TUPEANE (29)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA
Watu wakabaki kuduwaa tu kama haitoshi akataka kumchinja mwingine ikabidi watu wamzuie na kuanza kumshushia kipondo ajabu hii nikabaki kuangalia kiwiliwili cha yule Mama aliyechinjwa nikakumbuka tukio zima la jana usiku
Baada kumchinja Nipe nikupe.
SASA ENDELEA...
Hasira zikaanza kunijia nikakunja ndita na kwenda kumsogera mmoja kati ya wachawi nae alipoona namfata akataharuki na kuanza
kupiga kelele
“Nisamehee jamani nakufa miee nisamehee kila mmoja akabaki kushangaa
Kumbe hakuna binaadamu wa kawaida aliyeweza kuniona zaidi ya wale wachawi nikaanza kutembeza bakora ya moto kwa kila
Mmoja hapa naomba
Niseme kile ambacho niliahidi kusema kuhusu.
Dawa ya kumuona. Mchawi mtaani kwenu.chukua mti wa mbaazi pakaa na dawa inayoitwa Kamundu kisha usiku weka hiyo fimbo ya mti wa mbaazi begani utaona maajabu ya wachawi wanavyokuwa hasa usiku.
Angalizo kwako
Kumbuka uwe na nguvu ya ziada maana mchawi akigundua umemjuwa atafanya kila njama akupoteze jaribu na uwone!"
Sikutaka kuwaonea huruma hata kidogo nikazidi kuwachapa tu.
huku nao wakizidi kupiga kelele za kuomba msamaha.
Nilikuwa kama vile nimeweka pamba masikioni na kufumba macho sikuhitaji kuwa na huruma kwa watu kama hawa.
Wananchi wakabaki kushangaa kila mmoja akahofia na kusogea mbali na eneo lile.
Wakabaki kujiuliza tu hawa wachawi
Vipi mbona kama vile wanachapwa!"
Mwingine akajibu labda atakuwa mkuu wao ndio anawapa. Adhabu kwa kuvunja
Masharti kwa kile kipigo nilichokitoa sizani kama wakiwa hai
Watakubali kuendelea na
Uchawi nikaondoka eneo hilo baada polisi kufika. Na kuwachukuwa wachawi wale japo wananchi walitaka kuwauwa.
Nikarudi zangu nyumbani nikiwa sina raha kabisa taswila ya picha ya Kaka ikinijia
huku tukio zima la Jana usiku likizunguka kwenye kichwa changu. Nikiwa nimekaa kibarazani nawaza na kuwazua nikastushwa na sauti ya Mama akiniita Latifa mwanangu!"
Nikainua uso wangu kumtizama mchozi ukanidondoka
ikabidi akae chini na kunishika begani akaniuliza
“Latifa mwanangu vipi unaumwa au?"
Nikamtizama kwa sekunde kazaa usoni kisha nikamjibu.
“hapana Mama siumwi ila nimewakumbuka tu ndugu zangu Wazazi wangu!"
Mama nae akanitizama kwa masikitiko makubwa na kusema.
“Ni kweli nafahamu ni jinsi gani unavyojisikia vibaya kukaa mbali na familia yako Latifa kumbuka wewe nakuchukulia kama mwanangu wa kukuzaa ijapokuwa katika maisha yangu sikuwai kupata. Mtoto wakike naitaji uendelee kuhishi hapa nyumbani ila kwa uzuni uliyokuwa nayo naitaji nikupe nauli ili uende kuwaona Wazazi wako!"
ile kauli ya Mama ikanifanya nitabasamu kwa mbali na kujuwa kweli mchezo umekwisha.
Hatimae siku kama tatu hivi zikapita nikiwa nishapanga kuicheza ishu Mimi na Figisu yani Mimi nitarudi kwenye umbo langu Figisu atakuwa kama Shemale yani aondoke kama Latifa.
Mie nibaki kama Hafidhi mwenyewe ili maisha yasonge.
Siku hiyo nilikuwa nimekaa kibarazani na
Grace tukipiga story mbili tatu.
Nikamuuliza swali
“hivi Grace katika maisha yako mpaka sasa umefanya kazi wapi na wapi?"
“Mmh! sijui hata nikujibu nini Latifa shogaangu maana maisha yangu yamejaa majanga tu
kila siku yanazuka mapya
yani mpaka sasa nimefanya kazi kampuni kama tano hivi nafanyiwa zengwe naacha au naachishwa kuna kampuni moja ya kutengeneza mabati.
Ipo kule tazara basi nakumbuka nilipoenda kuomba kazi ilinibidi nitoe rushwa ya ngono ndio nikaajiliwa.
Ajabu baada kufanya kazi kwa miezi kazaa tu.
Nikabambikiwa kesi ya wizi. Nikaenda kufungwa jera miezi sita!"
Nikajikuta nasema duhuu
“ina maana Grace ushawai kufungwa jera sio?"
“ndio nilifungwa pasipo kutenda kosa lolote lile
nikaja kutoka kama Mungu vile kuna Mwanaume akatokea kunipenda akatangaza ndoa namie sikuwa na hiyana nikakubali kila kitu hatimae nikaolewa. Maisha ya ndoa wapo wanaosema ni matamu nami nikatamani kuuwonja huo utamu
Kumbe sivyo nilivyozania
Baada kupita miezi sita tu ndoa ikawa kama bigijii iliyoisha utamu na kuitaji kutemwa Mwanaume yule akaanza visa kila kukicha kunipiga kama vile Mimi nimekuwa ngoma.
Mtoto wa kike nikachoka maisha ya kupigwapigwa sijayazoea mie
Nikarudi nyumbani kwetu hivi nikwambiavyo ndoa ya tatu sasa naachika nasemekana mie tasa sizai!"
Baada kusema vile Grace
akaanza kulia sikuwa na budi
kumbembeleza kumbe hakujuwa kama wachawi washafanya yao.
Nikamwambia kitu kwa kumuuliza
“Grace je iwapo ikatokea Kaka yangu akaja kujitambulisha kwenu akuowe je utakubali au?"
Kabla ya kujibu akanitizama tu!"
“Grace nijibu basi!"
“ndio nitakubali kwa nini nikatae wakati naishi moyo mpweke japo nahisi sitoweza kudumu kwenye ndoa hiyo sababu ya utasa wangu!"
Hakika nilimuonea huruma sana Grace sikutaka kumuacha ateseke na njia pekee ni kumuowa.
“Grace kama upo Tayari basi jiandae kumpokea Kaka yangu nitaenda kumwambia leo hii na je upo tayari kubadirisha dini kutoka ukristo uje kuwa Muislamu?"
Akajibu ndio niko tayari hata sasa hivi!
Basi siku ya siku ikafika ya Mama kunikabizi nauli ili niweze kwenda nyumbani kwetu Mtwara.
Wakanisindikiza hadi ubungo Mama akazidi kunisisitizia
“Latifa mwanangu kwanza kabisa nakutakia safari njema Allah (s.w.t)
Akufikishe salama salimini wasalimie sana wazazi wako ila nakuomba chondechonde usitusahau kuja kututembelea!"
Nikaitikia tu sawa hapa nikaitaji kucheza mchezo yani kama vile kiini macho tu nikakumbatiana na figisu na kuchenji maumbo yetu nikatoka katika
Ushemale na kurudi katika umbile langu
Figisu ndio akawa Shemale ila anauwezo wa kujibadirisha mbele ya safari huko. Tukarudi nyumbani
Nikiwa nina furaha ajabu kila kitu sasa kimekwisha
kilichobaki ni kwenda nyumbani kwa kina Grace nikatangaze nia.
Ikabidi niongee na Mama kwanza
“Mama"
“Abee mwanangu!"
“mi kuna jambo muhimu naitaji kuongea nawe!"
“ongea tu mwanangu mi nipo hapa nakusikiliza tu"
“Mi kuna binti nimetokea kumpenda naitaji kumuowa Mama!"
Ajabu Mama akaguna na kujishika mikono kichwani bila kutamka chochote kile!
Kisha akasema
“inamaana huyo Husnaty akutoshi sio mpaka unataka kuongeza mke mwingine!"
“Sio hivyo Mama Husnaty sikumpenda mmenilazimisha tu kumuowa
sasa nimeona chaguo langu sahihi naitaji kumuowa!"
“Ahaa wakati unamchokonoa mtoto wawatu mpaka ukampa mimba ulikuwa humpendi sasa unadai ohoo mmenilazimisha sasa basi
Nikiwa kama Mama yako huyo binti mwambie hakuna ndoa wewe ni Mume wamtu!"
Nikaona nitumie njia hii ili niweze kumtisha Mama kwa kumwambia
“Sasa Mama kama hutaki mi niowe Mwanamke ninaye
Mpenda mie
Kesho tu naenda Kilwa!"
Akastuka na kusema
“alaalaa wee mtoto usitake kuzua balaa
Haya mlete huyo Binti umuowe
Yani niko Tayari kukupa chochote mwanangu mpendwa staki kusikia unaenda Kilwa
Mama akaanza kulia.
Kwanza nikatabasamu na kujisemea moyoni
Ehee mambo yametiki nikatangaze nia kwa kina Grace usiku ulipotimia tukiwa sebureni tunakula Mama akaanzisha mada ya Mimi kutaka kuowa mke wa pili kwa upande wa Baba hakuwa na chakuongea zaidi ya kuniunga mkono tu. Kipembe je Husnaty atakubali
Ajabu hata yeye
akasema
“kwa upande wangu sina neno kwani nikisema hapana nitakuwa nimevunja kanuni ya dini yetu japo jambo lenyewe la ghafla binafsi nakutakia kila la kheli.
Kesho yake nikaenda kuongea na Grase sikupata shida maana mipango yote niliipanga kipindi nipo Shemale
Japo akamuulizia Latifa nikamjibu kasafiri
Nazani atarudi mwezi wa sita basi Grace akasilimu na kuwa muislamu nikampa jina la Wahida
Mshenga akatafutwa siku ambayo naowa ndio siku ambayo Husnaty anajifungua watoto mapacha wakike na wakiume hakika furaha iliongezeka siku hadi siku nikatumia nafasi ya zilezile saba za mwanzo Bibiye Wahida akashika ujauzito yani hakuamini
kama kweli ana mimba
akaenda hospital zaidi ya tatu kupima majibu ni yaleyale yeye ni mjamzito alilia machozi ya furaha akajiona ni mmoja kati ya wanawake hapa duniani
Niliweza kumaliza masomo yangu vyema nasasa ni mmoja kati ya mainjinia wakubwa tu.
Kingine namshukuru Mwenyezi Mungu wake zangu wanaishi kama ndugu au zaidi ya ndugu maana nilinunua nyumba mbili kila mmoja akae kwake wakakataa na kudai wao ni mwili mmoja.
Ewe Kaka ewe Dada Mama au Baba na wengineo tuheshimu vijiji tunavyokwenda kwani kila kijiji kina tamaduni zake na Mira zake sio kujifanya mjuwaji tu yasije kukutokea kama yaliyonitokea mie hakika niliteseka sana
Nikaumia sana leo hii kwangu imebaki kama history tu kingine tuamini Ushetani na uchawi upo ila hauna mamlaka mbele ya utawala wa Mwenyezi Mungu tupambane na Ushetani kwa kufanya ibada hii dunia ni kama njia tunapita makazi ya milele yapo Akhera
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni