TUPEANE (8)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA NANE
Mama hakuwa na jinsi zaidi ya kuondoka huku akijifuta machozi nahisi hata begi lake akaliona zito kulivuta, nikawapoteza wale ndugu bandia kumbuka nina uwezo wa ajabu kwahiyo ni vitu vidogo sana kufanya hivyo kwanza nafsi ikaniuma kwa kumkana mama yangu mzazi lakini kama kulia kashalia kwenye msiba wangu inakuwaje aamini bado niko hai wakati washanizikaSASA ENDELEA...
Siku hiyo nikiwa nimekaa kitandani nawaza na kuwazua jinsi ya kumpata nipe nikupe gafla kwenye pembe ya chumba changu akaingia mtu akiwa amebeba kikapu akaangaza angaza macho chumba kizima kisha akakiweka kikapu chake chini akapanda kitandani na kuanza kunitambuka tambuka huku akiimba “awilee tungoree awilee,,,tungoreee,,,awileee akanitambuka kama dakika kumi hivi kisha akanishika miguu na kunivutia chini ya kitanda laiti angejuwa mi nani asingefanya upumbavu ule anao ufanya tena mchana kweupe ananiwangia baada kunishusha akanilaza kifudi fudi akatoa kwenye kikapu sijui madawa gani na kuanza kunipaka paka mgongoni huku akikazana kuimba tu nikawa nimejikausha kimyaa nione mwisho wake nini huyu mama, baada kumaliza akasepa na kuniacha pale pale chini nikataka kumuonyesha mimi noma na nikajuwa amerudi nyumbani kwake nikayeyuka vuu na kwenda hadi chumbani kwake nikawa nipo chini ya kitanda chake ile nafika tu na yeye ndio anaingia si akaniona unajuwa alistuka sana hakutegemea akabaki kujiuliza nani kamleta huyu huku, akatoka mbio kurudi chumbani kwangu kunicheki je nipo nami nikawai kufika tu akanikuta kwanza akajifikicha macho vizuri anaota au akaja kunishika sijui kunikagua kitendo cha kunishika tu nikamdaka pale pale nikamgeuza bata na kumfukuza kwa mateke mpaka nnje kuna mzee nikamsikia anasema "wee Nassoro njoo umkamate bata huyu huku, nikatoka nnje na kumkuta yule bibi kashadakwa kibaya zaidi aliyemkamata ana kisu tayali nikimcheki mchozi unamtoka dahaa, nifanye nini kumuokoa asichinjwe, nikanyoosha kidole mpaka kwa yule kijana na kujikuta anajikwaa akaenda chini puhu na kuanza kupiga kelele “yalaaa babuuuu mguuu wanguuuu...nakufaa....babu yake akatoka mbio mbio akiwa anauliza “nini tena mjukuu Wang?" mguu babuu,' “umefanyaje?" akawa anaushika shika na kuukanda kanda kwa kumnyoosha, “ayiiiiiiii...babu inaumaaaa...babuu niachee nikazama ndani nikiwa nacheka nazani hata hamu ya kuchinja bata hawakuwa nayo siku hiyo,baada kupita siku tatu mama mwenye nyumba anatafutwa na mumewe watoto zake na ndugu zake wengine huku watu wakisema labda nipe nikupe kashafanya yake kitambo, wakati wanaangaika kumtafuta usiku na mchana mwenzao anawaona anawasikia kinacho mshinda kuongea tu kashakuwa bata siri naijuwa mimi peke yangu siku hiyo usiku wa manane nikaamua kutoka kwenda kumsaka nipe nikupe katika kupiga dolia zangu kwenye kichaka kimoja hivi nikasikia sauti kama ya mwanamama hivi akiomba asiuliwe “nisamehe nipe nikupe nimefanya hivi kuipata dawa tu kwa sababu nimezunguka kijiji kizima dawa hakuna ndio nikaziona katika shamba lako, “sio umeziona katika shamba langu nani umemuomba?"
“sikumuona wa kumuomba nisamehe, nikaweza kuitambua ile sauti kama ya mama hivi, nikawai faster asije akauwa nikatua mbele yao yani kati kati mama nikiwa nimempa mgongo nipe nikupe natizamana nae kwa mara ya kwanza nakutana na kiumbe huyu hakuna mfano wake kibaya zaidi wanakiongozi wao je huyo yukoje?"
akastuka kwa sauti ya kuunguruma akauliza “nani wewe?" niite Hafidhi j ikram, “khakha!Khalkha! kumbe wewe bwana mdogo umekuwa wa ajabu hivi kwanza pisha nimuangamize huyo mwanamke,' “hakuna anaye angamizwa hapa nimekuja kumlinda tu,' “kijana naona maumivu uliyopewa kipindi kile kuzimu hujatosheka sio sasa basi naita jeshi wakukamatee aiiiishiii ni kitendo cha faster nikamtupia kaa la moto mdomoni akabaki kuugulia maumivu akasepa mbio chezea mimi wewe utajamba nikamgeukia mama akiwa anatetemeka nikam beba na kumrudisha nyumbani kwa bibi huku nikimsisitizia arudi mjini haraka sana kesho yake hasubuhi kijiji hakifai hiki nikatoka nikiwa najongea gafla mbele yangu kuna mijitu miwili mireeefu ya kutisha,
Kitendo cha kuona ile mijitu ya kutisha iko mbele yangu nikaingiwa na hofu kidogo nikatoka mbio ikawa mkimbize mkimbize tu mpaka tukatokea mto rufiji nikatua juu ya daraja nao wakatua kwa kishindo wakiwa wanafuka moshi kwa kuhema kumbe hadi kunguru anavyo paa kule juu some time anachoka kama binaadamu akimbiapo, tukabaki kutizamana tu nikaweza kuwasoma kitu cha kuwaangamiza nacho ni maji tu kwa jinsi walivyokuwa wakiyatolea macho maji ya mto ule kisha kunitizama mimi gafla mmoja kati yao akanyoosha mkono na kunizaba zinga la kofi nikajikuta natupwa kule wakaanza kunishambulia kwa kunitemea moto na kunilalua na mikucha yao nikajitahidi kupambana kila nikijibu mapigo ya kuwatemea moto wanacheka nikachumpa na kuzama kwenye maji wakabaki kushangaa shangaa tu nikaibuka na kurudi juu nikiwa nimehifazi maji tumboni kwangu kama liter ishirini nikaanza kuyatema kwa fujo kama vile zima moto wakaanza kutatalika huku wakipiga mayowe ya uchungu kumbe hesabu zangu zilienda sawa katika jitihada za kutaka kuyakimbia maji wakajikuta wanadondokea mtoni na kupotea kabisa ndugu msomaji uache usiku uitwe usiku tu maana mambo mengi yanatokea ukiwa wewe umelala mwenzako ndio anaingia kazini siku zote unapo lala mtangulize Mungu maana yeye ndio kila kitu katika ulinzi wako unaweza kuchezewa na wachawi wakakufanyisha kazi zao na kukulisha nyama mbichi za binaadamu umelala unaota unakula nyama stuka,
nikarudi chumbani kwangu nikiwa nafurahia ushindi ile kuingia tu nikamkuta bibi ananisubili kwa hamu, “hivi Hafidhi kwa nini umekuwa mzaifu sana?" nikabaki kuduwaa pasipo kujibu swali lake, “si nakuuliza wewe kubwa jinga, “ahaa bibi mimi sio kubwa jinga nina akiri zangu kamili ohoo nitakinukisha sasa hivi,' “nenda zako huko usinitishe wala nini wakati vijitu viwili tu vimekutoa jasho la kwapani,' “sasa bibi wewe kwa akili yako vile vijitu au mijitu?" “sikia nikwambie Hafidhi mpaka sasa malkia anasononeka sana kwa utendaji wa kazi yako unafanya kazi kizembe sasa basi kama umeshindwa rudi nyumbani atumwe mwingine kuna vijana kibao wanaitaka hii nafasi hawakuipata malkia akakuteuwa wewe,' “bibi kusema kweli mi najiona niko tofauti yani kama nimepungukiwa na vitu flani hivi, akaniambia “embu sogea hapa,' nikasogea akanishika na kuanza kunikagua gafla akastuka “hii Mungu wangu akabaki kusikitika tu, “bibi kwani vipi mbona unasikitika imekuwaje kwani?"
“kusema kweli mjukuu wangu kuna vitu muhimu ukuchukuwa kutoka kuzimu embu twende haraka ukakabiziwe, tukapotea na kwenda kuzimu ni sehemu mbaya kwa watenda dhambi wote wanatupwa huku yani full mateso kwenye moto wakiwa wanaogerea huku wengine wakimwagiwa asidi wengine wamening'inizwa kwa minyororo yani umepitishwa kwenye haja kubwa na kutokea mdomoni usiombe ndugu yangu kuzimu kuna tisha vibaya sana Kuna binaadamu wa kila namna masuper star hadi watu wa kawaida wengine ni watumishi wa Mungu hapa duniani kumbe ni watenda zambi wakubwa mateso yana muda wake mwisho wa siku unakuwa mtu wa kawaida tu ukiwa kule kule kuzimu na kuwa mwanajeshi wa kupambana na viumbe vibaya ambavyo bado wapo duniani hata mimi nilivyo letwa kwa mara ya kwanza niliteseka sana kwa kunyweshwa usaha wa motoo na miba ya samaki nikatamani kufa lakini huko haufi cha moto utakiona kuna mashekhe mahostadhi mapadri wachungaji yani mtu anatwangwa kwenye kinu watu wapatao elfu tatu wamejazwa kwenye kinu hiko wakiwa wanatwangwa hiyo michi ni unene wa mbuyu nikapita kwenye daraja la moto na kushuhudia watu wakiteseka nikafika mbele ya markia baada kuniona tu akanyanyuka kutoka kwenye kiti na kunifata baada kunifikia akaniwasha zinga la kofi mpaka nikayumba na kuinama kama haitoshi akanishika na kuninyanyua ile anataka kunipiga kofi lingine nikamdaka mkono wake na kumchapa kofi yeye kitendo cha kumpiga tu gafla kuzimu kukatikisika kama kimbunga hivi kila kiumbe kikashangaa khaa! hata malkia hakutegemea kufanya kitendo kile akaamrisha nikamatwe nikachumpa na kwenda mbiio mpaka kwenye kiti cha malkia na kuishika fimbo yake akapiga kelelee “hapanaa usishike hiyo, nikajifanya sijasikia nikaibeba kwa mkono wa kushoto kama haitoshi nikakichukua na cheni yake tokea niwe kuzimu hata siku moja sijawai kumuona akiivaa kumuonyesha ya kwamba mimi ni noma nikaivaa baada kuivaa tetemeko la ajabu likatokea kila kitu kikawa kinayumba na wengine kupeperushwa kwenda sehemu mbali mbali aliyepeta nafasi akashikilia sehemu ni tetemeko lililo ambatana na upepo mkali sana nikajikuta nasema “achaa...gafla kila kitu kikatulia na kuwa shwali dahaa kutoka chini ya ardhi likaibuka zinga kiumbe joka si joka dragon si dragon sijui yukoje kila kile kiumbe kikahofia, baada kupanda juu zaidi huku macho yake yakizunguka kama bahari akapumua na kutua moshi mzito mweusii akamtizama kila mmoja wetu mwisho akanikazia macho mimi akanitizama kwa muda na kuanza kucheka “hahahaha!hahahaha! wewe ndio Hafidhi j ikram?"
sikuweza kufahamu ananiuliza au ananizihaki nikabaki kumtumbulia mimacho tu, “nakuuliza kijana wewe ndio Hafidhi j ikram au?"
ndio mimi kwani vipi?" jibu swali kijana sio kuuliza maswali, “wewe ni kama nani unaniuliza maswali?"
oky kijana huu sio muda wa kubishana cha umuhimu nataka nikwambie kitu kimoja ya kwamba katika dunia hii kuna viumbe vingi sana tena vya ajabu ila muumba wa vyote ni Mwenyezi Mungu sasa basi kila sehemu ya nchi au kitongoji lazima kuwe na kiongozi wa kuongoza eneo lile japo wengine wanatawala kimabavu au kwa kutumia rushwa ili apate uongozi sasa basi huku kuzimu kiongozi mkuu ni mimi hii kasri yote ni yangu na huyu binti ni binti yangu mimi ndio nimemkabizi madaraka haya ila inavyo onekana ni mzembe sana mpaka umemnyang'anya cheo ninacho kuomba muowane uwe mfalme na yeye awe malkia sawa kijana?" nikajikuta naitikia “sawa mkuu ila sio kwa sasa niache kwanza niende duniani nikaifanye kazi moja tu kisha nitarudi kufunga ndoa na malkia, “sawa kijana waweza kwenda, nikapotea gafla na kujikuta nipo ndani ya chumba nilichopanga nikajipumzisha kwa kulala nikaja kustuka baada kusikia mlango ukigongwa kwa fujo sana “ngoo,,ngoo,, nikajinyanyua kiuvivu na kwenda kufungua gafla nikasukumiziwa ndani na kujikuta nayumba kabra ya kwenda chini kumcheki aliye nisukumiza ni,,,,,
Sikuweza kuamini macho yangu baada kumuona ni mama yangu mzazi akaja kunivamia pale chini na kuitaji kunipa denda nikaugeuza uso wangu na kuishia kunilamba shavuni akanishika kichwa changu na kunigeuza akiitaji tunyonyane denda kilazima kama haitoshi akaivua blauzi yake na kubaki na sidilia tu nayo akajiandaa kuifungua nikazidi kuchanganyikiwa nikajiinua na kumsukumizia pembeni nikaanza kumfokea
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni