizimu ya kishetani, yale maji yakaacha kushuka nikajivika umbo langu la kawaida tu nikajichanganya kwenye msiba nikakiona kivuli cha yule binti kikiangaika nikauchota mchanga na kuupuliza ukaenda moja kwa moja kukisomba kile kivuli na kusepa nacho cha ajabu bibi kila wakati akawa ananiangalia mimi akiwa aamini amini ni mimi au anafananisha,
Bibi akawa anazidi kushangaa shangaa tu mwisho akanyanyuka na kwenda sehemu aliyokaa babu akamnong'oneza kitu na kuonyesha kidole sehemu niliyo kaa mimi babu akaangalia baada kuniona na yeye akanyanyuka kunifata akanisalimia kwa kunipa mkono
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU